MC44
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 2,169
- 3,297
Chakula kilo moja kwa siku?Pole sana mkuu,yaliyokukuta kwenye nguruwe
yaliwahi kunikuta.Ila kuna mfugaji ameniambia
kuwa nilikosea,nguruwe mmoja anatakiwa kula kilo moja
ya pumba kwa siku.muda wote uliobakia anatakiwa apewe maji ya kutosha.
Na ikitokea akawa mzembe wa kula,jitahidi uondoe hayo masalia
ili asizoee kula kila wakati.Hayo mabaki kama unafuga bata au kuku wawekee hayo mabaki
na nguruwe mpe maji tu mpaka kesho yake utakapompa haki yaki ya kilo moja ya pumba.
Hii inasaidia kwamba kesho yake ukimuwekea hiyo kilo moja atakula na kumaliza
maana atakuwa na njaa ya jana.
pia epuka mtindo wa kuwawekea nguruwe vitu mbalimbali kama vile mabaki ya vyakula
au makabichi n.k.ukifanya hivyo unamzoesha kula kila mara bila mpangilio
ambao utakughalimu,maana wakihisi njaa watakupigia kelele na kukukosesha amani.
Natarajia kufuga tena kwa kufuata maelekezo hayo,nione kama nitaweza
kupata faida.Hayo maelezo hapo juu nilipewa na mdau anayefuga
ambaye nilimtembelea nikaona mabanda yake ndo akanipa siri hiyo.
Hii umeifanya au umeitoa kwa wale ma spika?