Mrejesho: Safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa Katavi - Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4

Uko vizuri sana, barikiwa.
Habarini za jioni wanajanvi, ni jioni nyingine tena baada ya shuruba za siku nzima, nimelejea tena tuendelee na mrejesho wangu. Lakini kuna watu humu wenyewe ni watu wa kuongea maneno ya kukatisha tamaa, ohhh mara uyu sio mkulima, mara uyu hakuna kitu.
Ngoja nikwambie ndugu yangu, kama humu tungefahamiana Kwa majina ungecheka sana, maana Kuna watu humu akitoa comment unaweza kudhani maisha ameyapatia kumbe nae bado anajitafuta na pengine bado anazungusha Cv na kulilia ajira, kumbe hajui kazi zipo lakini ajira hakuna.
Tunaendelea....... Nipo mwanza sasa baada ya kumaliza kusafishia SHAMBA na nikaona muda bado mrefu nikaamua kurudi mwanza kwaajiri ya kufanya kufanya manunuzi ya vitendea kazi lakini pia kwenda kumuona mtaalamu furani aweze kurekebisha mambo flani [emoji16],kumbuka unaingia vitani.
Basi tarehe za mwanzo wa mwezi wa tisa safari ikaanza kurudi KATAVI. Hapo mimefanya manunuzi ya Kila kitu kuanzia majembe, panga, solo pamp, madawa ya wadudu, mbegu za mahindi aina ya DK 719 TEMBO BABA LAO,dawa za magugu, maturubai kwaajili ya kambi, vyombo vya kupikia, dawa za aina mbalimbali kama Malaria, tumbo, dawa za vidonda, nyembe, sindano za viatu na nyuzi, sindano ya mkono,kumbuka kule ni shambani hakuna chereani, kwaiyo hata nguo ya kazi ikichanika nashona mwenyewe, au Farm boots imepasuka nashona mwenyewe like that wadau. Ndo maisha ya SHAMBA hayo.
Yani ni kwamba sikutaka kuwa napoteza muda kitu kidogo tu hadi niende MWESE NO4, kumbuka kule ni shambani ukiingia umeingia, maitaji kuyapata Yako mbali, Yani nilifungansha Kila kitu ambacho kingeitajika kwenye kambi yangu, kumbuka hapo nikifika ni kujenga kambi yangu kule shambani yani nikae kule shamba, maana nilifikiria mvua zikianza kunyesha ningesumbuka sana kuwa natoka kule kuja shambani pili kingine kilichonifanya kujenga kambi ni kitendo Cha Jamaa yangu Kasukari ninapotoka SHAMBA unakuta nae amekwenda shambai na tunapisha muda wa kurudi. Lakini kikubwa zaidi ni mtu ambae tulikuwa hatujazoena maana alihisi pengine ni wale vibaka wa Town kumbe Mimi Sina iyo tabia.

11.SAFARI YA KURUDI MPANDA KUTOKEA MWANZA HAWAMU YA PILI.
Basi ndugu zangu zafari ikaanza kutoka mwanza kwenda Mpanda, wakati wa kurudi nilipanda Bus ya Nyehunge Express, majira ya jioni tukaingia Mpanda, sasa nikafikiria nikisema niende Kwa Jamaa yangu yule wa hapo Town nitaangaika na hile mizigo, nilifanya kumpigia simu tu hakaja pale stand tukasalimia a nikampa na zawadi ya dagaa wa mwanza, Yani jamaa yangu alifulai sana.
Kumbuka nimefika jioni na vigari vya kwenda MWESE NO4 havipo maana yake ni kwamba Hadi kesho yake asubui, hivyo nilikesha pale stand na ndugu zangu wasukuma, Yani nyomi ya wasukuma wanahama kutoka mikoa mingine kuja Mpanda Yani ni vulugu tu Kila mahari.
Nilikesha hapo, hatimaye kukapambazuka salama. Kwakuwa Kuna vitu baadhi sikununua mwanza niliona tiaenda kununua kule, mfano misumari ya kujengea kambi, nyundo na vitu kama nyanya, vitunguu, mafuta ya maweze NK. Maana kule mafuta ya maweze yanatumika sana ukanda ule na pia Yana Bei nafuu.
Basi mnamo majira ya saa3 asubui nikawa nimaliza manunuzi yangu na nikachukua bajaji ya kwenda Hadi kule stand ya mizengo pinda kwenye ofisi za Nyehunge Express nilipoacha mizigo yangu. Tulichukua na kuelekea stand kunakopaki magari madogo ya kuelekea vijijini, nilipandisha mizigo yangu na, baada ya muda mchache gari ikaanza mwendo.
Labda niseme kwamba Yani nilifanya manunuzi ambayo Kuna vitu baadhi Hadi namaliza kilimo Kuna vitu nilikuwa navyo na niligawaia rafiki zangu kama vile Dotto Msukuma, Mfipa wa sumbawanga, ndugu yangu Kasukari na Mzee mwenye SHAMBA, hao nilio wataja utaona mbeleni ni jinsi gani waligusa maisha yangu njkaamua kuwapa baadhi ya vitu nilivyo bakiza kambini.

