Mrejesho: Safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa Katavi - Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4

Mrejesho: Safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa Katavi - Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4

Mkuu we kila sehemu unataka kwenda? Ukiona mtu analeta mrejesho ujue hiyo kitu alifanya ama bado anafanya, huyu kilimo alifanya mwaka jana bila kukosea. Sidhani kama bado yuko huko Katavi akiendelea na kilimo.

We kama vipi twende sisi wawili huko tukajikite tupige heka zetu 5.
Mkuu naomba uwe mwenyeji wangu nataka kuja huko kulima pia nipo mwanza now.
 
Habarini za jioni wanajanvi, ni jioni nyingine tena baada ya shuruba za siku nzima, nimelejea tena tuendelee na mrejesho wangu. Lakini kuna watu humu wenyewe ni watu wa kuongea maneno ya kukatisha tamaa, ohhh mara uyu sio mkulima, mara uyu hakuna kitu.
Ngoja nikwambie ndugu yangu, kama humu tungefahamiana Kwa majina ungecheka sana, maana Kuna watu humu akitoa comment unaweza kudhani maisha ameyapatia kumbe nae bado anajitafuta na pengine bado anazungusha Cv na kulilia ajira, kumbe hajui kazi zipo lakini ajira hakuna.
Tunaendelea....... Nipo mwanza sasa baada ya kumaliza kusafishia SHAMBA na nikaona muda bado mrefu nikaamua kurudi mwanza kwaajiri ya kufanya kufanya manunuzi ya vitendea kazi lakini pia kwenda kumuona mtaalamu furani aweze kurekebisha mambo flani [emoji16],kumbuka unaingia vitani.
Basi tarehe za mwanzo wa mwezi wa tisa safari ikaanza kurudi KATAVI. Hapo mimefanya manunuzi ya Kila kitu kuanzia majembe, panga, solo pamp, madawa ya wadudu, mbegu za mahindi aina ya DK 719 TEMBO BABA LAO,dawa za magugu, maturubai kwaajili ya kambi, vyombo vya kupikia, dawa za aina mbalimbali kama Malaria, tumbo, dawa za vidonda, nyembe, sindano za viatu na nyuzi, sindano ya mkono,kumbuka kule ni shambani hakuna chereani, kwaiyo hata nguo ya kazi ikichanika nashona mwenyewe, au Farm boots imepasuka nashona mwenyewe like that wadau. Ndo maisha ya SHAMBA hayo.
Yani ni kwamba sikutaka kuwa napoteza muda kitu kidogo tu hadi niende MWESE NO4, kumbuka kule ni shambani ukiingia umeingia, maitaji kuyapata Yako mbali, Yani nilifungansha Kila kitu ambacho kingeitajika kwenye kambi yangu, kumbuka hapo nikifika ni kujenga kambi yangu kule shambani yani nikae kule shamba, maana nilifikiria mvua zikianza kunyesha ningesumbuka sana kuwa natoka kule kuja shambani pili kingine kilichonifanya kujenga kambi ni kitendo Cha Jamaa yangu Kasukari ninapotoka SHAMBA unakuta nae amekwenda shambai na tunapisha muda wa kurudi. Lakini kikubwa zaidi ni mtu ambae tulikuwa hatujazoena maana alihisi pengine ni wale vibaka wa Town kumbe Mimi Sina iyo tabia.

