Red black
JF-Expert Member
- Nov 29, 2019
- 5,962
- 17,648
Million'sSijaelewa yani ulipata 800 milliliters
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Million'sSijaelewa yani ulipata 800 milliliters
Mkuu hongera sana,nimekufuatilia mguu Kwa mguu.Naomba kuuliza maswali mawili.Wakuu habari natumaini mu wazima wa afya njema na muendelezo wa sikuu hizi.
Nimelejea baada ya siku mbili tatu hizi kuwa kmy kulingana na harakati za hapa na pale.
Tunaendelea wakuu............
Maisha ndani ya shamba yakaendelea nukapuliza dawa ya magugu iyo ni palizi ya pili sasa,piga dawa ya viutalifu na mahindi yakawa yanaendelea vizuri kabisa yani shamba likawa linapendeza hadi wenyeji wakawa wanashangaa uyu jamaa amepanda mbegu gani?
Maisha yakaendelea yani sikutaka kupoteza muda kabisa.
Muda wa mavuno ukawadia,ukweli ni kwamba kwangu mimi nasema nilipata faida maana sikutumia mbolea yoyote,sikutumia gharama ya kulima shamba.Kwaiyo gharama niliyotumia ilukuwa ni kukodi shamba,palizi ya kwanza,madawa ya kuua wadudu na dawa za magugu.
Jumla nikipiga mahesabu laki 8 ilitumika hadi kumaliza kazi kabisa hadi kuvuna maana ndio pesa nilikuwa nimeitenga kwenye account.
Mavuno niliyopata zilikuwa gunia 42,nikatoa gunia tatu za msosi nyumbani nikauza 39,nilipata 2730000/= iyo ndio pesa niliokunja kwa kiwango changu.
Niliuza kwa bei ya70000 kwa gunia,yani sikutaka kutunza maana niliona nitaingia gharama tena za utunzaji na pengine bei ikapolomoka.
KITU MHIMU UNACHOTAKIWA KUELEWA.
Mimi sio mkulima mkubwa,na sukuwa na mataji mkubwa kwaiyo kwanafasi yangu mimi naona nilipata faida kulingana na kile kidogo nilicho wekeza.Ingiwa na jua wengine mtakuja na hesabu zenu hapa lakini ukweli ndo huo.
Nimeamua ku share experience yangu kwa sisi tusio na mitaji mikubwa ya kuanzia,hivyo ukiamua kuanza hata na kidogo kinakutoa.Kikubwa uende ukiwa na nia na kupenda kile unachofanya.
UZURI WA KILIMO NI KWAMBA.....
Vitu ambavyo nimeviona ni kwamba katika kilimo ukiamua kujiweka kutoka kimaisha ni haraka sana maana pesa ya kilimo unaikamata kwa pamoja na unafanya kile ulichokusudia.Sawa msoto unakuwepo lakini ukiipata inafanya lengo lako kwa wakati mmoja.Nina mifano mingi za jamaa zangu tulio anza nao kilimo wakati huo wao walipambana na wako katka viwango vikubwa.
ACHA KUSIKILIZA MANENO YA WATU.
Kijana mwenzangu acha kusikiliza maneno ya watu,kila mtu anashida zake,tambua shida zako na hakuna atakae kusaidia katika kujikomboa kutoka kwenye huu umasikini tulionao.Unapoamua kufanya maamuzi ya utafutaji jiangalie mwenyewe maana leo hao hao watakuponda haaa mara umeona maisha yamemshinda ameamua kwenda kulima,kikubwa angalia je uyu anaekusema anatoa mchango gani katika maisha yako? au akikusema utapungukiwa nini?.Katika kilimo hizi mitaji za milioni moja, mbili,tatu na kuendelea ukiamua kupambana ni msimu mmoja tu unaipata.
Mhimu,kama mtaji wa kianzio ni mdogo kama ulivyokuwa wangu,tafta kuwekeza maeneo ambayo bado mvua ni za kutosha,aridhi ina rutuba na pia mshamba yana bei nafuu.Hii itakusaidia kupunguza gharama kwa sisi tusio na mitaji mikubwa ya kuendesha kilimo.
VIJANA,KUKAA MJINI WAKATI HATUNA KAZI ZA KUELEWEKA NA KUOMBA OMBA NI UJINGA NA UJINGA MKUBWA SANA.