12.NIMEFIKA MWESE NO4 HAWAMU YA PILI TENA.
Baada ya kuwa nimefika mwese nilichukua pikipiki tukafunga mizigo kupeleka Kwa yule Jamaa niliefikia mara ya kwanza wakati namsubiri Jamaa yangu Kasukari kuja kunipokea, kama unakumbuka mwanzo siku nafika Mwese mara ya kwanza. Basi tutafika Kwa uyo jamaa nikamkuta, kwakweli pia ni poa sana, baada ya bkufungua mizigo nilitoa mfuko wenye dagaa kilo Moja na mafuta ya maweze Lita Moja na chumvi nikamkabidhi mke wake. Yani walifurai sana, sometimes unajiongeza Ili kujenga URAFIKI,sio unakaa kaa tu kama kama mzoga.Kumbuka wakati naanza safari ya kutoka kule Mpanda nilikuwa nawasiliana na Jamaa yangu Kasukari kwamba atakuja kunipokea na kunisaidia mizigo kushusha kule IGONGE na nilimwambia ningempa chochote na alikubali lakini kitu cha kushangaa nilipofikia nikipiga simu haipatikani hapo imefika sa kumi na moja na nusu, alafu kumbuka kuelekea kule unapita msituni ingawa hakukuwa na wanyama wanaodhuru. Basi nikaona uyu jamaa pengine amekwama kuja hivyo nikapangua zile mizigo miepesi nikafunga na begi langu mgongoni na Toch Kali yenye mwanga safari ikaanza wakati huo Nina redio yangu nikipiga wimbo wa Rose mhando.... Woga ndo umaskini wako mwanangu.. malengo yako utakamilisha vipi we kijana... Kila kitu unasema uwezi uwezi.. kwani wengine waliweza vipi we kijana... Kutwa kucha unashindana na Jua, Jua likisogea na we unasogea.... Kivuri kikisogea na we we unasogea... Umeshindwa kupambanua nyakati we kija... Jifunze Kwa walio fanikiwa kijana Umejiloga mwenyewe ehheeeeeeee... Tantalilaaaaaa.. tintiiiiiiiiiii.... Tantalilaaaaaa.. tintiiiiiiiiiii.
Hatimaye nikafika Kwa ndugu yangu Kasukari, nikakuta amefunga geto naona alikwenda pia shambani, maana alikuwa amelima maharage ya bondeni ambayo wanamwagilia kutumia mifereji kutoka kwenye mto. Basii muda si mrefu akawa amefika na akaanza kuniambia Mwamba!! Yani nilishishindwa kuja nilikuwa napulizia sumu ya wadudu kwenye maharage pole sana Mwamba. Namimj hakuna shida, nikamwambia Jamaa yangu chukua mazaga humo upike kwani maana Mimi nimechoka, ilibidi nimpe dagaa na viungo vyote apike na pia nilimpa dagaa kilo Moja na mafuta yake kama zawadi yake, kumbuka baada ya muda wa wiki kadhaa mbeleni niliamia kambini kwangu na niliondoka na mizigo yangu na zile dagaa nilizo mpa ilikuwa ni mboga yake baada ya kuondoka pale, hivyo nilimwambia hizo dagaa zake atunze tu maana yake ni kwamba tungekula dagaa zangu Hadi naondoka pale kwake nilikuwa na dagaa wengi sana.
Tulimaliza kula na kujiegesha , maana yake Ile sio kulala Yani unaamka asubui mbavu zinauma kinoma, kumbuka kitanda Cha miti ya mianzi juu godoro la nyasi Yani mwanaume unatakiwa ujikubali popote pale.
Kukapambazuka salama lakini kumbuka Kuna mizigo zangu zilibaki kule kijijini, hivyo Kuna wajukuu wa yule Mzee Yani ni watoto wa vijana wa yule Mzee, kwaiyo niliongea na baba yayo nikachukuwa vijana wawili tukapandadisha kijijini. Nikisema kupandisha acha kushangaa[emoji3064][emoji3064] ndio lugha inatumika kule mashambani, utaskikia oya Mwanangu unapandisha kijijini? Na Mimi ndio ngoja nikuagize chumvi na kiberiti Kwa GAMA. Uyu Gama ni jamaa Mangi mmoja maarufu sana pale kjjijini Yani uwezi kwenda kwenye Duka lake ukakoswa kitu Yani hata pilipili utaipata anauza na Huduma zote za miamala ya kifedha Kijiji kizima Hadi vijiji vya jirani wote ni Pale. Anauza Jumla na reja reja, Yani anapiga pesa ni balaaa.
Basi ikabidi niwape pesa wale madogo tukapandisha kijijini, tulifika nikawapeleka kwanza mgahawani kunywa chai Yani madogo walivyo rudi walikwenda kusimulia makwao, maana chai ni kitu hadimu kule mashambani. Baada ya kumaliza kupata chai tulienda kuchukua mizigo na safari ya kurudi ikaanza, kabla ya hapo tulipotoka kupata chai tulikwenda Kwa uyo Mangi mwenye duka Ili kwamba niweze kuweke Salio la kutosha kwenye simu yangu ime vyepesi kuwa nanunua muda wa maongezi juu Kwa juu maana kule hakuna vocha na pia niliweka Salio la M PESA Kwa kunilaisishia kuwa nalipia mtambo wangu wangu Solar kutoka kampuni x maana niliununu Kwa mkopo unalilipia kidogo kidogo. Niliuchukua Kwa ajiri ya Matumizi ya kambini kwangu, kuchaji simu na kupata mwanga. Kumbuka kule hakuna umeme.Safari ya kurudi shambani iliwadia na wale madogo Kila mtu amebeba Mzigo wake na tukafika salama Kwa jamaa yangu Kasukari.
 
