Mrejesho: Safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa Katavi - Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4

Mrejesho: Safari yangu ya kwenda kulima mkoa wa Katavi - Wilaya ya Tanganyika, kijiji cha Mwese 4

Wakuu habari natumaini mu wazima wa afya njema na muendelezo wa sikuu hizi.
Nimelejea baada ya siku mbili tatu hizi kuwa kmy kulingana na harakati za hapa na pale.
Tunaendelea wakuu............

Maisha ndani ya shamba yakaendelea nukapuliza dawa ya magugu iyo ni palizi ya pili sasa,piga dawa ya viutalifu na mahindi yakawa yanaendelea vizuri kabisa yani shamba likawa linapendeza hadi wenyeji wakawa wanashangaa uyu jamaa amepanda mbegu gani?
Maisha yakaendelea yani sikutaka kupoteza muda kabisa.

Muda wa mavuno ukawadia,ukweli ni kwamba kwangu mimi nasema nilipata faida maana sikutumia mbolea yoyote,sikutumia gharama ya kulima shamba.Kwaiyo gharama niliyotumia ilukuwa ni kukodi shamba,palizi ya kwanza,madawa ya kuua wadudu na dawa za magugu.
Jumla nikipiga mahesabu laki 8 ilitumika hadi kumaliza kazi kabisa hadi kuvuna maana ndio pesa nilikuwa nimeitenga kwenye account.

Mavuno niliyopata zilikuwa gunia 42,nikatoa gunia tatu za msosi nyumbani nikauza 39,nilipata 2730000/= iyo ndio pesa niliokunja kwa kiwango changu.
Niliuza kwa bei ya70000 kwa gunia,yani sikutaka kutunza maana niliona nitaingia gharama tena za utunzaji na pengine bei ikapolomoka.

KITU MHIMU UNACHOTAKIWA KUELEWA.
Mimi sio mkulima mkubwa,na sukuwa na mataji mkubwa kwaiyo kwanafasi yangu mimi naona nilipata faida kulingana na kile kidogo nilicho wekeza.Ingiwa na jua wengine mtakuja na hesabu zenu hapa lakini ukweli ndo huo.
Nimeamua ku share experience yangu kwa sisi tusio na mitaji mikubwa ya kuanzia,hivyo ukiamua kuanza hata na kidogo kinakutoa.Kikubwa uende ukiwa na nia na kupenda kile unachofanya.

UZURI WA KILIMO NI KWAMBA.....
Vitu ambavyo nimeviona ni kwamba katika kilimo ukiamua kujiweka kutoka kimaisha ni haraka sana maana pesa ya kilimo unaikamata kwa pamoja na unafanya kile ulichokusudia.Sawa msoto unakuwepo lakini ukiipata inafanya lengo lako kwa wakati mmoja.Nina mifano mingi za jamaa zangu tulio anza nao kilimo wakati huo wao walipambana na wako katka viwango vikubwa.

ACHA KUSIKILIZA MANENO YA WATU.
Kijana mwenzangu acha kusikiliza maneno ya watu,kila mtu anashida zake,tambua shida zako na hakuna atakae kusaidia katika kujikomboa kutoka kwenye huu umasikini tulionao.Unapoamua kufanya maamuzi ya utafutaji jiangalie mwenyewe maana leo hao hao watakuponda haaa mara umeona maisha yamemshinda ameamua kwenda kulima,kikubwa angalia je uyu anaekusema anatoa mchango gani katika maisha yako? au akikusema utapungukiwa nini?.Katika kilimo hizi mitaji za milioni moja, mbili,tatu na kuendelea ukiamua kupambana ni msimu mmoja tu unaipata.
Mhimu,kama mtaji wa kianzio ni mdogo kama ulivyokuwa wangu,tafta kuwekeza maeneo ambayo bado mvua ni za kutosha,aridhi ina rutuba na pia mshamba yana bei nafuu.Hii itakusaidia kupunguza gharama kwa sisi tusio na mitaji mikubwa ya kuendesha kilimo.

