nimefuga kuku,nimefuga nguruwe na sasa nafuga ngombe,dhana kuwa nguruwe anakula sana sio kweli,nguruwe anahitaji si zaidi ya kilo 3 kwa siku,lakini chakula kiwe na virutubisho vyote!kazi nguruwe unahitaji kuwa na mtaji wa chakula hadi watakapoanza kujiendesha wenyewe,ambapo sio chini ya mwaka ukijitahidi na kufuata kanuni na pia wasiwe wengi au wachache sana,msuli uko kwenye kulisha kwani anakutegemea asilimia 100 ili aishi na kukua inavyotakiwa,ni kweli mbegu zipo wanafikisha kilo 100 na zaidi ndani ya.miezi 6,ila ukimzembea ukamlisha pumba tuu hata kilo 40 utaishia kuzipata kwa taabu ndani ya mwaka, nilipata changamoto ya ugonjwa ASF ambao ukiingia shambani unafagia na hauna tiba,ni ugonjwa wa mlipuko ukitokea ni ngumu kiasi kuzuia hasa kama unafugia sehemu zenye muingiliano,uliondoa nguruwe wote na kuniacha na mkopo wa benki mkubwa tuu,ilibaki kidogo niwe chizi,niliuza vingi kulipa deni,nilikuwa na ngombe kipindi hicho ila nilikuwa siwapi attention kivile ila ndio walikuwa wananiwezesha nyumbani kwa kuilisha familia kipinndi hicho cha mpito,niamua kuwapa full attention baada ya hapo,uzuri pia wanahitaji chakula balanced ila ukikosa wanaishi kwa majani tuu tofauti na nguruwe,halafu anakupa hela kila siku kwa miezi 10 ndani ya mwaka japo kidogo kidogo.......