Mkuu mi naomba connection ya huyo mtaalamu kama yuko vizuri haswa.
13.KAZI YA KUANZA KUJENGA CAMP KULE SHAMBANI KWANGU.
Wadau baada ya kuwa tumefika na mizigo yetu na wale madogo, ilikuwa ni siku ya Mimi kuandaa vitu flani ambavyo nilipewa na mtaalamu wangu na sikutaka jamaa yangu ajue chochote kuhusu ilo ila niliambiwa Hadi nifanye ilo jambo kule shambani ndio nianze kazi Yani Kwa ufupi nisifanye chochote kule shambani hadi niakikishe SHAMBA limekuwa na walinzi wa Babu, nikisema ivyo wakubwa mnaelewa na kazi iyo ilitakiwa nisifanye majira ya alfajiri sana Yani watu hawaja amka na utakiwi kuongea na mtu hata kama umekutana nae Kwa bahati mbaya.
Nashukuru zoezi nilimaliza na kazi ya ujenzi wa kambi ukaanza.
Siku iliyo fuata baada ya kumaliza lile zoezi nilienda SHAMBA nikiwa na panga, jembe na vifaa vingine kwaajiri ya kwenda kuchora ramani ni wapi nitaiweka kambi yangu na pia kuanza kukata miti na kuchimba mashimo na kusimika miti ya nguzo. Swala la miti halikuwa tatizo maana humo humo kwenye SHAMBA la Mzee kulikuwa Kuna miti kwenye Yale mashamba ambayo hayajalimwa kwaiyo unajikatia tu. Hivyo baada ya kuchora ramani ya kambi yangu ni wapi itakaa nilianza survey ya kuzungukia miti mizuri ambayo ingefaa kama nguzo nilifanikiwa kupata miti mizuri na imara kwaiyo nilikuta na kukusanya pamoja na kuanza kusomba kusogeza pale site ambapo nitajenga camp yangu.
Kwa siku iyo nilikamilisha kazi iyo ya kukata miti, maana haikuwa ni miti mingi ilikuwa kama ishirini hivi kwani ukubwa wa kambi yangu ikiwa ni chumba na sebule lakini vidogo tu sio vikubwa sana, Pia nilimptaia kazi jamaa mmoja Mfipa wa sumbawanga kazi ya kunikatia MIANZI ambayo ningetumia kuzungushia pembeni na kupiga juu Kwa kutumia misumari.Mlio Kaa shambani mtaelewa miti ya mianzi, Kumbuka sikutumia kamba maana nilikuwa nime nunua misumari kilo mbili mchanganyiko kulingana na Kila kazi. Nilimaliza kukata miti na kusogeza na nikarudi magetoni kwenda kurekebisha msosi Ili kwamba saa tisa nirudi kuendelea na kazi ya kuchimba mashimo na kusimika nguzo.
Around saa Tisa nili Rudi shambani Ili kunza kuchimba mashimo na kuweka nguzo wakati huo yule Mfipa wa sumbawanga anakata mianzi na watoto wake wanasogeza, uyo jamaa nilimkubali na nilikuwa Nampa kazi zangu nyingi maana alikuwa na familia kubwa ya watoto kwaiyo ukimpa kazi muda mchache anakukabidhi, Yani alimuwa mtu poa sana maana na yeye ndo alikuwa ndo ametoka kuhamia pale akitokea sumbawanga. Hivyo hakuwa na sehemu ya kupata pesa na pia hakua na chakula Kwaiyo alikuwa akitegema kazi ndo apate maitaji. Alipambana jioni iyo lakini akumaliza idadi ya mianzi niliyo itaka maana niliitaji mingi sana na ingefanya kazi ya kuzungushia uzio kwenye kambi yangu. Sikutaka camp yangu ikae vibaya Yani nilitaka niwe ndani ya usalama ukizingatia kule ni maporini.
Siku iyo nilifunga kazi na kurudi nyumbani kwani Jua lilizama na Kazi tukaishia pale.