11.SAFARI YA KURUDI MPANDA KUTOKEA MWANZA HAWAMU YA PILI.
Basi ndugu zangu zafari ikaanza kutoka mwanza kwenda Mpanda, wakati wa kurudi nilipanda Bus ya Nyehunge Express, majira ya jioni tukaingia Mpanda, sasa nikafikiria nikisema niende Kwa Jamaa yangu yule wa hapo Town nitahangaika na mizigo kwenda kwake,maana kulikuwa ni mbali.Nilimpigia simu tu akaja pale stand tukasalimia nikampa zawadi ya dagaa wa mwanza, Yani jamaa yangu alishukuru sana.
Kumbuka nimefika jioni na magari ya kwenda MWESE NO4 hayakuwepo muda huo maana yake ni kwamba hadi kesho yake asubui, hivyo nilikesha pale stand na ndugu zangu wasukuma, Yani nyomi ya wasukuma wanahama kutoka mikoa mingine kuja Mpanda Yani ni vurugu tu Kila mahari.
Nilikesha hapo, hatimaye kukapambazuka salama. Kwakuwa Kuna vitu baadhi sikununua mwanza niliona tiaenda kununua kule, mfano misumari ya kujengea kambi, nyundo na vitu kama nyanya, vitunguu, mafuta ya maweze nk. Maana kule mafuta ya maweze yanatumika sana ukanda ule na pia yana Bei nafuu.
Basi mnamo majira ya saa3 asubui nikawa nimemaliza manunuzi yangu na nikachukua bajaji ya kwenda hadi kule Stand ya Mizengo pinda kwenye ofisi za Nyehunge Express nilipoacha mizigo yangu. Tulichukua na kuelekea stand kunakopaki magari madogo ya kuelekea vijijini, nilipandisha mizigo yangu na baada ya muda mchache gari ikaanza mwendo.
Labda niseme kwamba Yani nilifanya manunuzi ambayo Kuna vitu baadhi Hadi namaliza kilimo Kuna vitu nilikuwa navyo na niligawaia rafiki zangu kama vile Dotto Msukuma, Mfipa wa sumbawanga, ndugu yangu Kasukari na Mzee mwenye SHAMBA, hao nilio wataja utaona mbeleni ni jinsi gani waligusa maisha yangu njkaamua kuwapa baadhi ya vitu nilivyo bakiza kambini.