Ndugu yangu ebu tuambizane tu ukweli sio kwamba natukana ndio hali alisi kabisa,hivi unataka kuniambia kwa kufanya kazi kama hizi tutafikia malengo yetu au kutoboa maisha? Siku moja nimefika stand ya mabasi Nyamuhongoro hapa mjini yani hadi unaskitika ingawa na wewe unashida yani ushanga kuona umati wa vijana hadi wazee wakiwa katika foleni ya kudandia abiria apeleke kwenye bus apate chochote yani hadi huruma.Unataka kuniambia hata kama kwa siku utapata 20000,kiuhalisia ni pesa tu itaishia kulipa kodi ya chumba,kula na nauli za dalala.Hata kwenye uwezo wa kununua debe la mahindi ukaweka ndani uwezo huo haupo,zaidi ya kwenda kupima robo kilo au nusu kwa Mangi.
Mjini tutaweza kukaa lakini kwa akili kubwa,msimu unaenda unalima mazao yako,meingine chakula mengine unauza kufanyia maendeleo yako.Kati ya vitu katika familia vinavyochukua bajeti kubwa ni chakula,tukiweza kuthibiti hapa maisha unatoboa.Ebu tujiwekeze mashambani ndugu zangu,kuna wakati hata unatembea mjini unabaki kujiuliza hivi mimi niko kundi gani? au ninasindikiza wengine tu.
Usione watu wanatembelea magari makali,wengi wanamashamba uko vijijini,lakini mimi na wewe kutwa ni kupinga tu ohhh kilimo ni cha masikini ohhh mara kilimo hakina faida.Aya ngoja tuendeele kulaumu serikali kwamba haitoi ajira.
CHANGAMOTO KATIKA KILIMO ZIPO.
Usiende katika kilimo ukiamini kupata tu,tambua kilimo ni kama kazi nyingine au biashara zingine lakini kikubwa ni kutokata tamaa na pia upende kile unachokifanya.
Ukifanya kazi ya kilimo kwa kuipenda unaweza kuchelewa lakini lazma ufanikiwe siku moja.Kila kazi yaitaji uvumilivu.Hata waliofanikiwa katika kilimo walijitoa.
Epuka sana katika kilimo habari ya wewe kukaa uko ukiamini kuna mtu umemuweka anasimamia,hakikisaha umepata mtu sahihi na atakae fanya kazi hile kama yake,lakini eti wewe umekaa mjini ukiamini kazi inaendelea kwa kupiga simu tu.
Kilimo kinaitaji Physical supervision,maana yake ni kwamba muda mwingi unatumia kuzunguka shambani na kukagua namna mazao yanavyo endelea na changamoto zipi zinakabili mazao yako.
KITU NILICHOJIFUNZA NA KUJIONEA.
Katika wilaya Tanganyika Mkoa wa Katavi ni wilaya ambayo bado ina maeneo makubwa sana ya uwekezaji katika kilimo na ufugaji,utake kufuga Nyuki sawa,ufuge nguruwe sawa,mbuzi sawa yani ufugaji wowote unakubalika.Pia kuna mito mikubwa ambayo hata ukiamua kufanya kilimo cha umwagiliaji inawezekana.
Ninataka sasa kurudisha majeshi kijijini maana haiwezekani kukaa mjini wakati maisha yanaendelea kunichapa.Yani nataka nikawekeze maisha yangu huko,siku nikirudi mjini lazima niwe na kitu cha kuonekana kwamba nimefanya nini.
Ndugu zangu niwatakie maandalizi mema ya sikukuu ya Mwaka mpya,lakini pia tukikumbuka je mwaka unaonza una tumejipanga vipi kuhakikisha tunafikia malengo yetu.Tusikalili tu maisha ya sehemu moja,ukiona sehemu uliopo mambo hayaendi badili upepo nenda mahali pengine pambana.
Kama una swali lolote karibu uniulize nitakujibu bila hiyana yoyote.
Mafundi mitambo wa Jamiiforums mnisaidie kupanga huu uzi kwa mtiririko.