Asubui nitaendelea wadau ......Ngoja nilale.
 
Wanajanvi Salaam,

Ni matumaini yangu wanajanvi mko wazima na mnaendelea na harakati za upambanaji wa kutafuta mkate wa familia.

Napenda kuleta mlejesho wangu kuhusu safari yangu ya kwenda Mpanda kufanya kilimo Cha mahindi.
Wadau kama mnakumbuka mwaka jana nilileta Uzi hapa uliosema, NAITAJI KWENDA KUFANYA KILIMO MKOA WA KATAVI. Baadhi ya wadau walitoa michango Yao ya kunitia moyo na kunipa usahuri zaidi nmna ya kufanya kilimo uko.

1. SAFARI YA KUTEMBELEA MAONYESHO YA KILIMO YA NANE NANE MWANZA KUPATA MBINU ZA KILIMO.
Ikumbukwe wakati nafikiria kwenda mkoa wa KATAVI nilikuwa nime acha kazi ambayo nilikuwa nikifanya Moja ya 5 stars Hotel uko Zanzbar, mshahara ulikuwa ni mdogo na muajiri anachelewesha kulipa na kazi ni manyanyaso na haina pumziko Wala likizo. Mkataba haieleweki Wala Nini.

Kwakweli nilikuwa nikienda kazini lakini akili yangu inawaza mbali kila uchao. Baada ya kuwa nimeacha kazi nilirudi Nyumbani na ndipo nikaanza kufikiri ni wapi nitaenda kufanya kilimo, ndipo wazo likaniijia nitakwenda mkoa wa KATAVI. Nilileta Uzi hapa jamvini kutaka kujua maoni mbalimbali kutoka Kwa wadau na kujua namna gani ya kuanza kilimo.

Ikumbukwe kilimo sio mara ya kwanza nilikuwa naanza hapana, nyumbani tumekuwa tukilima na pia kabla ya kujiingizia kwenye mambo ya ajira nilikuwa nafanya kilimo na nilianza kuona mafanikio lakini niliacha na kutimkia kwenda kuajiriwa, lakini sikuona faida ya ajira iyo.

Kwaiyo nilikwenda kulima nikiwa naamini nitaweza, maana uzoefu nilikuwa nao.

Niliamua kutembelea maoanyesho ya wakulima NANE NANE, Ili kupata kujua abc kuhusu mbegu na madawa.
Baada ya kujua mengi hapo, ndio safari yangu iliwadia kuelekea mkoa wa KATAVI.

