Mrejesho: Nimesafiri na BAJA 250 XLR kupitia mbuga ya Mikumi, kwa niliyoyaona sipiti tena

Utakuwa ni mtu mwenye bahati kuona wanyama wote hao kwenye mbuga ya mikumi. mimi nimeshapita kwenye mbuga hiyo karibu mara ishirini, mchana jioni hata usiku wanyama nilioona tena kwa kujiona kuwa nina bahati ni swala, twiga na tembo. Zamani kidogo nilishawahi kuona viboko kadhaa kwenye dimbwi fulani hivi ila mbuga hiyo ya mikumi kwa anayepita barabarani kuona simba au chui nadhani anafaa kuingia kwenye orodha ya watu wenye bahati. kwa mbuga kama serengeti na manyara sio tatizo.
 

Mkuu! Inawezekanaje uwe katika 150km/h kwenye pikipiki, umevaa helmet na uweze kusikia kichaka kinatikisika? Ni kichaka kikubwa kiasi gani na huo mtikisiko ulikuwa na kelele kiasi cha kuuzidi muungurumo wa pikipiki na upepo unaovuma!
Nina mashaka na hii stori yako
 
teh teh teh..karibu univunje mbavu kwa kucheka mkuu. usije fanya kosa hilo tena kupita mikumi na tukutuku utakua kitoweo
 
we jamaa ni muongo sijapa ona mimi naijua mbuga ya mikumi vizuri ni nadra tena nadra sana tena sana kupita kiasi kukuta na simba barabarani na most simba wanavuka barabara saa moja moja au mbili na alfajili, pili chui wa mikumi wapo juu kabisa kule kwenye miyombo coz ya kuwainda kirahisi.
sasa huo upuuzi unao tueleza hapa tafuta wengine wa kuwaongopea.

unapo danganya watu wazima tunao ijua hiyo mbuga nnje ndani uwe makini na details zako.


 
Hayajawakuta tu wandugu mm nimepita saa 11kama na 30 ni hatari unaweza kuzimia kweny pikipiki
 
mbona kama ni hadithi ambazo tulikuwa tunasoma na kusimuliwa kutoka katka kitabu cha wagagagigikoko enzi za shule ya msingi?
 
Hahahah we jamaa umetunywesha chai walahi.....

Mikumi hii hii???

hivi we mama unajua ushaanza kuzeeka?dalili kuu ya kuanza kuzeeka ni kupenda kuchunguza kama ulichoambiwa ni kweli au lah!!!yaani wewe siku hizi kazi yako kuu ni kuchunguza thread za chai na kahawa kutwa kuchwa!!!

wenzako thread za chai tunazifurahia kichizi,thread ikinyooka inatukera tunaona bora tushinde kulekule jukwaa la siasa!dont be too serious mama life is easy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…