Mrejesho: Ufugaji wa nguruwe, kilimo cha matikiti maji na ufugaji ng'ombe wa maziwa

Chakula kilo moja kwa siku?
Hii umeifanya au umeitoa kwa wale ma spika?
 
Yaani kwa mwezi nguruwe wanakula laki 3! God forbid!!! Nikagundua nimekuwa mzalishaji mkubwa wa mbolea badala ya nguruwe!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Elimu sahihi na taarifa sahihi , tembelea mabanda ya hao watu, alie post au hao walio like post , ujifunze.. hiyo ni miez minne

huyu ndani yuko mdau anaitwa Malafyale .. ni baba lao kwenye huu ufugaji , miez sita hadi 120 kg anafika , anafugia morogoro hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeyafurahia sana maneno yako yooote hasa ushauri uliompa muanzisha mada na mfano wa baba yako. Bila shaka tunahitaji kautafiti ka vitendo kabla ya kuyaendea yasemwayo. Kwa mfano, kama mdau angepata fursa ya kujitolea wiki mbili tatu kumsaidia kazi baba yako, angeondoka pale na elimu kubwa kuliko maneno ya matapeli.

Sehemu uliyoniacha kidogo ni kuhusu hawa motivational speaker. Kiufupi, hawakupi mwanga bali wanakupa sababu za kujigeuza fursa kwao. Hawana wanachojua zaidi ya maongezi na uongo.

Mtu mwenye kukupa mwanga hasiti kukuonya juu ya changamoto utakazokutana nazo na masuluhisho ya ukweli. Wao watakwambia changamoto zipo lakini watakupa vile vile suluhisho jepeeesi la kimaandishi halafu...kafie mbele, wao washachukua 20,000 yao.
 
Nilikua nafuga nguruwe, nilifikisha hadi nguruwe 58 ila nataka nibadili nianze kufuga ng'ombe wa maziwa, sababu kubwa ni Homa ya nguruwe African swine fever huku kwetu inapukutisha balaa, nimechoka stress

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Plz nisaidie formula ya hiz kitu..unawachanganyia pumba na mashudu alone? Au unachanganya na maji pia?
Mimi si mfugaji nguruwe lakini pumba laini ya mpunga,pumba ya mahindi,mashudu ya alizeti,pig boost ni miongoni mwa viambata kwenye mchanganyiko wa chakula cha nguruwe.
Naamini wajuzi wapo humu watakusaidia mkuu
 
Mimi si mfugaji nguruwe lakini pumba laini ya mpunga,pumba ya mahindi,mashudu ya alizeti,pig boost ni miongoni mwa viambata kwenye mchanganyiko wa chakula cha nguruwe.
Naamini wajuzi wapo humu watakusaidia mkuu
Mkuu hii pig boost ungeielezea kidogo kwa faida ya wengi, ni nini hasa na upatikanaji wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…