12.NIMEFIKA MWESE NO4 HAWAMU YA PILI TENA.
Baada ya kuwa nimefika mwese nilichukua pikipiki tukafunga mizigo kupeleka Kwa yule Jamaa niliefikia mara ya kwanza wakati namsubiri Jamaa yangu Kasukari kuja kunipokea, kama unakumbuka mwanzo siku nafika Mwese mara ya kwanza. Basi tukafika Kwa uyo jamaa nikamkuta, kwakweli pia ni poa sana. Baada ya kufungua mizigo nilitoa mfuko wenye dagaa kilo Moja na mafuta ya maweze Lita Moja na chumvi nikamkabidhi mke wake. Yani walifurai sana, sometimes unajiongeza Ili kujenga urafiki,sio unakaa kaa tu kama kama mzoga.Kumbuka wakati naanza safari ya kutoka kule Mpanda nilikuwa niwasiliana na Jamaa yangu Kasukari kwamba atakuja kunipokea na kunisaidia mizigo kushusha kule IGONGE na nilimwambia ningempa chochote na alikubali lakini kitu cha kushangaa nilipofika nikipiga simu haipatikani hapo imefika sa kumi na moja na nusu, alafu kumbuka kuelekea kule unapita msituni ingawa hakukuwa na wanyama wanaodhuru. Basi nikaona uyu jamaa pengine amekwama kuja hivyo nikapangua zile mizigo miepesi nikafunga na begi langu mgongoni na Toch Kali yenye mwanga safari ikaanza wakati huo Nina redio yangu nikipiga wimbo wa Rose mhando.... Woga ndo umaskini wako mwanangu.. malengo yako utakamilisha vipi we kijana... Kila kitu unasema uwezi uwezi.. kwani wengine waliweza vipi we kijana... Kutwa kucha unashindana na Jua, Jua likisogea na wewe unasogea.... Kivuri kikisogea na we we unasogea... haujui kupambanua nyakati we kija... Jifunze Kwa walio fanikiwa kijana..... Umejiloga mwenyewe ehheeeeeeee... Tantalilaaaaaa.. tintiiiiiiiiiii.... Tantalilaaaaaa.. tintiiiiiiiiiii.
Hatimaye nikafika Kwa ndugu yangu Kasukari, nilikuta amefunga geto naona alikwenda pia shambani, maana alikuwa amelima maharage ya bondeni ambayo wanamwagilia kutumia mifereji kutoka kwenye mto. Basi muda si mrefu akawa amefika na akaanza kuniambia Mwamba!! Yani nilishindwa kuja nilikuwa napulizia sumu ya wadudu kwenye maharage pole sana Mwamba. Namimj hakuna shida, nikamwambia Jamaa yangu chukua mazaga humo upike maana Mimi nimechoka sana.Kumbuka baada ya muda wa wiki kadhaa mbeleni niliamia kambini kwangu na niliondoka na mizigo yangu na zile dagaa nilizo mpa ilikuwa ni mboga yake,hivyo nilimwambia hizo dagaa zake atunze tu maana yake ni kwamba tungekula dagaa zangu Hadi naondoka pale kwake nilikuwa na dagaa wengi sana.
Tulimaliza kula na kujiegesha , maana yake Ile sio kulala yani unaamka asubui mbavu zikiwa zinauma kinoma, kumbuka kitanda Cha miti ya mianzi na juu ni godoro la nyasi yani mwanaume unatakiwa ujikubali popote na kwalolote katika maisha.
Kukapambazuka salama lakini kumbuka Kuna mizigo zangu zilibaki kule kijijini, hivyo Kuna wajukuu wa yule Mzee Yani ni watoto wa vijana wa yule Mzee.Kwaiyo niliongea na baba yao nikachukuwa vijana wawili tukapandadisha kijijini. Nikisema kupandisha acha kushanga[emoji3064][emoji3064] ni msemo ambayo inatumika kule mashambani.Utasikia oya Mwanangu unapandisha kijijini? Na Mimi ndio!! jamaa ngoja nikuagize chumvi na kiberiti Kwa GAMA. Uyu Gama ni Mangi mmoja maarufu sana pale kjjijini Yani uwezi kwenda kwenye Duka lake ukakoswa kitu Yani hata pilipili utaipata inauzwa na Huduma zote za miamala ya kifedha Kijiji kizima hadi vijiji vya jirani wote ni Pale. Anauza Jumla na reja reja, yani anapiga pesa ni balaaa.
Basi ikabidi niwape pesa wale madogo tukapandisha kijijini, tulifika nikawapeleka kwanza mgahawani kunywa chai yani madogo walivyo rudi kwao walikwenda kusimulia makwao, maana chai ni kitu hadimu kule mashambani. Baada ya kumaliza kupata chai tulienda kuchukua mizigo na safari ya kurudi ikaanza, kabla ya hapo tulipotoka kupata chai tulikwenda Kwa uyo Mangi mwenye duka Ili kwamba niweze kuweka Salio la kutosha kwenye simu yangu iwe vyepesi kuwa nanunua muda wa maongezi juu Kwa juu maana kule hakuna vocha na pia niliweka Salio la M PESA Kwa kunilaisishia kuwa nalipia mtambo wangu wangu Solar kutoka kampuni x maana niliununua Kwa mkopo unalilipia kidogo kidogo. Niliuchukua Kwa ajiri ya Matumizi ya kambini kwangu, kuchaji simu na kupata mwanga. Kumbuka kule hakuna umeme.Safari ya kurudi shambani iliwadia na wale madogo Kila mtu akabeba Mzigo wake na tukafika salama Kwa jamaa yangu Kasukari.
 
Mkuu we kila sehemu unataka kwenda? Ukiona mtu analeta mrejesho ujue hiyo kitu alifanya ama bado anafanya, huyu kilimo alifanya mwaka jana bila kukosea. Sidhani kama bado yuko huko Katavi akiendelea na kilimo.