2.SAFARI KUTOKA MWANZA KUELEKEA KATAVI.
Mnamo mwezi wa nane mwaka jana ndipo safari yangu ilianza, nilikata tiketi stand ya nyengezi katika kampuni ya NBS na atimae majira ya alfajiri safari ikaanza.

Kuhusu mwenyeji wa kunipokea kule kulikuwa na jamaa ambae tuliwai kufanya nae kazi uko Zanzbar na kwao ni Mkoa wa KATAVI na yeye pia alikuwa amecha kazi miaka mitatu iliyopita ivyo tulikuwa tuna wasiliana, japo yeye alikuwa mjini na maeneo mengi ya viijiji alikuwa hayajui lakini aliniambia Kuna jamaa anafahamiana nae yupo Kijiji cha MWESE NO4 anafanya kilimo Cha maharage.

Baada ya kuniunganisha na uyo jamaa wa MWESE niliongea nae na akaniambia maeneo aliopo mashamba yanapatika, ukitaka ambalo limefyekwa unakodi Kwa 50000,Hadi 30000. Ni maelewano tu, ukitaka upewe pori ufyeke ulime ni bure lakini kunakuwa na makubaliano baina Yako na mwenye eneo ni misimu mingapi utalima na kumuachia shamba lake.

Mazungumzo na uyo jamaa wa MWESE tuliyafanya kabla sijaondoka Rock City, hivyo alinipa abc kuhusu uko aliko.

3.NIMEFIKA TAYARI MKOA WA KATAVI.
Baada ya kuwa nimewasili salama majira ya Saa kumi na mbili jioni, nilipokelewa na mwenyeji wangu hapo mjini na kuelekea kwake, nilifurai sana kuonana na jamaa yangu ambae tuliachana kwa muda mrefu.

Usiku tulikula na kupiga story za kule zanzbar wakati tukiwa pamoja na na ndipo nilikwenda kupumzika, huku akili yangu ikiwa na shauku ya kuingia pori kuchapa kazi. Ikumbukwe wakati naelekea kule nilikuwa tayari nimebeba baadhi ya vitendea kazi na nguo nzito za bariadi pamoja na sora yangu kwaajili ya Matumizi ya kuchage simu na mwanga pia. Pia nilibeba dagaa wa kutosha mafuta ya kupikia, vitabu vya kusoma wakati nikiwa pori, radio, dawa za aina mbalimbali kumbuka ni shamba lazima uwe na Huduma kama hizo.

4. SAFARI INA ANZA KUTOKA KATAVI MJINI KUELEKEA KIJIJI CHA MWESE NO4.
Baada ya kuamka asubui tulisalimina na mwenyeji wangu na ndipo tukafanya mawasiliano na yule jamaa wa mwese, akanipa ramani ya kufika kule na akasema yeye anapandisha kutoka alipo na nitamkuta stand ya MWESE NO4 ananisubiri, kitendo Cha kuniambia ANAPANDISHA KUTOKA ALIKO. akili yangu nikajua tu kumbe uyu jamaa ayupo kijijini hapo Bali yupo pembezoni, kwakuwa nilikuwa nimeamua kujidunga sindano nilisema moyoni litakalo kuwa na liwe poa tu. Nilichojionea mkoa wa KATAVI wageni ni wengi sana hususani jamii ya kisukuma.

Sitaki kusema uongo, kama Kuna kabila ambalo nalikubali hapa Tanzania ni Wasukuma, ni jamii ambayo haina wivu Wala chuki Kwa mgeni ukifikia katika malango ya msukuma yupo tayari kukusaidia Kwa kile alicho nacho Ili wewe upate. Nitaelezea uko mbele ukalimu wa wa wasukuma.

Kutoka Mpanda mjini hadi MWESE NO4 ni kama masaa manne kufika hapo kijijini, katika hii almashauri ya wilaya ya Tanganyika Ina vijiji vingi ikiwamo center maalufu ya wakulima wa mahindi na ndipo kituo kikubwa Cha wanunuzi wa Mahindi kutoka mikoani na nchi jirani za SADEC.

Kwakweli center hiyo imechangamka sana na harakati ni nyingi. Japo vijiji ni vingi lakini sivijui vingine Kwa majina yake.

Kitu kingine kilicho nishangaza ni namna kulivyo na majina ya vijiji ambavyo vinajulikana Kwa namba, kwaiyo ukisema unaenda MWESE lazima useme unaenda namba ngapi? Kuna NO 10,NO 9 NO 8, NO 7,NO 6,NO 5,NO 4, NO 3,NO 2, na NO 1.

