Mrejesho: Ufugaji wa nguruwe, kilimo cha matikiti maji na ufugaji ng'ombe wa maziwa

Inategemeana upo mkoa gani! Kwenye lunch ni Kati ya laki 8- milioni moja! Kwa wafugaji bei maelewano
Mkuu mbona mie nimeona mtandaoni bei za ng'ombe wa kisasa ni zaidi ya hizo; ndama na mitamba ni milioni moja na nusu wakati n'gombe mkubwa wa maziwa ni milioni 2.5?
 
Samahani...mbegu ulipata wapi mimi nipi Arusha na nataka kuanza ufugaji
 
samahani...mbegu ulipata wapi mimi nipi Arusha na nataka kuanza ufugaji
Kwa msaada tu, ingia instagram "Malafyale pig farms" wana mbegu nzuri, hawa wako morogoro. Contacts zao zipo huko utazipata.
 
Kwanza hongera kwa kuamua kuwekeza kwenye ufugaji na pole kwa changamoto ulizopitia. Ufugaji wa nguruwe ni rahisi sana na unalipa hivyo haukudanganywa kabisa. Nimeona tatizo kubwa kwako lilikuwa ni lishe ila sijajua pia kama ulikuwa unawapatia vitamini na dawa za minyoo. Nguruwe wanahitaji mlo kamili na si mashudu tu, na mlo wenyewe unaweza kuundaa mwenyewe kwa kutumia vyakula ghafi vinavyotuzunguka na hili litakupunguzia gharama za ulishaji kwa 50% au zaidi. Nitajitahidi kesho nikutumie kitini chenye namna bora ya kuandaa chakula na kwa kutumia malighafi zinazotuzunguka, kinajumuisha pia mali ghafi hizo na utashangaa ilivyo rahisi na yenye tija. Tutashare pia uzoefu zaidi lakini nguruwe ni kuwapa mlo kamili plus maji ya kunywa ya kutosha, wawe na banda bora na safi, wapate dawa & chanjo tu. Miezi sita unawauza vizuri sana. Hongera sana tena na kesho nitajitahidi kushare nawe.
 
Mkuu focal hicho kitini naomba usinisahau, maana na mie nafanya huo ufugaji.
 
Mkuu mbona mie nimeona mtandaoni bei za ng'ombe wa kisasa ni zaidi ya hizo; ndama na mitamba ni milioni moja na nusu wakati n'gombe mkubwa wa maziwa ni milioni 2.5?
Hiyo Bei niliyokupa ni ya vituo vya serikali, binafsi ni ghali hata zaidi ya 2.5
 
Nani pia naomba hicho kitini
 
nimefuga kuku,nimefuga nguruwe na sasa nafuga ngombe,dhana kuwa nguruwe anakula sana sio kweli,nguruwe anahitaji si zaidi ya kilo 3 kwa siku,lakini chakula kiwe na virutubisho vyote!kazi nguruwe unahitaji kuwa na mtaji wa chakula hadi watakapoanza kujiendesha wenyewe,ambapo sio chini ya mwaka ukijitahidi na kufuata kanuni na pia wasiwe wengi au wachache sana,msuli uko kwenye kulisha kwani anakutegemea asilimia 100 ili aishi na kukua inavyotakiwa,ni kweli mbegu zipo wanafikisha kilo 100 na zaidi ndani ya.miezi 6,ila ukimzembea ukamlisha pumba tuu hata kilo 40 utaishia kuzipata kwa taabu ndani ya mwaka, nilipata changamoto ya ugonjwa ASF ambao ukiingia shambani unafagia na hauna tiba,ni ugonjwa wa mlipuko ukitokea ni ngumu kiasi kuzuia hasa kama unafugia sehemu zenye muingiliano,uliondoa nguruwe wote na kuniacha na mkopo wa benki mkubwa tuu,ilibaki kidogo niwe chizi,niliuza vingi kulipa deni,nilikuwa na ngombe kipindi hicho ila nilikuwa siwapi attention kivile ila ndio walikuwa wananiwezesha nyumbani kwa kuilisha familia kipinndi hicho cha mpito,niamua kuwapa full attention baada ya hapo,uzuri pia wanahitaji chakula balanced ila ukikosa wanaishi kwa majani tuu tofauti na nguruwe,halafu anakupa hela kila siku kwa miezi 10 ndani ya mwaka japo kidogo kidogo.......
 
Ng'ombe uko nao wangapi? Walikuwa wakikupa wastani wa lita ngapi kwa mmoja? Makadirio ya lita ngapi kwa ujumla wao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…