We kama vipi twende sisi wawili huko tukajikite tupige heka zetu 5.
🤣🤣🤣 mkuu nimeona notification nikajua lazima useme haha sometimes maisha yanachanganya sana, kila sehemu unataman kwenda. TUONDOKE KAMA UPO SERIOUS MKUU.
 
M
Mkuu we kila sehemu unataka kwenda? Ukiona mtu analeta mrejesho ujue hiyo kitu alifanya ama bado anafanya, huyu kilimo alifanya mwaka jana bila kukosea. Sidhani kama bado yuko huko Katavi akiendelea na kilimo.

We kama vipi twende sisi wawili huko tukajikite tupige heka zetu 5.
Mm nitakua mwenyeji wenu
 
Habarini za jioni wanajanvi, ni jioni nyingine tena baada ya shuruba za siku nzima, nimelejea tena tuendelee na mrejesho wangu. Lakini kuna watu humu wenyewe ni watu wa kuongea maneno ya kukatisha tamaa, ohhh mara uyu sio mkulima, mara uyu hakuna kitu.
Ngoja nikwambie ndugu yangu, kama humu tungefahamiana Kwa majina ungecheka sana, maana Kuna watu humu akitoa comment unaweza kudhani maisha ameyapatia kumbe nae bado anajitafuta na pengine bado anazungusha Cv na kulilia ajira, kumbe hajui kazi zipo lakini ajira hakuna.
Tunaendelea....... Nipo mwanza sasa baada ya kumaliza kusafishia SHAMBA na nikaona muda bado mrefu nikaamua kurudi mwanza kwaajiri ya kufanya kufanya manunuzi ya vitendea kazi lakini pia kwenda kumuona mtaalamu furani aweze kurekebisha mambo flani [emoji16],kumbuka unaingia vitani.
Basi tarehe za mwanzo wa mwezi wa tisa safari ikaanza kurudi KATAVI. Hapo mimefanya manunuzi ya Kila kitu kuanzia majembe, panga, solo pamp, madawa ya wadudu, mbegu za mahindi aina ya DK 719 TEMBO BABA LAO,dawa za magugu, maturubai kwaajili ya kambi, vyombo vya kupikia, dawa za aina mbalimbali kama Malaria, tumbo, dawa za vidonda, nyembe, sindano za viatu na nyuzi, sindano ya mkono,kumbuka kule ni shambani hakuna chereani, kwaiyo hata nguo ya kazi ikichanika nashona mwenyewe, au Farm boots imepasuka nashona mwenyewe like that wadau. Ndo maisha ya SHAMBA hayo.
Yani ni kwamba sikutaka kuwa napoteza muda kitu kidogo tu hadi niende MWESE NO4, kumbuka kule ni shambani ukiingia umeingia, maitaji kuyapata Yako mbali, Yani nilifungansha Kila kitu ambacho kingeitajika kwenye kambi yangu, kumbuka hapo nikifika ni kuanza kujenga kambi yangu kule shambani yani nikae kule kule shamba, maana nilifikiria mvua zikianza kunyesha ningesumbuka sana kuwa natoka kule kuja shambani pili kingine kilichonifanya kujenga kambi ni kitendo Cha Jamaa yangu Kasukari ninapotoka SHAMBA unakuta nae amekwenda shambai na tunapisha muda wa kurudi. Lakini kikubwa zaidi ni mtu ambae tulikuwa hatujazoena maana alihisi pengine ni wale vibaka wa Town kumbe Mimi Sina iyo tabia.

