MREJESHO: Simuelewi mume wangu

MREJESHO: Simuelewi mume wangu

Poleni na majukumu, wiki kama mbili zimepita nilikuja kuomba ushauri kuwa mme wangu hataki tushiriki tendo la ndoa, nashukuru wote mlionishauri na kunitia moyo. Mungu awabariki sana.

Mrejesho upo hivi; baada ya kukaa naye chini kumuuliza shida ni nini ameishia kunijibu kuwa anatumia eti dozi ya kupunguza mwili akimaliza dozi mambo yatakuwa mazuri kama mwanzo.

Kiukweli bado sijaridhika na hili jibu, naona kama ni usanii vile. Hivi kuna dozi ya kupunguza mwili ambayo mtumiaji anakatazwa kufanya mapenzi na mke wake? Naona tu kama mapicha picha bado yanaendelea.

Naombeni mnisaidie, vipi kutakuwa na ukweli wowote kuhusu haya majibu yake?

Pia soma: USHAURI: Simuelewi mume wangu
Nilishawahi kipindi kimoja kutumia PEP, nikiamua kusafiri kipindi chote hicho 28 days. Shida yangu ilikuwa hivi, itawezekanaje kutumia mpira kwa mrs???? Nitampa sababu ipi??? So nikaona isiwe tabu, nikamuaga naenda safari, kweli nilitoka kanda ya ziwa nikaend Mkulanga, baadae huyo Mpanda..siku zikaisha, nikatiq timu home.

Inawezekana hili pia limemfika mmeo, huwezi jua..
 
Sina harufu Wala tatizo lolote nipo tu vizuri alafu pia hanaga kinyaa maana kipindi tunafanya kuwa alikuwa anapiga deki kila sehemu Mimi kilichobaki sahivi nahisi tu Kuna mtu kamloga maana nishajikatia tamaa
Nimesikitika hapo kumpigisha deki. Umemlisha uchafu mumeo. Achaneni na huo upuuzi.
 
Poleni na majukumu, wiki kama mbili zimepita nilikuja kuomba ushauri kuwa mme wangu hataki tushiriki tendo la ndoa, nashukuru wote mlionishauri na kunitia moyo. Mungu awabariki sana.

Mrejesho upo hivi; baada ya kukaa naye chini kumuuliza shida ni nini ameishia kunijibu kuwa anatumia eti dozi ya kupunguza mwili akimaliza dozi mambo yatakuwa mazuri kama mwanzo.

Kiukweli bado sijaridhika na hili jibu, naona kama ni usanii vile. Hivi kuna dozi ya kupunguza mwili ambayo mtumiaji anakatazwa kufanya mapenzi na mke wake? Naona tu kama mapicha picha bado yanaendelea.

Naombeni mnisaidie, vipi kutakuwa na ukweli wowote kuhusu haya majibu yake?

Pia soma: USHAURI: Simuelewi mume wangu
🤣🤣 yupo kwenye dozi ya perp guadiola ,kitu dengu mzee ,inaonekana aliteleza na wese jingi ila huo utelezi ulikuwa si salama
 
Ngoja arud nimwambie anioneshe maana nimetafuta nyumba nzima sijaona dawa zozote zile nahisi hapa Kuna kausanii kanaendelea

Na ukomae kabisa kuweka wazi kwamba unaipenda ndoa Yako na uko tayari kujitetea Kwa yeye kuweka Bayana shida ni Nini, bila hivyo mwambie unaondoka. Na kurudi itabidi mshirikishe watu wazima.

Hatukatai kuwa na changamoto au tatizo, tunachogomba ni kukaa kimya au kutoa utetezi wa kitoto.

Kwa ilivyoelezwa hapa inaonekana kabisa una Nia ya dhati kunusuru ndoa na unaipenda ndoa Yako, fight for it.
 