Na iyo namba 4 ndio Kijiji cha mwisho kinaenda kupakana na Wilaya ya uvinza Mkoa wa Kigoma.

5. TAYARI NIMEFIKA KIJIJI CHA MWESE NO4.
Kwakweli ni safari ya masaa kama manne lakini yenye shuluba kali, maana ilikuwa wakati wa kiangazi kwaiyo barabara ni vumbi kweli kweli yani unafika utamaniki kama ni binadamu, kama una roho nyepesi safari Yako inaweza kuishia hapo NO 4.

Lakini siku zote waenga walisema ukitaka Mali utaipata shambani, msemo huu ni kweli na hakika. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Wakati Niko njia nikawasiliana na Jamaa yangu wa MWESE NO4 akaniambia yeye anapandisha kutoka alipo hivyo akanielekeza kwamba nikifika hapo stand nitaulizia kwenye mji wa jamaa flani tumpe jina la Kapumputika haya ni majina ya wabende wa mkoa wa KATAVI. Baada ya kuwa nimefika stand niliuliza kwenye mji huo na ndipo nichukua pikipiki na akafunga mizigo yangu tukaelekea hapo Katika mji huo alipo nielekeze kwamba atanikuta.

Kitu kilicho nivutia katika kijijini hicho ni uwepo wa maziwa mengi, Yani kidumu Cha Lita Tano Bei ni 2000, kwakweli nilishaanga sana, Wenyeji wakasema kijijini hapo wafugaji ni wengi na mifugo Iko maporini huko. Kwakweli maziwa ni mengi sana.

5.SAFARI INAANZA KUTOKA MWESE NO4 KUELEKEA IGONGE KWA JAMAA YANGU, AMBAPO KUNA SHAMBA.
Baada ya kuwa nimefika katika mji huo nilijitambulisha na kusema nimeelekezwa na fulani, tumpe jina la Kasukari.

Nilikaa kama masaa mawili ndipo mwenyeji wangu Kasukari akawa amefika, tukasalimia na kutambulishana maana hatujuwani na hatujawai kuonana na nimemfahamu kupitia jamaa yangu yule tuliekuwa nae Zanzibar.

Kumbe uyu Kasukari nae ni mtu wa kutoka mkoa wangu japo kabila tofauti lakini katika mazungumzo tunaelewana vizuri tu.

Uyu Kasukari na yeye sio mzaliwa wa uko ila alienda tu kusaka furusa na alikuwa amejikita katika kilimo Cha maharage, mahindi na ufugaji wa kuku wa kienyeji.

Baada ya maongezi mafupi aliniambia sasa tuchukue mizigo tuanze safari, nilimuuliza vipi kama ni mbali tuchukue pikipiki, alisema mwamba!! hapa tukisema tuchukue pikipiki atatupiga bei kubwa na njia ya pikipiki ni mzunguko. Hivyo tupite short cut, lakini akaniambia mwamba!! Maisha ya uko utaweza? nilimuwakikishia Niko imara na ujio wangu sijalazimishwa na mtu, nimekuja mwenyewe kulima.

Kwakweli nilikuwa na mizigo mingi, tuligawana Kila mtu akabeba na safari ikaanza kuelekea IGONGE shambani. Tulipanda milima na kushika mabonde kama vile tuko vitani,mithili ya wanajeshi walio vitani wakiwa na mabegi mazito na siraha migongoni mwao.

Ni mwendo wa lisaa limoja na nusu tukaingia ndani ya IGONGE, uko IGONGE sio kijiji ni mashambani ambako watu wanafanya kilimo lakini makazi Yao ya kudumu Yako MWESE,japo ni kama vile niliona wengi wameshafanya makazi ya kudumu huko.Huduma zote za mahitaji mhimu hadi uende NO4 , ndipo utapata huduma za kifedha na maitaji yote uko, kwaiyo unapoingia kule Make sure umefanya window shopping ya mahitaji yote.