11.SAFARI YA KURUDI MPANDA KUTOKEA MWANZA HAWAMU YA PILI.
Basi ndugu zangu zafari ikaanza kutoka mwanza kwenda Mpanda, wakati wa kurudi nilipanda Bus ya Nyehunge Express, majira ya jioni tukaingia Mpanda, sasa nikafikiria nikisema niende Kwa Jamaa yangu yule wa hapo Town nitaangaika na hile mizigo, nilifanya kumpigia simu tu hakaja pale stand tukasalimia a nikampa na zawadi ya dagaa wa mwanza, Yani jamaa yangu alifulai sana.
Kumbuka nimefika jioni na vigari vya kwenda MWESE NO4 havipo maana yake ni kwamba Hadi kesho yake asubui, hivyo nilikesha pale stand na ndugu zangu wasukuma, Yani nyomi ya wasukuma wanahama kutoka mikoa mingine kuja Mpanda Yani ni vulugu tu Kila mahari.
Nilikesha hapo, hatimaye kukapambazuka salama. Kwakuwa Kuna vitu baadhi sikununua mwanza niliona tiaenda kununua kule, mfano misumari ya kujengea kambi, nyundo na vitu kama nyanya, vitunguu, mafuta ya maweze NK. Maana kule mafuta ya maweze yanatumika sana ukanda ule na pia Yana Bei nafuu.
Basi mnamo majira ya saa3 asubui nikawa nimaliza manunuzi yangu na nikachukua bajaji ya kwenda Hadi kule stand ya mizengo pinda kwenye ofisi za Nyehunge Express nilipoacha mizigo yangu. Tulichukua na kuelekea stand kunakopaki magari madogo ya kuelekea vijijini, nilipandisha mizigo yangu na, baada ya muda mchache gari ikaanza mwendo.
Labda niseme kwamba Yani nilifanya manunuzi ambayo Kuna vitu baadhi Hadi namaliza kilimo Kuna vitu nilikuwa navyo na niligawaia rafiki zangu kama vile Dotto Msukuma, Mfipa wa sumbawanga, ndugu yangu Kasukari na Mzee mwenye SHAMBA, hao nilio wataja utaona mbeleni ni jinsi gani waligusa maisha yangu njkaamua kuwapa baadhi ya vitu nilivyo bakiza kambini.