Asante sana, Kwa mfano mahindi yanategemea na aina ya mbegu uliyopanda, Kuna mbegu za muda mfupi na muda mrefu. Kwa mkoa wa KATAVI ukipanda mbegu ya muda mfupi inakula kwako maana itaiva wakati wa mvua nyingi hivyo itapelekea mahindi kuoza shambani. Hivyo ni Bora upande mbegu ya muda mrefu. Mbegu ya Seedco chapa tembo 719 ni mbegu inafanya vizuri sana. Kuhusu mazao Mimi niliona Kila zao linakubali ni wewe tu unataka ulime Nini. Asante.Mkuu hongera sana,nimekufuatilia mguu Kwa mguu.Naomba kuuliza maswali mawili.
1.ulitumia muda Gani Hadi kuuza mazao yako.?
2.Ni mazao Gani mengine ya biashara unayoshauri mtu anaweza kulima katavi mbali na mahindi?
Ahsante
Ni kweli mkuu, furusa zipo katika wilaya ya Tanganyika.View attachment 2854052
View attachment 2854053Nilifika mwese mwezi wa tatu mwaka huu, hakika niliona fursa huenda siku moja nikarudi
View attachment 2854054
Ni kweli kabisa [emoji1787] kamanda, kama safari yangu nilianzia hapa Jamiiforums kwanini nisilete mrejesho ndugu zangu?Hii habari nzuri sana inaonesha ujasiri na kuchukua maamuzi na kutafuta ujuzi wa kazi. Kwenda sehemu hata kibanda ujenge mwenyewe. Hii ndio faida ya JF kuwa na watu kama hawa hawana choyo ya kuleta mrejesho.
Mkuu nikienda sasa hivi si mda sahihi pia? Na shamba si nitapata huko tanganyika kwa 50k? Samahani kwa maswali mengi.Inategemeana na Kilimo Gani, Kwa upande wa mahindi sana mvua zinaanza mwezi wa kumi hapo zimewai na kuendelea. Asante sana ndugu yangu.
Nazungumzia kilimo cha mahindi mkuu.Katavi wanalima sana yani
NitarudiHabarini za jioni wanajanvi, ni jioni nyingine tena baada ya shuruba za siku nzima, nimelejea tena tuendelee na mrejesho wangu. Lakini kuna watu humu wenyewe ni watu wa kuongea maneno ya kukatisha tamaa, ohhh mara uyu sio mkulima, mara uyu hakuna kitu.
Ngoja nikwambie ndugu yangu, kama humu tungefahamiana Kwa majina ungecheka sana, maana Kuna watu humu akitoa comment unaweza kudhani maisha ameyapatia kumbe nae bado anajitafuta na pengine bado anazungusha Cv na kulilia ajira, kumbe hajui kazi zipo lakini ajira hakuna.
Tunaendelea....... Nipo mwanza sasa baada ya kumaliza kusafishia SHAMBA na nikaona muda bado mrefu nikaamua kurudi mwanza kwaajiri ya kufanya kufanya manunuzi ya vitendea kazi lakini pia kwenda kumuona mtaalamu furani aweze kurekebisha mambo flani [emoji16],kumbuka unaingia vitani.
Basi tarehe za mwanzo wa mwezi wa tisa safari ikaanza kurudi KATAVI. Hapo mimefanya manunuzi ya Kila kitu kuanzia majembe, panga, solo pamp, madawa ya wadudu, mbegu za mahindi aina ya DK 719 TEMBO BABA LAO,dawa za magugu, maturubai kwaajili ya kambi, vyombo vya kupikia, dawa za aina mbalimbali kama Malaria, tumbo, dawa za vidonda, nyembe, sindano za viatu na nyuzi, sindano ya mkono,kumbuka kule ni shambani hakuna chereani, kwaiyo hata nguo ya kazi ikichanika nashona mwenyewe, au Farm boots imepasuka nashona mwenyewe like that wadau. Ndo maisha ya SHAMBA hayo.
