Mrejesho: Safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa Katavi - Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4

Nasubiria inspiring story...
 
Wakuu natumaini mnaendelea vyema,
Napenda kusema hili kwenye wengi Kuna mengi. Nilichojionea hapa Jukwaani Kuna watu Wana comment mengine ni kucheka tu na kuya angalia yalivyo na kuyaacha. Wewe kama kijana ukiamua kupambana pambana.

Tunaendelea tuliopo ishia........
Maisha ndani ya IGONGE yakaendelea, kumbuka baada ya lile sekeseke la yule bubi likiwa limekwisha akaondoka, lakini moyoni nikabaki najiuliza uyu Bibi ameamua kutoa kauri hiyo pengine Kuna jambo atafanya, lakini Kwa kuwa na Mimi nilienda kujitafuta na nikielewa Changamoto kama hizo zinatokea nikasema Kwa Hali yoyote nitapambana nae sio kupiga bali nitamshinda Kwa njia njingine. Nikisema ivyo wakubwa mtaelewa, watato hawatanielewa. Basi ndugu zangu nikaendelea kuchapa kazi.
Kumbuka wakati huo nipo Kwa jamaa yangu Kasukari na yeye pale alipokuwa amekita kambi halikuwa eneo lake alipewa nyumba na kijana wa yule Mzee alienikodishia SHAMBA akae, maana yale maeneo ni kama wote walioko pale ni familia Moja ya yule Mzee. Yule Mzee alikuwa ameoa wanawake watatu na wote na wote alizaa nao, kwaiyo anawatoto wengi wa wanawake totauti tofauti na Jumla ya wototo wake wanafikia 35,Kwa wale wanawake walioachana na akaoa tena bi mdogo ambae anaishi nae sasa pia amezaa nae watoto wawili Jumla ya watoto 37 hayo ni maelezo ya yeye mwenyewe aliniambia. Kwaiyo vijana wake wote hao wanaishi humo , Kila kijana alimkatia eneo lake na wote wanakaa humo, na mabinti zake pia wengine wameolewa humo humo na wanaishi na waume zao humo.

Kumbuka maisha yakaendelea naamka alfajiri naenda shamba kusafisha mchana narudi Kwa Jamaa yangu Kasukari, lakini nikawaza mbona nitaangaika sana, maana kutoka Kwa kambi ya Kasukari kwenda shambani kwangu ilikuwa ni nusu saa tu unafika shambani kwangu lakini niliona kabisa mvua zikianza kuonyesha Nita fell kabisa, maana kule shambani hakukuwa na nyumba yoyote ni mashamba tu, kwaiyo nikawaza lazima nijenge camp yangu huko shambani. Kitu kingine kilichonifanya nipate Mawazo ya kujenga camp yangu, maana baadae nilikuja kuona tutakapo elekeza jamaa yangu Kasukari tutakosana maana kumbuka jamaa hakuwa na mke kwaiyo sometimes unatoka SHAMBA unanjaa unakuta jamaa amefunga geto na haujui aliko na anarudi time zimekwenda wakati huo wewe una njaa ya kufa mtu, akirudi ni story ndefu sana. Maana nilikuja kuelewa hakutaka kunipa funguo za geto, siunajua for the first time mtu kukuamini ni ngumu hadi akujue vizuri, kwaiyo Kwa Hali Ile niliona Malengo yangu hayata timia.
Kazi ya kusafisha SHAMBA ikamalizika, kumbuka hapo nilipiga kazi wiki mbili tu SHAMBA likawa kama kiwanja Cha Mpira, watu walikuwa hawanielewi kabisa, wengine wanasema anavuta bangi, lakini nikitu ambacho sijawi kutumia kabisa maishani yangu. Nikamaliza kusafisha na nikaamua kurudi tena mwanza kwenda kujipanga kikamilifu sasa na kununua Kila kitu ambacho kitafaa katika kilimo na maitaji yangu yote,na pia kwenda kumuona mkali wa tiba, kumbuka kilimo nacho kimeingiliwa, ni vita kama vita nyingine. Kumbuka tena vile vitisho vya yule bibi, kwamba tutaona kama utavuna kwenye hili shamba. Kumbuka wakati huo niliwai sana maana muda wa majira ya mvua ulikuwa Bado kabisa ilikuwa ni mwezi wa nane Jua linawaka sana.
 
 
Tutaendelea sangapi tena Mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…