12.NIMEFIKA MWESE NO4 HAWAMU YA PILI TENA.
Baada ya kuwa nimefika mwese nilichukua pikipiki tukafunga mizigo kupeleka Kwa yule Jamaa niliefikia mara ya kwanza wakati namsubiri Jamaa yangu Kasukari kuja kunipokea, kama unakumbuka mwanzo siku nafika Mwese mara ya kwanza. Basi tutafika Kwa uyo jamaa nikamkuta, kwakweli pia ni poa sana, baada ya bkufungua mizigo nilitoa mfuko wenye dagaa kilo Moja na mafuta ya maweze Lita Moja na chumvi nikamkabidhi mke wake. Yani walifurai sana, sometimes unajiongeza Ili kujenga URAFIKI,sio unakaa kaa tu kama kama mzoga.Kumbuka wakati naanza safari ya kutoka kule Mpanda nilikuwa nawasiliana na Jamaa yangu Kasukari kwamba atakuja kunipokea na kunisaidia mizigo kushusha kule IGONGE na nilimwambia ningempa chochote na alikubali lakini kitu cha kushangaa nilipofikia nikipiga simu haipatikani hapo imefika sa kumi na moja na nusu, alafu kumbuka kuelekea kule unapita msituni ingawa hakukuwa na wanyama wanaodhuru. Basi nikaona uyu jamaa pengine amekwama kuja hivyo nikapangua zile mizigo miepesi nikafunga na begi langu mgongoni na Toch Kali yenye mwanga safari ikaanza wakati huo Nina redio yangu nikipiga wimbo wa Rose mhando.... Woga ndo umaskini wako mwanangu.. malengo yako utakamilisha vipi we kijana... Kila kitu unasema uwezi uwezi.. kwani wengine waliweza vipi we kijana... Kutwa kucha unashindana na Jua, Jua likisogea na we unasogea.... Kivuri kikisogea na we we unasogea... Umeshindwa kupambanua nyakati we kija... Jifunze Kwa walio fanikiwa kijana Umejiloga mwenyewe ehheeeeeeee... Tantalilaaaaaa.. tintiiiiiiiiiii.... Tantalilaaaaaa.. tintiiiiiiiiiii.
Hatimaye nikafika Kwa ndugu yangu Kasukari, nikakuta amefunga geto naona alikwenda pia shambani, maana alikuwa amelima maharage ya bondeni ambayo wanamwagilia kutumia mifereji kutoka kwenye mto. Basii muda si mrefu akawa amefika na akaanza kuniambia Mwamba!! Yani nilishishindwa kuja nilikuwa napulizia sumu ya wadudu kwenye maharage pole sana Mwamba. Namimj hakuna shida, nikamwambia Jamaa yangu chukua mazaga humo upike kwani maana Mimi nimechoka, ilibidi nimpe dagaa na viungo vyote apike na pia nilimpa dagaa kilo Moja na mafuta yake kama zawadi yake, kumbuka baada ya muda wa wiki kadhaa mbeleni niliamia kambini kwangu na niliondoka na mizigo yangu na zile dagaa nilizo mpa ilikuwa ni mboga yake baada ya kuondoka pale, hivyo nilimwambia hizo dagaa zake atunze tu maana yake ni kwamba tungekula dagaa zangu Hadi naondoka pale kwake nilikuwa na dagaa wengi sana.
Tulimaliza kula na kujiegesha , maana yake Ile sio kulala Yani unaamka asubui mbavu zinauma kinoma, kumbuka kitanda Cha miti ya mianzi juu godoro la nyasi Yani mwanaume unatakiwa ujikubali popote pale.
Kukapambazuka salama lakini kumbuka Kuna mizigo zangu zilibaki kule kijijini, hivyo Kuna wajukuu wa yule Mzee Yani ni watoto wa vijana wa yule Mzee, kwaiyo niliongea na baba yayo nikachukuwa vijana wawili tukapandadisha kijijini. Nikisema kupandisha acha kushangaa[emoji3064][emoji3064] ndio lugha inatumika kule mashambani, utaskikia oya Mwanangu unapandisha kijijini? Na Mimi ndio ngoja nikuagize chumvi na kiberiti Kwa GAMA. Uyu Gama ni jamaa Mangi mmoja maarufu sana pale kjjijini Yani uwezi kwenda kwenye Duka lake ukakoswa kitu Yani hata pilipili utaipata anauza na Huduma zote za miamala ya kifedha Kijiji kizima Hadi vijiji vya jirani wote ni Pale. Anauza Jumla na reja reja, Yani anapiga pesa ni balaaa.
Basi ikabidi niwape pesa wale madogo tukapandisha kijijini, tulifika nikawapeleka kwanza mgahawani kunywa chai Yani madogo walivyo rudi walikwenda kusimulia makwao, maana chai ni kitu hadimu kule mashambani. Baada ya kumaliza kupata chai tulienda kuchukua mizigo na safari ya kurudi ikaanza, kabla ya hapo tulipotoka kupata chai tulikwenda Kwa uyo Mangi mwenye duka Ili kwamba niweze kuweke Salio la kutosha kwenye simu yangu ime vyepesi kuwa nanunua muda wa maongezi juu Kwa juu maana kule hakuna vocha na pia niliweka Salio la M PESA Kwa kunilaisishia kuwa nalipia mtambo wangu wangu Solar kutoka kampuni x maana niliununu Kwa mkopo unalilipia kidogo kidogo. Niliuchukua Kwa ajiri ya Matumizi ya kambini kwangu, kuchaji simu na kupata mwanga. Kumbuka kule hakuna umeme.Safari ya kurudi shambani iliwadia na wale madogo Kila mtu amebeba Mzigo wake na tukafika salama Kwa jamaa yangu Kasukari.