VIJANA,KUKAA MJINI WAKATI HATUNA KAZI ZA KUELEWEKA NA KUOMBA OMBA NI UJINGA NA UJINGA MKUBWA SANA.
Ndugu yangu ebu tuambizane tu ukweli sio kwamba natukana ndio hali alisi kabisa,hivi unataka kuniambia kwa kufanya kazi kama hizi tutafikia malengo yetu au kutoboa maisha? Siku moja nimefika stand ya mabasi Nyamuhongoro hapa mjini yani hadi unaskitika ingawa na wewe unashida yani ushanga kuona umati wa vijana hadi wazee wakiwa katika foleni ya kudandia abiria apeleke kwenye bus apate chochote yani hadi huruma.Unataka kuniambia hata kama kwa siku utapata 20000,kiuhalisia ni pesa tu itaishia kulipa kodi ya chumba,kula na nauli za dalala.Hata kwenye uwezo wa kununua debe la mahindi ukaweka ndani uwezo huo haupo,zaidi ya kwenda kupima robo kilo au nusu kwa Mangi.
Mjini tutaweza kukaa lakini kwa akili kubwa,msimu unaenda unalima mazao yako,meingine chakula mengine unauza kufanyia maendeleo yako.Kati ya vitu katika familia vinavyochukua bajeti kubwa ni chakula,tukiweza kuthibiti hapa maisha unatoboa.Ebu tujiwekeze mashambani ndugu zangu,kuna wakati hata unatembea mjini unabaki kujiuliza hivi mimi niko kundi gani? au ninasindikiza wengine tu.
Usione watu wanatembelea magari makali,wengi wanamashamba uko vijijini,lakini mimi na wewe kutwa ni kupinga tu ohhh kilimo ni cha masikini ohhh mara kilimo hakina faida.Aya ngoja tuendeele kulaumu serikali kwamba haitoi ajira.
CHANGAMOTO KATIKA KILIMO ZIPO.
Usiende katika kilimo ukiamini kupata tu,tambua kilimo ni kama kazi nyingine au biashara zingine lakini kikubwa ni kutokata tamaa na pia upende kile unachokifanya.
Ukifanya kazi ya kilimo kwa kuipenda unaweza kuchelewa lakini lazma ufanikiwe siku moja.Kila kazi yaitaji uvumilivu.Hata waliofanikiwa katika kilimo walijitoa.
Epuka sana katika kilimo habari ya wewe kukaa uko ukiamini kuna mtu umemuweka anasimamia,hakikisaha umepata mtu sahihi na atakae fanya kazi hile kama yake,lakini eti wewe umekaa mjini ukiamini kazi inaendelea kwa kupiga simu tu.
Kilimo kinaitaji Physical supervision,maana yake ni kwamba muda mwingi unatumia kuzunguka shambani na kukagua namna mazao yanavyo endelea na changamoto zipi zinakabili mazao yako.

KITU NILICHOJIFUNZA NA KUJIONEA.
Katika wilaya Tanganyika Mkoa wa Katavi ni wilaya ambayo bado ina maeneo makubwa sana ya uwekezaji katika kilimo na ufugaji,utake kufuga Nyuki sawa,ufuge nguruwe sawa,mbuzi sawa yani ufugaji wowote unakubalika.Pia kuna mito mikubwa ambayo hata ukiamua kufanya kilimo cha umwagiliaji inawezekana.
Ninataka sasa kurudisha majeshi kijijini maana haiwezekani kukaa mjini wakati maisha yanaendelea kunichapa.Yani nataka nikawekeze maisha yangu huko,siku nikirudi mjini lazima niwe na kitu cha kuonekana kwamba nimefanya nini.