6.MAISHA NDANI YA IGONGE.
Baada ya kuwa tumefika IGONGE Kwa Jamaa yangu Kasukari, ni mtu ambae alikuwa anakaa peke yake maana hakuwa na mke wala mtoto, hivyo maisha yalikuwa ni ya kijeda zaidi ndani geto fulu nyasi juu na miti, wakati godoro likiwa ni la nyasi ndani yake, maisha yakaanza hapo, kweli Kuna wakati nilikuwanawaza mbona nimekuja kuteseka huku? roho nyingine inaniambia nirudi mjini, lakini nikajiambia hivi nitakuwa na akili kweli?. Nimeacha kazi kuja kulima alafu tena nirudi mjini nitafanya nini? ndipo nilisema nitapambana kufa na kupona hadi kieleweke. Yani sikati tamaa hadi mwisho.

Kesho yake asubui kulivo pambazuka sikutaka kupoteza muda nilimwambia Kasukari ni wakati sasa tufanye survey nicheki hayo mashamba Ili nianze kusafishia, ni kweli Jamaa yangu Kasukari alikuwa ni mtu muelewa sana aliniambia Kuna Mzee flani anamashamba makubwa hivyo tungependa kumuona kwake.

Lakini usiku huo niliona kwangu ni mgumu sana maana sikulala Yani panya ilikuwa ni vurugu kama vile ni panya watu, ukizubaa unaliwa kidole, kumbe ni sababu jamaa alikuwa kutunza mahindi umo geto kwaiyo walikuwa wanakimbizana kutafuta chakula maana ilikuwa ni kiangazi hivyo mashambani watu wameshavuna hakuna chakula tena. Ndo maana ilikuwa vurugu.

Mnamo saa tatu asubui safari ya kuelekea kuona shamba lifika na tukaenda Kwa uyo mzee, maana haukuwa mbali sana na Kwa jamaa yangu Kasukari . Baada ya kuwa tumewasili Kwa uyo mzee hatukumkuta, tuliambiwa na mke wake yuko shambani, tulielekea kule shambani na tukamkuta na ndipo jamaa yangu Kasukari alinitambulisha na kumueleza lengo langu la kuitaji SHAMBA, ikumbukwe Mimi sikuwa na fedha za kununua bali nilikuwa naitaji kukodi tu. Hivyo Mzee aliniuliza unataka SHAMBA la kufyeka ulime bure alafu utaniachia au unataka ambalo limeisha fyekwa tayari? ,Kwakuwa lengo halikuwa la kufyeka msitu, nilimwambia naitaji ambalo liko tayari, aliniambia bei ni elfu 70 Kwa heka.

Si unajua tena wakiona watu tumetoka town wanajua tuna ela kumbe njaa Kali.Kwakuwa Jamaa yangu Kasukari alikuwa ameniambia Bei,sikutaka kuwa mzungumzaji, yote nilimuachia Kasukari akasimamia mazungumzo na ndipo Mzee alikubali 50000/Kwa heka Moja. Baada ya kuwa tumezungukia maeneo ya uyo mzee, Kuna eneo nililipenda maana lilikuwa karibu na mto, target yangu ilikuwa ni kuweka bustani ya mboga mboga kwaajiri ya Matumizi yangu ya kambi. Hivyo nilimwambia anikatie sehemu iyo.

Basi Mzee aliniambia utaanzia hapa na kuishi kule akaweka alama, kwakweli ni kama alikadilia tu, maana Mimi niliitaji Eka mbili tu kulingana na bajeti yangu, lakini nilivokuja kupima na Jamaa yangu Kasukari zilikuwa kama ekari 3 na nusu.

Nilimpa laki Moja, hakuna Cha maandikiano mzee, kazi kazi tu.

7.KAZI YA KUSAFISHA SHAMBA INA ANZA RASIMI NDANI YA IGONGE.
Wakuu sikutaka kupoteza muda kabisa Yani ndio ivyo uelewe au usielewe, kwakuwa SHAMBA nililikuwa nimelimwa mahindi na alikuwa amemaliza kuvuna hivyo kulikuwa na vichaka vichaka maana jamii ya pale hawana utamaduni wa kuchapa kazi kwaiyo kilimo Chao ni Cha mazoea, unakuta amelima hapa, ameluka akalima pale, Yani hata kama Kuna kakichacha hana muda wa kufyeka, na kitu kingine hata shamba hawalimi ndio wakapanda, Yani wanafyeka na kuchimba mashimo na kuweka mbegu, lakini mahindi yanavyo Toka asikwambie mtu. Mahindi yanasimama sema hawana utamaduni wa kupanda mbegu Bora na kupuliza madawa ya kuuwa wadudu. Wao wanapanda zile mbegu za kienyeji ndefu lakini mahindi yanatoka tu.

