Mrejesho: Ufugaji wa nguruwe, kilimo cha matikiti maji na ufugaji ng'ombe wa maziwa

Uko wap mkuu Mimi binafsi nahitaji sana ng'ombe wa maziwa
 
Hongera kwa kufanikiwa kweny ufugaji wa ng'ombe...Kilimo na ufugaji ndivyo ilivyo wewe umepatia ng'ombe..mwingine kapitia tikiti..mwingine kapatia kuku...mwingine kapatia nguruwe...mwingine kapatia nyanya...lakini huwezi kutoa general conclusion kuwa kilimo hiki ni pasua kichwa...
kuna mwingine kakosea ng'ombe pia...tuendelee kupambana
 
Kiufupi Tu kwenye kilimo ni about best luck, unaweza kuoutshine weather problem but you hit market disaster instead
 
"Nakamua siku 300 na kwa kweli ng'ombe wameniweka mjini na ninawaheshimu! Wakianza kukamuliwa ile asubuhi au jioni mlio wa maziwa kwenye ndoo kwangu ni Bora kuliko mlio wa ATM ikiwa inatoa pesa!

Nikiwa maumwa pesa inaingia, nikiwa mzima pesa inaingia. Changamoto kubwa ni ma bwana mifugo, utunzaji wa nyasi na wanahitaji eneo kubwa! Ila nguruwe na matikiti pasua kichwa!"

Uko maeneo gani mkuu!! Umenivutia sana. Kama hutojali tatafute namna ya kuonana.
Ahsante
 
Asante sana!
Ni nguruwe wa umri gani anakula kilo moja tu ya pumba kwa siku? au ni yeyote tu awe mkubwa au mdogo?
Nguruwe haitaji vyakula vingine zaidi ya pumba?

Nitashukuru kama nitapata mwanga kidogo kwenye hili
 
Ni wa umri wowote,unaweza kumpa na vyakula vingine ila cha msingi ni kuzingatia muda wa kula.
ule muda ukishapita hicho chakula kitoe ili kesho yake ukiweka anakifakamia chote muda ule ule na baada ya hapo ni mwendo wa maji
hadi kesho yake.
 
Asante sana Kaka kwa ufafanuzi huu
Hivi huu muda wa kula ni kama nikiamua nampa asubuhi saa moja. Ina maana nitampa tena kesho yake saa moja hiyo hiyo.

Sasa ninatakiwa kutoa mabaki hayo saa ngapi kama hakumaliza?
Naomba mwanga kidogo hapo mkuu. Au ni muda ule wa kula mfano nikiweka saa moja inatakiwa akae nacho kwa saa ngapi ndipo nikitoe kama hajamaliza?
 
Asante sana!
Ni nguruwe wa umri gani anakula kilo moja tu ya pumba kwa siku? au ni yeyote tu awe mkubwa au mdogo?
Nguruwe haitaji vyakula vingine zaidi ya pumba?

Nitashukuru kama nitapata mwanga kidogo kwenye hili
Nguruwe wanahitaji usafi,hivyo kabla ya kuweka chakula unahitaji kusafisha banda maana yake huwezi kuweka chakula kabla ya saa mbili.

Hivyo ukiweka chakula masaa mawili mpaka manne yanamtosha kuwa amekula na kushiba.baada ya hapo toa hayo masalia na hakikisha
maji ya kunywa yapo muda wote.

Naomba nikukumbushe kuwa mimi sijaanza kufuga,ila ujuzi huu nimeupata kwa jamaa yangu ambaye nimemkuta anafuga nguruwe.

Kwa ufanisi,nikawa namshangaa na kumsimulia nilivyopata hasara ndo akanipa abc za kufuga wanyama hawa kwa faida.

Nguruwe wake ni wasafi na wana afya bora. Usafi huo wa kila siku unasaidia kuondoa ile harufu mbaya ya nguruwe unafugia nyumbani na si rahisi wageni kugundua kama una nguruwe kwa sababu ya kuidhibiti harufu kwa njia ya usafi.
 
Ushauri mulua
 
Mie mfugaji wa nguruwe nawapatia mashudu ya mise mara moja tu
Kila mwezi nachoma sindani za vitamin
Kila baada ya miezi miwili nachoma sindano za minyoo
Matokeo
Wanakula chakula kidogo sana
Wanakuwa vuzuri sana picha nitaweka kesho.
Nilivyoona mise...nikakumbuka SIDO kigoma, hongera
 
Nilikua nafuga nguruwe, nilifikisha hadi nguruwe 58 ila nataka nibadili nianze kufuga ng'ombe wa maziwa, sababu kubwa ni Homa ya nguruwe African swine fever huku kwetu inapukutisha balaa, nimechoka stress

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole yaani ATM inayotembea ( nguruwe) inapukutishwa na swine fever, homa imeshindwa kudhibitiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…