Ndugu zangu niwatakie maandalizi mema ya sikukuu ya Mwaka mpya,lakini pia tukikumbuka je mwaka unaonza una tumejipanga vipi kuhakikisha tunafikia malengo yetu.Tusikalili tu maisha ya sehemu moja,ukiona sehemu uliopo mambo hayaendi badili upepo nenda mahali pengine pambana.
Kama una swali lolote karibu uniulize nitakujibu bila hiyana yoyote.

Mafundi mitambo wa Jamiiforums mnisaidie kupanga huu uzi kwa mtiririko.
Iyo ndio mbegu niliyolima wadau.
Kwakweli ni mbegu inafanya vizuri sana kama utahudumia, yani inabeba mahindi makubwa. View attachment 2854587View attachment 2854585View attachment 2854586
 

Attachments

  • 5-13.jpg
    5-13.jpg
    67.6 KB · Views: 61
Asante sana, Kwa mfano mahindi yanategemea na aina ya mbegu uliyopanda, Kuna mbegu za muda mfupi na muda mrefu. Kwa mkoa wa KATAVI ukipanda mbegu ya muda mfupi inakula kwako maana itaiva wakati wa mvua nyingi hivyo itapelekea mahindi kuoza shambani. Hivyo ni Bora upande mbegu ya muda mrefu. Mbegu ya Seedco chapa tembo 719 ni mbegu inafanya vizuri sana. Kuhusu mazao Mimi niliona Kila zao linakubali ni wewe tu unataka ulime Nini. Asante.
Mkuu vipi mavuno ya dk 9089 yalikuwa mazuri?
 
Mkuu vipi mavuno ya dk 9089 yalikuwa mazuri?
Mkuu Dk 90-89 yenyewe ilibeba vizuri sana tena sana, lakini Changamoto yake ni kwamba Yani inashambuliwa sana na wadudu waalibifu lakini ukithibiti mapema inafanya vizuri, lakini pia haitaki mvua nyingi maana inakomaa haraka sana.
Yenyewe nilichelewa kuipanda Ili iva vizuri.
Lakini ningeipanda pamoja na tembo ingeoza sana maana ingeivia kwenye mvua nyingi.
Kingine Dk punje zake ni ndogo ndogo sana, uwezi linganisha na mnyama Tembo 719 Yani punje zake ni kubwa sana. Pia inavumilia mvua nyingi. View attachment 2854743
IMG_0027-1024x683.jpg
 
Mkuu jifunafu..nikija huko na m6 nje na matumizi..
Nikataka kulima kama ifuatavyo
1.mahindi m3
2.maharage m2
3.karanga au choroko 1m

Naomba unieleweshe mchanganuo wa gharama za matumizi
Pia ikienda poa naeza pata gunia ngapi
Muda wa kukaa huko....soko ninalo ila bei ya kuuza
Je pia lazma niende kwa mtaalam?
Pls....
 
Mkuu jifunafu..nikija huko na m6 nje na matumizi..
Nikataka kulima kama ifuatavyo
1.mahindi m3
2.maharage m2
3.karanga au choroko 1m

Naomba unieleweshe mchanganuo wa gharama za matumizi
Pia ikienda poa naeza pata gunia ngapi
Muda wa kukaa huko....soko ninalo ila bei ya kuuza
Je pia lazma niende kwa mtaalam?
Pls....
Hahahaha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hapo ngoja kwanza nchekeeee, kwamba Kwa mtaalamu.
Lakni ninachojua Kwa hesabu iyo ni kubwa sana Kwa mazingira ya uko najua Itafanya kazi kubwa sana maana ni kwamba gharama za mashamba na uendeshaji Bado upo chini, cost kubwa inakuja kwenye upande wa madawa. Na itapendeza zaidi uwe na vijana wa mkataba maana yake ni kwamba wao watafanya kazi Hadi mavuno.
Upande wa maharage wanaanza kuandaa mashamba mwezi wa pili. Kama Kuna mengine sijakujibu unaweza kuja PM tukaongea zaidi.
 
Back
Top Bottom