Mrejesho: Ufugaji wa nguruwe, kilimo cha matikiti maji na ufugaji ng'ombe wa maziwa

Asante ninazifatilia
 
Asante, chakula changu kikuu nilikuwa nawapa pumba zilichanganywa na mashudu ya alizeti
 
Binafsi nakushauri USIRUDI tena kwenye NGURUWE na TIKITI.

Ni muda wa kukomaa na kukuza kile kinacholeta MWANGA.

Trial and Error is Over. Komaa Na Ng'ombe Wa Maziwa.
Nguruwe hakuwapatia tu, wafugaji nguruwe wengi wanaotegemea pumb hawapati faida lukuki.
Mashudu baba ni balaa zito yani ukiwalisha asubuhi hadi jioni alafu mziki wake utaniambia ndani ya miezi mitano
 
sabuwanka

Mkuu nimependa sana mrejesho wako
Umetoa elimu yenye exprience yan hujaleta bla bla umeenda field umerud na matokeo yote HASI na CHAYA sasa mi nitahitaji unipe mrejesho wa Hao ngombe wa kisasa juu ya ufugaji wake,Bei zao na vitu vingne vinavyohusiana maana next week tu nilitaka nijitupe kwenye nguruwe ila naona Elimu yako imenifumbua sana hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo zuri kwa mazao yasiotunzika hasa matunda inabidi kuwe na uwekezaji mkubwa wa viwanda vya matunda ili vinunue mali ghafi toka kwa wakulima kwa mkataba
 
Kabla ya kufuga unahitaji kupata elimu ya kutosha juu ya ufugaji, chakula +banda+madawa ila sio mengi na ni rahisi Sana! Karibu ni mradi mzuri ukilingana na imani za wengi! Wateja wa maziwa huwezi wamaliza ni wengi kila mahali. Ushauri mkubwa ninaokupa wasiliana na afisa mifugo aliye karibu nawe,
 
Umesema ukweli ijapo juu ya ufugaji wa nguruwe kuna sehemu ulikuwa unakwama

inawezakana ulileta ufugaji wa makaratasi zaidi kumbe makaratasi sio usahihi wa jambo

Ila tunashkuru kwa mrejesho
Alikwama kwenye chakula. Nguruwe huwezi kumlisha pumba tu utegemee atakuwa kwa kiwango kinachotakiwa.

God save us
 
Hahahahahaha mkuu umenivunja mbavu eti "Kulisha nguruwe ni kipawa toka mbinguni" ase umenena Mimi nilianza na 10 wakubwa uwiiii wasikieni tu nguruwe wanakula vibaya mno hahahaha malengo yangu nifikishe 100+ nilinyoosha mikono sijui inakuwaje ukiwa na number kubwa kwenye ulaji niliuza woteee shubamit Ila nasikia kuna hybrid nzur wanakua fasta na hawali sana au ndo janja za wauza piglets
 
Natamani kupata taarifa kwa mfaidika wa wale wadau wa piglets wa humu na insta, maana piglets wao ukiwaona katika post zao na umri unaotajwa kidogo huwa naona kisanga. Na pia bei zao za piglets sio haba zimesimama kwelikweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ulikosea kwenye chakula .ulitakiwa uchanganye pumba,mashudu na siku nyingine unampa majani au mabaki ya mboga mboga.Ratiba na kiasi cha chakula nacho ni kitu muhimu. Nguruwe anaweza kula mara moja kwa siku lakini akashiba na akanenepa.Nguruwe ni kama binadamu hata apataje chakula lakini kama tumbo lake limejaa minyoo unategemea atanenepaje?

Wewe ulikuwa unalisha minyoo na watakuwa walinenepa sana he he! MRADI WA NGURUWE ASIKUDANGANYE MTU UNALIPA SANA na hiyo IMANI potofu kuhusu kula muda wote sio kweli hao ni wanyama tabia zao zinategemea na utakavyowafundisha wewe.

Mimi nafuga nguruwe na huwa tunawalisha mara moja kwa siku saa tano asubuhi kila siku na wakimaliza kula wanalala ni kujamba tu tu kama scania mpaka kesho yake na chakula tunachompa kila nguruwe ni koleo mbili (spade) naona ni kama kilo na nusu na chakula huwa ni mchanganyiko wa pumba na mashudu na siku nyingine tunawapa majani na mabaki ya mboga mboga au maganda ya ndizi.

KWA FAIDA YAKO ULE UCHAFU unaotoka kwenye utumbo mpana wa NG'OMBE (TAULO) ni chakula kizuri sana kwa nguruwe. Nenda bucha kakusanye mara moja moja unawapa watalamba mpaka ukuta siku hiyo he he! TAHADHARI NYINGINE NI MBEGU.CHAGUA MBEGU NZURI NA ANGALIA UNAPOWAPANDISHA WASIWE WANRUDIANA WAO KWA WAO MAANA YAKE BABA KUMPANDA MTOTO AU MAMA AU DADA INACHANGIA PIA KUWA NA NGURUWE WENYE AFYA DHAIFU.TAFUTA DUME LENYE MBEGU NZURI TOKA UPANDE MWINGINE KABISA NA KAZI YAKE IWE NI KUPANDA NA KILA NGURUWE WAKIZAA TENGA WA KUNENEPESHWA KWA NYAMA NA WA KUZAA .
 
Nilichojifunza hapa ni kuwa, hakuna fursa ya kufanikiwa kirahisi rahisi. Pia katikati ya watu wanaosema wamefanikiwa kwenye jambo fulani basi hapo hapo ujue kuna wengi zaidi walioshindwa vibaya sana katika fursa hiyo hiyo.

Kufanikiwa ni suala binafsi na mara nyingi limezungukwa na siri kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…