Mrejesho: Nimesafiri na BAJA 250 XLR kupitia mbuga ya Mikumi, kwa niliyoyaona sipiti tena

Mrejesho: Nimesafiri na BAJA 250 XLR kupitia mbuga ya Mikumi, kwa niliyoyaona sipiti tena

Mengine sina tatizo nayo ila hapo kwenye speed 180 umetupiga kamba!
 
Pole sana.Nafikiri uliposhuka kwenye chombo INZI walikuandama sana.pole sana.sisi morani ni kawaida kukutana nao porini hao nduli ns mara nyingine tunapambana nao na hata kuwanyanganya mawindo yao!!!
 
uongo Mikumi hata kutembea inawezekana hadi Doma simba wa Mikumi wanakula viepe chui wanakula miguu ya kuku glowila
 
Sheria ya kupita mbuga za wanyama ni spidi hisiyozidi 50km per hour hivyo unatakiwa ushtakiwe kwa kuvunja sheria

Hiyo ni night speed. Soma vizuri vibao vyao utaona wameandika NIGHT SPEED 50KPH
 
Kama jitu la miraba minne linakuwa hivi sijui vimbaumbau wanakuwaje!
 
steph curry njoo umuone mwenzio huku..inabidi um..register kwenye ile team yetu ya rally mwakani...bwahahaaa
 
Kwa hiyo speed 150 ni uongo uliotukuka halafu ufuke humps kwa mwendo huo utakua mzima wewe
 
Wewe ni mwongo kupindukia maana habari ilivyonioongo mtupu.

Hizo ni fix za kitoto sana, hakuna hicho kitu. Nimeshafanya kazi porini miaka, nimefanya census + road count..hako ka-movie noo punguza kidogo. Si kweli hata kdg
 
Wewe ni mwongo kupindukia maana habari ilivyonioongo mtupu.
Umeona eh? maana hiyo speed aliyokuwa anatumia na hayo matukio yaliyotoke ni vigumu kuvihusisha! utumie pikipiki 150km/h ugeuze shingo kuangalia simba,kichaka mtikisiko,nyati mvuka njia wacha wee!
 
Mmehabarikaje Wandugu ,
nimerud niliandika uzi kuomba uzoefu kwa waliozoea kusafiri kupitia Mbuga ya mikumi na mm nilikuwa natska kupita na Mwanandama wangu ,
niliondoka Moro saa 8 kwa speed ya MOTOCHINI 150 nilifika saa 9:30
safar inaendelea nimefika Mwanzo wa mbuga naona amani tu ,nimepata kujionea swala makundi kwa makundi,pundamilia na twiga kwa mbali huku tembo nao wakiendelea kutembea kwa kujigamba
safari inaendeleaa....,. wakati bado nipo katikati ya mbuga ghafla kwenye kichaka nasikia kinatikisika ghafla simba kama watano wanatoka wakiwa wa damu mdomoni wakawa wananitizama watatu wakaunguruma huku wanafata usawa wangu nilichofanya nikuongeza speed 180 kwan BAJA haina kujali BAMPS,wakatrot kidogo wakarud zao,mbele kidogo mita 200 kwenye mti mkubwa namuona chui akiwa na swala kwenye mti,
viumbe walionitisha ni Nyati waliopita kwa makundi kuvuka barabara ilibid nisisimame bali nirud nilipotoka hadi nilipoona wamepita wote ndio nikapita speed 120 lakin walirud baadhi kunifukuzia lkn kwa kua wote mnamwelewa ndama alivyo ,nilitaka kuzimia nimekutana na simba wawili mbele kulia na kushoto wawili katikati wameacha nafas nilichofanya nikuwapita kama mwewe au kipanga hao nduli kwan wote mnajua mziki wao ulivyo
USHAURI:Jaman ndugu zangun hapo mbugani sio pa kupita jion wala usiku,mm nimepita jioni mengi niliyoyaona sipiti tena bora nipakie pikipiki kwenye lori ,mnaotaka picha ni ngumu kupata labda ningekua nipo na wewe ukashuka kunipiga picha zingetokea vizuri
HEBU TUAMBIE NA WEWE YALIYOKUKUTA MM NILIPATA PRESSURE SIKU 3
Bwana msema uongo mchana kweupe tuambie hiyo pressure ya kupanda au kushuka?na ilikupata baada ya kumaliza safari yako au ukiwa mbugani na ulitibiwa haospitali ipi huku ukiambatanisha na copy ya cheti!jitu ongo hiliwala halioni haya!
 
Nahisi wakati umesimama tumbo lilianza kupiga miayo na ulikuwa kias flan hv unaangalia life saving tree in case maji yamezid unga ! Congrats kwa ujasiri huu.
 
Yaani unapita speed 150 na unaweza kuona simba ana damu mdomoni!!

Halafu ni nadra sana kuona wanyama hao wote ukiwa unapita Mikumi.

Ila poa tu ngoja tumeze!!

Umeniwahi mkuuu kusema hiloo ahahahaa
 
Kabla ya kuingia mikumi hapo mwanzoni kuna sehemu ya kuchimba dawa na mabasi mengi husimama, ingekuwaje kama ungesubiri basi lipite hlf ulifuate kwa nyuma???
japo stoi yaonekana fiksi. lakini kufuata basi pia ni hatari mfano. bsi likikuta kundi la nyati litasimama na wewe lazima usimame. haya mabasi yanaharaka hivyo hilo basi litaanza kupush mdogomdogo kati ya kundi mana haliwezi kaadakika nyingi kama kundi kubwa. wewe utafanyaje UTAJITOSA mwendo kwa speed ya binadamu kutembea kulifuata basi likipasua kundi la nyati. SUBUTU Kama hujakutana na nyati menye mtoto harafu katoto kake kajisogeze kwako
 
Watanzania wakati mwingine jamani tujifunze kucheka; this is just funny as hell!! Tunachukulia vitu too serious...

635443339454949826ManLaughingbw.jpg
 
Back
Top Bottom