Sina harufu Wala tatizo lolote nipo tu vizuri alafu pia hanaga kinyaa maana kipindi tunafanya kuwa alikuwa anapiga deki kila sehemu Mimi kilichobaki sahivi nahisi tu Kuna mtu kamloga maana nishajikatia tamaa

Haijawahi kutokea tafrani inahisisha yeye kutilia shaka unacheouka? Kwa mwanaume anaempenda mtu ikitokea hizo mambo za kutoka na mwingine inavuruga Kila sekta na taasisi zote za mwili.
 
Usiongee tu sababu bado hayajakukuta na wewe ebu jaribu kufikiria kwa makini alafu uvivae viatu vyangu uone Kama vitakutosha ni mume wangu wa ndoa tunalala kitanda kimoja tunakaribia mwaka hataki kufanya mapenzi nimefanya kila njia imeshimdikana alafu juzi baada ya kutaka kuondoka anasingizia yupo kwenye dozi ya kupunguza mwili huo ni uongo viwango vya mwisho kinachoniuma zaidi inawezekana yeye anafanya uko nje akija Hana habari huo ni ubinafsi tena ni zaidi ya ushetani hata Kama anachepuka angenifikiria na mm mke wake yakishakukuta ndoutanielewa ninachomaanisha
Yatanikutaje mimi Mwanaume. Sawa, je umeshawahi ongea na Mshenga wenu, kanisani au kwa ndugu na jamaa wa karibu ili kama kuna tatizo mliweke sawa kuliko kuja huku JF na kushauriwa uchepuke? Nifahamuvyo, mashaka ya ndoa yana utaratibu wa kuya handle. Kwanza ni nyie kwa nyie then kama inashindikana mnataka na kushirikisha wengine kama mshenga,kanisa/msikiti, wazee wenye hekima, rafiki mnaoheshimiana au hata wazazi na sio kukurupuka. Ndoa itakushinda.
 
Nimeshafanya mbinu zote ndugu yangu Ila hamna lolote Kuna wakati nawaza kalogwa bana eh! Nshajikatia tamaa mtu gani huyu Kuna siku niliamka na hasira nikataka kuondoka alichanganyikiwa kiukweli alivyosikia naondoka bahati nzuri Kuna mtu mzima aliingilia kutusuluisha nikamwelezea matatizo yang na mme wangu akiwepo uzuri yule baba ni mtu mzima Kama baba yetu akamwambia mwanangu jitahidi umridhishe mke wako usipofanya hivyo unamtengenezea mazingira ya kuanza kukusaliti alitushauri tu vitu vingi. akanambia mke wangu naomba usiondoke baada ya hapo nikajua hata tutafanya Ila wapi ana kazi tu ya kunipet pet nisiondoke inakera kwakweli Kuna muda kichwa kinajaa mawazo natamani hata nipige ukunga
Una watoto?
 
Ndoa ni tendo la ndoa. Ndio maana watu wanaungana kwaajili ya kufanya hilo tendo na kutengeneza familia.

Ingekuwa ndoa sio tendo ungeona sawa mwenzako akienda kuliwa na mtu mwingine, usingejali kwasababu ndoa sio tendo.

Na kama wewe ni mwanaume rijali na una mke utakubaliana na ukweli kuwa sio rahisi kukaa zaidi ya wiki mbili bila kufanya tendo labda kama una matatizo.

Ndio maana ndoa za kikristu (Catholic), ukioa au ukiolewa na ukakuta mwenzako hana uwezo wa kufanya hilo tendo..ndoa inabatilishwa mara moja bila pingamizi.

Na wenzetu waislam wanaoa mke wa pili kama wa kwanza hawezi kumtimizia ipasavyo.

Hii ndana kuwa ndoa sio tendo la ndoa mnaitoa wapi?
Inaonyesha unapenda minyanduano i
 
Wewe umejuaje kama bibi zetu walivumilia? Walikwambia?

Issue ya mtu kusafiri miaka kumi na kuwepo nae hapo unalala nae na hakugusi ni mambo mawili tofauti.

Kwanini asipewe sababu tatizo ni nini ili dada wa watu ajue anarekebisha vipi?
Kukaa kimya muda wote huo maana yake ni nini?

Ndoa ni tendo mengine mbwembwe tu.