13.KAZI YA KUANZA KUJENGA CAMP KULE SHAMBANI KWANGU.
Wadau baada ya kuwa tumefika na mizigo yetu na wale madogo, ilikuwa ni siku ya Mimi kuandaa vitu flani ambavyo nilipewa na mtaalamu wangu na sikutaka jamaa yangu ajue chochote kuhusu ilo ila niliambiwa Hadi nifanye ilo jambo kule shambani ndio nianze kazi Yani Kwa ufupi nisifanye chochote kule shambani hadi niakikishe SHAMBA limekuwa na walinzi wa Babu, nikisema ivyo wakubwa mnaelewa na kazi iyo ilitakiwa nifanye majira ya alfajiri sana Yani kabla ya watu kuamka napia utakiwi kuongea na mtu hata kama umekutana nae Kwa bahati mbaya.
Nashukuru zoezi nilimaliza na kazi ya ujenzi wa kambi ukaanza.
Siku iliyo fuata baada ya kumaliza lile zoezi nilienda SHAMBA nikiwa na panga, jembe na vifaa vingine kwaajiri ya kwenda kuchora ramani ni wapi nitaiweka kambi yangu na pia kuanza kukata miti na kuchimba mashimo na kusimika miti ya nguzo. Swala la miti haikuwa tatizo maana humo humo kwenye SHAMBA la Mzee kulikuwa na miti kwenye Yale mashamba ambayo hayajalimwa kwaiyo unajikatia tu. Hivyo baada ya kuchora ramani ya kambi yangu ni wapi itakaa nilianza survey ya kuzungukia miti mizuri ambayo ingefaa kama nguzo nilifanikiwa kupata miti mizuri na imara kwaiyo nilikata na kukusanya pamoja na kuanza kusomba kusogeza pale site ambapo nitajenga camp yangu.
Kwa siku iyo nilikamilisha kazi iyo ya kukata miti, maana haikuwa ni miti mingi ilikuwa kama ishirini hivi kwani ukubwa wa kambi yangu ilikuwa ni chumba na sebule lakini vidogo tu sio vikubwa sana, Pia nilimpatia kazi jamaa mmoja Mfipa wa sumbawanga kazi ya kunikatia MIANZI ambayo ningetumia kuzungushia pembeni na kupiga juu Kwa kutumia misumari.Mlio Kaa shambani mtaelewa miti ya mianzi. Kumbuka sikutumia kamba maana nilikuwa nime nunua misumari kilo mbili mchanganyiko kulingana na Kila kazi. Nilimaliza kukata miti na kusogeza na nikarudi magetoni kwenda kurekebisha msosi Ili kwamba saa tisa nirudi kuendelea na kazi ya kuchimba mashimo na kusimika nguzo.
Around saa tisa nilirudi shambani Ili kunza kuchimba mashimo na kuweka nguzo wakati huo yule Mfipa wa sumbawanga anakata mianzi na watoto wake wanasogeza pale site. Uyo jamaa nilimkubali na nilikuwa nampa kazi zangu nyingi maana alikuwa na familia kubwa ya watoto kwaiyo ukimpa kazi muda mchache anakukabidhi,yani alikuwa ni mtu poa sana maana na yeye ndo alikuwa ameamia pale akitokea sumbawanga. Hivyo hakuwa na sehemu ya kupata pesa na pia alikuwa Hana,maana yake ndio wakati alikuwa amefika na alikuwa ajalima mazao kwaiyo alikuwa akitegemea apate kazi ndio apate maitaji ya kuhudumia familia yake.Alipambana jioni iyo lakini akumaliza idadi ya mianzi niliyo itaka ilikuwa ni mingi sana Kwa sababu ingefanya kazi ya kuzungushia uzio kwenye kambi yangu. Sikutaka camp yangu ikae vibaya Yani nilitaka niwe ndani ya usalama ukizingatia kule ni maporini.
Siku iyo nilifunga kazi na kurudi nyumbani kwani Jua lilizama na Kazi ikaishia pale.

Asubui nitaendelea wadau ......Ngoja nilale.
 
Back
Top Bottom