Yani ni kwamba sikutaka kuwa napoteza muda kitu kidogo tu hadi niende MWESE NO4, kumbuka kule ni shambani ukiingia umeingia, maitaji kuyapata Yako mbali, Yani nilifungansha Kila kitu ambacho kingeitajika kwenye kambi yangu, kumbuka hapo nikifika ni kujenga kambi yangu kule shambani yani nikae kule shamba, maana nilifikiria mvua zikianza kunyesha ningesumbuka sana kuwa natoka kule kuja shambani pili kingine kilichonifanya kujenga kambi ni kitendo Cha Jamaa yangu Kasukari ninapotoka SHAMBA unakuta nae amekwenda shambai na tunapisha muda wa kurudi. Lakini kikubwa zaidi ni mtu ambae tulikuwa hatujazoena maana alihisi pengine ni wale vibaka wa Town kumbe Mimi Sina iyo tabia.
11.SAFARI YA KURUDI MPANDA KUTOKEA MWANZA HAWAMU YA PILI.
Basi ndugu zangu zafari ikaanza kutoka mwanza kwenda Mpanda, wakati wa kurudi nilipanda Bus ya Nyehunge Express, majira ya jioni tukaingia Mpanda, sasa nikafikiria nikisema niende Kwa Jamaa yangu yule wa hapo Town nitahangaika na mizigo kwenda kwake,maana kulikuwa ni mbali.Nilimpigia simu tu akaja pale stand tukasalimia nikampa zawadi ya dagaa wa mwanza, Yani jamaa yangu alishukuru sana.
Kumbuka nimefika jioni na magari ya kwenda MWESE NO4 hayakuwepo muda huo maana yake ni kwamba hadi kesho yake asubui, hivyo nilikesha pale stand na ndugu zangu wasukuma, Yani nyomi ya wasukuma wanahama kutoka mikoa mingine kuja Mpanda Yani ni vurugu tu Kila mahari.
Nilikesha hapo, hatimaye kukapambazuka salama. Kwakuwa Kuna vitu baadhi sikununua mwanza niliona tiaenda kununua kule, mfano misumari ya kujengea kambi, nyundo na vitu kama nyanya, vitunguu, mafuta ya maweze nk. Maana kule mafuta ya maweze yanatumika sana ukanda ule na pia yana Bei nafuu.
Basi mnamo majira ya saa3 asubui nikawa nimemaliza manunuzi yangu na nikachukua bajaji ya kwenda hadi kule Stand ya Mizengo pinda kwenye ofisi za Nyehunge Express nilipoacha mizigo yangu. Tulichukua na kuelekea stand kunakopaki magari madogo ya kuelekea vijijini, nilipandisha mizigo yangu na baada ya muda mchache gari ikaanza mwendo.
Labda niseme kwamba Yani nilifanya manunuzi ambayo Kuna vitu baadhi Hadi namaliza kilimo Kuna vitu nilikuwa navyo na niligawaia rafiki zangu kama vile Dotto Msukuma, Mfipa wa sumbawanga, ndugu yangu Kasukari na Mzee mwenye SHAMBA, hao nilio wataja utaona mbeleni ni jinsi gani waligusa maisha yangu njkaamua kuwapa baadhi ya vitu nilivyo bakiza kambini.
12.NIMEFIKA MWESE NO4 HAWAMU YA PILI TENA.
Baada ya kuwa nimefika mwese nilichukua pikipiki tukafunga mizigo kupeleka Kwa yule Jamaa niliefikia mara ya kwanza wakati namsubiri Jamaa yangu Kasukari kuja kunipokea, kama unakumbuka mwanzo siku nafika Mwese mara ya kwanza. Basi tukafika Kwa uyo jamaa nikamkuta, kwakweli pia ni poa sana. Baada ya kufungua mizigo nilitoa mfuko wenye dagaa kilo Moja na mafuta ya maweze Lita Moja na chumvi nikamkabidhi mke wake. Yani walifurai sana, sometimes unajiongeza Ili kujenga urafiki,sio unakaa kaa tu kama kama mzoga.Kumbuka wakati naanza safari ya kutoka kule Mpanda nilikuwa niwasiliana na Jamaa yangu Kasukari kwamba atakuja kunipokea na kunisaidia mizigo kushusha kule IGONGE na nilimwambia ningempa chochote na alikubali lakini kitu cha kushangaa nilipofika nikipiga simu haipatikani hapo imefika sa kumi na moja na nusu, alafu kumbuka kuelekea kule unapita msituni ingawa hakukuwa na wanyama wanaodhuru. Basi nikaona uyu jamaa pengine amekwama kuja hivyo nikapangua zile mizigo miepesi nikafunga na begi langu mgongoni na Toch Kali yenye mwanga safari ikaanza wakati huo Nina redio yangu nikipiga wimbo wa Rose mhando.... Woga ndo umaskini wako mwanangu.. malengo yako utakamilisha vipi we kijana... Kila kitu unasema uwezi uwezi.. kwani wengine waliweza vipi we kijana... Kutwa kucha unashindana na Jua, Jua likisogea na wewe unasogea.... Kivuri kikisogea na we we unasogea... haujui kupambanua nyakati we kija... Jifunze Kwa walio fanikiwa kijana..... Umejiloga mwenyewe ehheeeeeeee... Tantalilaaaaaa.. tintiiiiiiiiiii.... Tantalilaaaaaa.. tintiiiiiiiiiii.
