Mrejesho: Ufugaji wa nguruwe, kilimo cha matikiti maji na ufugaji ng'ombe wa maziwa

Hongera boss unataka kusema nguruwe mkubwa anakula 1.5kg serious?
Na kwenye taulo ni kweli hapo hahahhah nyingine kiboko ni utumbo wa samaki kwa wale wa karibu na ziwa/bahari.
Naomba nikuulize hivi kuchemsha chakula mfano maganda kama viazi,utumbo n.k na kuwapa cha baridi mfumo UPI ni sahihi?
 
NINGEKUSHAURI SIKU MOJA MOJA UCHEMSHE NA SIKU NYINGINE UWAPE MAJANI MABICHI.WASIPOPATA VITAMINI ZOTE VIZURI NDIO ILE YA NGURUWE KULA WATOTO ANAPOZAA.UNAWEZA PIA UKAWA NA ODA YA YALE MADAMU YA NG'OMBE KULE MACHINJIONI UKAYACHEMSHA NA UKACHANGANYA NA MBOGA MBOGA AU MAJANI.USIMPE MADAMU AU MASHUDU YA ALIZETI PEKEE YAKE ATANENEPA SANA NA MAFUTA YATAKUWA MENGI KULIKO NYAMA! NGURUWE ANALIPA KIONGOZI!!!!!
 
Shukrani, nimekuelewa, naomba ufafanuzi zaidi juu ya huo uchafu wa utumbo wa ng'ombe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni ukweli mtupu. Niko sehemu nahangaika na moja ya mradi uliosifiwa sana humu JF. Nasubiri nifike mwisho nije na Uzi uliokamillika.

Diana Spencer

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kitu haukuizingatia
Roughages
Concetrates &
Succulents Ratios katika kila meal unazowapa ngurue wako ....niko na elimu ya kilimo na mifugo ...Dairy cattle, pig industry, Beef cattles
poultry farming, bee keeping , crop productions kwa ujumla soon naingia shambani mimi kama mimi, ....nitakuja na mirejesho na updates
 
sabuwanka

ulinunua Ng'ombe wa Maziwa kiasi gani ? walikuwa na ukubwa gani ? ningependa kuanza kufuga Ng'ombe wa Maziwa lakini ningependa kuanza na ndama wa miezi kama 5-6 na niwakuze
 
Ng'ombe wa maziwa sikubishii sema capital yake ndo inatakiwa uwe vizur kwa kias chake, tofaut na nguruwe ambao unaweza anza hta na piglets10 na ukasonga
mtaji ni kiasi gani ? na nikisema nichukue ndama lets say wa miezi 5-6 na nikawakuza, au unadhani ni vizuri nikichukua Ng'ombe wakubwa tayari kwa ajili ya kukamuliwa ?
 
 
mkuu naomba kujua aina ya ujenzi wa banda unaathiri vipi ukuaji wa nguruwe. kwa kirefu kidpgo
 
Kilimo Cha Matikiti, Binafsi nimekifanya na Ni meaka wa tatu saizi tangu niingie rasmi kwenye kilimo kwa ujumla. Changamoto zipo nyingi sana na hasa hasa unapoingia kwa Mara ya kwanza. Nilichojifunza, kwanza, usiwe mwepesi wa kukata tamaa.Pili dhamira, unapoingia kwa Mara ya kwanza, iwe kujifunza zaidi namna ya kuhudumia kwa ufanisi zao husika ili likupe matokeo tarajiwa. Hapa epuka kulima pakubwa, anza na sehemu ndogo, nusu au eka Moja. Tatu, jifunze changamoto za zao husika, si tu kwa kusoma Bali shambani Moja kwa Moja, Nne Lima Hadi mwisho, hapa namaanisha usiishie katikati ya Safari, jitahidi na hakikisha unalima Mara nyingine ili kurekebisha makosa ya Nyuma. Mwisho husisha Mungu wako katika kilimo chako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha wanajamba kama scania...ila kwenye kila kufeli jua kuna factors nyuma yake asante mkuu kwa kuelewesha hili vizuri.
 
Heko kwako mleta mada uzi mzuri na watu wametiririka vyema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…