Mrejesho: Nimesafiri na BAJA 250 XLR kupitia mbuga ya Mikumi, kwa niliyoyaona sipiti tena

Mrejesho: Nimesafiri na BAJA 250 XLR kupitia mbuga ya Mikumi, kwa niliyoyaona sipiti tena

JITU LA MIRABA MINNE

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2015
Posts
726
Reaction score
476
Mmehabarikaje Wandugu,

Nimerudi niliandika uzi kuomba uzoefu kwa waliozoea kusafiri kupitia Mbuga ya mikumi na mimi nilikuwa nataka kupita na Mwanandama wangu.

Niliondoka Moro saa 8 kwa speed ya MOTOCHINI 150 nilifika saa 9:30.Safari inaendelea nimefika Mwanzo wa mbuga naona amani tu, nimepata kujionea swala makundi kwa makundi, pundamilia na twiga kwa mbali huku tembo nao wakiendelea kutembea kwa kujigamba.

Safari inaendeleaa...., wakati bado nipo katikati ya mbuga ghafla kwenye kichaka nasikia kinatikisika ghafla simba kama watano wanatoka wakiwa wa damu mdomoni wakawa wananitizama watatu wakaunguruma huku wanafata usawa wangu nilichofanya ni kuongeza speed 180 kwani BAJA haina kujali BAMPS, wakatrot kidogo wakarudi zao, mbele kidogo mita 200 kwenye mti mkubwa namuona chui akiwa na swala kwenye mti.

Viumbe walionitisha ni Nyati waliopita kwa makundi kuvuka barabara, ilibidi nisisimame bali nirudi nilipotoka hadi nilipoona wamepita wote ndio nikapita speed 120, walirudi baadhi kunifukuzia lakini kwa kuwa wote mnamwelewa ndama alivyo.

Nilitaka kuzimia nimekutana na simba wawili mbele kulia na kushoto wawili katikati wameacha nafasi, nilichofanya ni kuwapita kama mwewe au kipanga hao nduli kwani wote mnajua mziki wao ulivyo.

USHAURI: Jamani ndugu zanguni, hapo mbugani sio pa kupita jioni wala usiku, mimi nimepita jioni mengi niliyoyaona sipiti tena, bora nipakie pikipiki kwenye lori, mnaotaka picha ni ngumu kupata labda ningekuwa nipo na wewe ukashuka kunipiga picha zingetokea vizuri.

HEBU TUAMBIE NA WEWE YALIYOKUKUTA, MIMI NILIPATA PRESSURE SIKU 3
 
Waweza pita ila sio kwa honda xl 250r.walau kwa uchache ungekuwa na cc 400 ndo ungekuwa komfotabo halafu ni vizuri kuuma nyuma ya gari kubwa hasa mabasi maana yenyewe huwa kwa uchacje yanaenda 80km/hr
 
Minaona kilicho kusaidia ni mwendo wa MOTOCHINI Tofauti na hapo ingekula kwako
 
Nilijuta sana unaweza kuzimia ukimwona simba nilikuwa nadrive huku nawaza zile documentary za WILD LIFE simba alivyokuwa anamrukia nyati hadi leo sijarud DAR nawaza nirudije
 
Sheria ya kupita mbuga za wanyama ni spidi hisiyozidi 50km per hour hivyo unatakiwa ushtakiwe kwa kuvunja sheria
 
Mwongo mkubwa wewe! Mimi ninauzoefu wa kupitia hapo mikumi karibu kila wiki huu upuuzi ulioandika hapa sijawahi kuona. Eti ukasikia na kuona kichaka kikitikisika na simba wametokea na damu mdomoni! Unawezaje kusikia wakati umevaa helmet na pikipiki inaunguruma? Na wakati huo ulikuwa unaendesha umeangalia wapi , mbele au mbugani? Kwa speed ya 150 unaweza kuona huo utumbo ulioandika hapo?

Mwongo wewe.
 
Back
Top Bottom