Hatimaye nikafika Kwa ndugu yangu Kasukari, nilikuta amefunga geto naona alikwenda pia shambani, maana alikuwa amelima maharage ya bondeni ambayo wanamwagilia kutumia mifereji kutoka kwenye mto. Basi muda si mrefu akawa amefika na akaanza kuniambia Mwamba!! Yani nilishindwa kuja nilikuwa napulizia sumu ya wadudu kwenye maharage pole sana Mwamba. Namimj hakuna shida, nikamwambia Jamaa yangu chukua mazaga humo upike maana Mimi nimechoka sana.Kumbuka baada ya muda wa wiki kadhaa mbeleni niliamia kambini kwangu na niliondoka na mizigo yangu na zile dagaa nilizo mpa ilikuwa ni mboga yake,hivyo nilimwambia hizo dagaa zake atunze tu maana yake ni kwamba tungekula dagaa zangu Hadi naondoka pale kwake nilikuwa na dagaa wengi sana.
Tulimaliza kula na kujiegesha , maana yake Ile sio kulala yani unaamka asubui mbavu zikiwa zinauma kinoma, kumbuka kitanda Cha miti ya mianzi na juu ni godoro la nyasi yani mwanaume unatakiwa ujikubali popote na kwalolote katika maisha.
Kukapambazuka salama lakini kumbuka Kuna mizigo zangu zilibaki kule kijijini, hivyo Kuna wajukuu wa yule Mzee Yani ni watoto wa vijana wa yule Mzee.Kwaiyo niliongea na baba yao nikachukuwa vijana wawili tukapandadisha kijijini. Nikisema kupandisha acha kushanga[emoji3064][emoji3064] ni msemo ambayo inatumika kule mashambani.Utasikia oya Mwanangu unapandisha kijijini? Na Mimi ndio!! jamaa ngoja nikuagize chumvi na kiberiti Kwa GAMA. Uyu Gama ni Mangi mmoja maarufu sana pale kjjijini Yani uwezi kwenda kwenye Duka lake ukakoswa kitu Yani hata pilipili utaipata inauzwa na Huduma zote za miamala ya kifedha Kijiji kizima hadi vijiji vya jirani wote ni Pale. Anauza Jumla na reja reja, yani anapiga pesa ni balaaa.
Basi ikabidi niwape pesa wale madogo tukapandisha kijijini, tulifika nikawapeleka kwanza mgahawani kunywa chai yani madogo walivyo rudi kwao walikwenda kusimulia makwao, maana chai ni kitu hadimu kule mashambani. Baada ya kumaliza kupata chai tulienda kuchukua mizigo na safari ya kurudi ikaanza, kabla ya hapo tulipotoka kupata chai tulikwenda Kwa uyo Mangi mwenye duka Ili kwamba niweze kuweka Salio la kutosha kwenye simu yangu iwe vyepesi kuwa nanunua muda wa maongezi juu Kwa juu maana kule hakuna vocha na pia niliweka Salio la M PESA Kwa kunilaisishia kuwa nalipia mtambo wangu wangu Solar kutoka kampuni x maana niliununua Kwa mkopo unalilipia kidogo kidogo. Niliuchukua Kwa ajiri ya Matumizi ya kambini kwangu, kuchaji simu na kupata mwanga. Kumbuka kule hakuna umeme.Safari ya kurudi shambani iliwadia na wale madogo Kila mtu akabeba Mzigo wake na tukafika salama Kwa jamaa yangu Kasukari.