Mmehabarikaje Wandugu ,
nimerud niliandika uzi kuomba uzoefu kwa waliozoea kusafiri kupitia Mbuga ya mikumi na mm nilikuwa natska kupita na Mwanandama wangu ,
niliondoka Moro saa 8 kwa speed ya MOTOCHINI 150 nilifika saa 9:30
safar inaendelea nimefika Mwanzo wa mbuga naona amani tu ,nimepata kujionea swala makundi kwa makundi,pundamilia na twiga kwa mbali huku tembo nao wakiendelea kutembea kwa kujigamba
safari inaendeleaa....,. wakati bado nipo katikati ya mbuga ghafla kwenye kichaka nasikia kinatikisika ghafla simba kama watano wanatoka wakiwa wa damu mdomoni wakawa wananitizama watatu wakaunguruma huku wanafata usawa wangu nilichofanya nikuongeza speed 180 kwan BAJA haina kujali BAMPS,wakatrot kidogo wakarud zao,mbele kidogo mita 200 kwenye mti mkubwa namuona chui akiwa na swala kwenye mti,
viumbe walionitisha ni Nyati waliopita kwa makundi kuvuka barabara ilibid nisisimame bali nirud nilipotoka hadi nilipoona wamepita wote ndio nikapita speed 120 lakin walirud baadhi kunifukuzia lkn kwa kua wote mnamwelewa ndama alivyo ,nilitaka kuzimia nimekutana na simba wawili mbele kulia na kushoto wawili katikati wameacha nafas nilichofanya nikuwapita kama mwewe au kipanga hao nduli kwan wote mnajua mziki wao ulivyo
USHAURI:Jaman ndugu zangun hapo mbugani sio pa kupita jion wala usiku,mm nimepita jioni mengi niliyoyaona sipiti tena bora nipakie pikipiki kwenye lori ,mnaotaka picha ni ngumu kupata labda ningekua nipo na wewe ukashuka kunipiga picha zingetokea vizuri
HEBU TUAMBIE NA WEWE YALIYOKUKUTA MM NILIPATA PRESSURE SIKU 3