Wewe mkeo akunyime bila sababu ya msingi utamuelewa? Utavumilia?
Au unadhani mwanamke mihemko yake ya mwili inavumilika kirahisi?

Angekuwa ni mwanaume mwenzako analalamika hapa ungeshauri amteme mkewe, au atafute mwingine. Wabinafsi sana nyie watu. Na hamna akili ya kusolve matatizo kwenye ndoa mkitegemea mtavumiliwa.

Zama za kuwavumilia ujinga zilishapita tuambiane ukweli tuache ujinga wa kuharibu ndoa kwa makusudi halafu lawama ashushiwe mke.

Kama husemi tatizo ni nini umekaa tu kimya au unatoa sababu zisizoeleweka acha tu usaidiwe ili utie akili.

Kama haya yanayosemwa na mtoa mada ni kweli naunga mkono hoja atafute wa kumla hamna namna.

Kila tatizo mnasema mwanamke mpumbavu huvunja ndoa yake mwenyewe sasa hapo mpumbavu ni nani kama sio huyo mume.

Mambo yanabadilika, kama mnategemea wanawake wa miaka kumi ijayo wawe sawa na bibi zenu wa miaka 90 iliyopita kaa hapo usubiri mimi nimekaa paleeeee nakunywa 🍺
Ndio wale wale akina Joyce Kiria. Katika vitu ambavyo Mungu alinipa hekima ni kwenye maswala ya ndoa. Nifahamuvyo, issue za kindoa zina channel za kusuruhisha kama kuna tatizo. Kwanza alitakiwa kuongea na mwenza kujua nini tatizo ikishindikana ashirikishwe mshenga au wazee wa karibu wenye hekima au viongozi wa dini au hata wazazi ila sio kukurupuka huku nakushauriwa na Demi achepuke. Akifumaniwa ndio atadharirika zaidi na hakuna mtu atakayemuelewa akisema mme hakumgusa mwaka mzima. Nimekudharau sana leo Dada kwa ushauri wako eti achepuke
 
Sina harufu Wala tatizo lolote nipo tu vizuri alafu pia hanaga kinyaa maana kipindi tunafanya kuwa alikuwa anapiga deki kila sehemu Mimi kilichobaki sahivi nahisi tu Kuna mtu kamloga maana nishajikatia tamaa
Alikua anapiga deki KILA SEHEMU[emoji2960]
 
Ndio wale wale akina Joyce Kiria. Katika vitu ambavyo Mungu alinipa hekima ni kwenye maswala ya ndoa. Nifahamuvyo, issue za kindoa zina channel za kusuruhisha kama kuna tatizo. Kwanza alitakiwa kuongea na mwenza kujua nini tatizo ikishindikana ashirikishwe mshenga au wazee wa karibu wenye hekima au viongozi wa dini au hata wazazi ila sio kukurupuka huku nakushauriwa na Demi achepuke. Akifumaniwa ndio atadharirika zaidi na hakuna mtu atakayemuelewa akisema mme hakumgusa mwaka mzima. Nimekudharau sana leo Dada kwa ushauri wako eti achepuke
Nidharau vyovyote upendavyo.
Lakini ukweli utabaki pale pale usipomtimizia haja zake mkeo tena bila sababu za msingi wahuni watamtenda tena ile kinomanoma.

Hao washenga na viongozi wa dini hawajawahi kuwasaidia watu matatizo yao sana sana wanayazidisha.

Na watatangaza matatizo yako kwa watu wengine. Hawana msaada wowote zaidi ya kukupa vifungu vya maandiko na kukulazimisha uvumilie.

Na wao ndoa zao zipo juu ya mawe kama wengine.
Halafu utawapelekea mangapi? Mwishowe watakupuuza maana matatizo hayaishi yapo kila siku.

Kama nyie wawili mmeshindwa kusolve matatizo yenu kaa ukijua hakuna mwingine anayeweza.

Baki na mawazo yako nibaki na ya kwangu.

Sitakudharau wala kukulazimisha uone nipo sahihi.
 
Back
Top Bottom