Basi kazi ikaanza ya kusafisha Yani kukata vichaka na kupanua eneo kiaina, maana eneo lilikuwa ni kubwa sema upande wa kuelekea mtoni ilikuwa ni vichaka, kwangu niliona huko ndo Kuna mzigo hvyo sikutaka kuona kichaka , nilisafisha Hadi Mzee akashanga, Kwa vile sikuwa na masihara Yani ndani ya wiki moja SHAMBA likawa jeupe pee, raia wakaanza kushangaa na kuanza kumuuliza Jamaa yangu Kasukari hivi uyo ndugu Yako ni mwanajeshi ? Au labda atakuwa ni mpelelezi? Kwakuwa Mimi nilikuwa nimetumwa na kijiji, hivyo sikutaka kupoteza muda Wala mazoea yaliyopitiliza, maana tayari nilikuwa nimepata story ya jamii tunayoishi nayo,nilikuwa makini sana. Kazi ikaendelea .

8.KUFOKEANA NA MKE WA MZEE MWENYE SHAMBA NILILO KODI.
Wakuu ikumbukwe hapo ninaendelea na kazi ya kusafisha shamba. Naamka alfajiri natokea geto Kwa Kwa jamaa yangu Kasukari naenda shambani, ilikuwa ni mwendo wa nusu saa kutoka Kwa Kasukari kuja shambani.
Siku Moja nikiwa SHAMBA naendelea na harakati za kusafishia ndipo alikuja Bibi mmoja maana nilikuwa si mfahamu na sijawai kumuona, kumbe alikuwa ni mke mkubwa wa yule Mzee niliekodi kwake SHAMBA, lakini walikuwa wamesha achana na Mzee, na Mzee alikuwa ameoa bii mdogo ambae Mimi nilikuwa namfahamu.

Basi Wakuu baada ya kufika nilipo akaniuliza!! We kijana ni nani amekuruhusu usafishe Ili SHAMBA? Hapo anafoka kinoma[emoji12] nikamwambia kabla ya kunifokea tufahamiane we ni nanj ? Ili na Mimi nikupe maelezo. Dahhhh Bibi aelewi, anasema nani amekukodishia na umetoa Bei Gani? Nikaona uyu mama ngoja na Mimi nimkolomeee maana amekuja kigaidi. Basi nikamwambia sikia, kwavile umekuja Kwa shali na wewe ni mzazi wangu nimekupa heshima lakini uelewi nakuomba utoke hapa,mambo yote na majibu atakujibu yule Mzee kule, maana Mzee nae hakuwa mbali sana , hivyo akaondoka kaelekea Kwa Mzee baada ya kuona nimewasha moto.

Kumbe Mzee alikuwa anamuona wakati yuko pale shambani, baada ya kufika kule Kwa Mzee, Mzee nae akawa anamgombeza na uyo Bibi akarudi kwangu na kusema maneno haya.........Wewe kijana unajidai unajua sana tutaona kama utavuna kwenye hili shamba.

Na Mimi nikamjibu tena nitavuna sana zaidi Yako na utashangaa.

Baadae yule Mzee akaja pale shambani na kuniambia kijana usimskilize uyo ni mjinga, akaendelea kusema.. uyo alikuwa ni mke wangu mkubwa na tulisha achana na nilimgawia mashamba yake na mji wake ni ulekule, lakini bado ananifata katika mashamba yangu, Kila nikikodisha SHAMBA anataka nimpe ela. Kijana we chapa kazi Wala asikubabaishe we niangalie Mimi tu..

Itaendelea Nini kilitokea.

✅🙏🙏🙏
 
Mkuu ninakupongeza sana! Hii ni wake up call kwa vijana wanaong'ang'ania mjini wajiongeze.

Ila kwa mazingira unayoelezea vijana wengi wa mjini laini laini hawataweza labda wawe na mitaji waje walime kwa trekta na waweke vibarua. Yaani wao kazi yao iwe ni usimamizi tu! Na usishangae hata hilo wanaweza kufeli....tuna vijana wa kiume wa hovyo sana ...soft skin, weak and lazy. Kazi wanayoweza ni kuweka bundle kuponda vitu vya maendeleo kama hivi na kuchangia katika mada za celebrities wa mjini na mipira tu. Huu uzi wataupita kama hawauoni au watakuponda tu.
 
Back
Top Bottom