Faka25
JF-Expert Member
- Sep 14, 2021
- 1,988
- 1,442
Natumai wote mko salama.
Napenda kushiriki kwa uchungu na tahadhari kuhusu tukio lililonikumba hivi karibuni kupitia jukwaa hili. Niliingia mawasiliano na mmoja wa wanachama humu ambaye aliniahidi kutuma game pamoja na simu Tulizungumza kwa muda, akanivuta kwa uaminifu na hatimaye nikatuma kiasi cha pesa shilingi laki tatu sitini.
Baada ya hapo – mawasiliano yakakatika. Hajawahi kujibu tena, na kila dalili zinaonesha kuwa ilikuwa ni njama ya kitapeli.
Ninachotaka kufikisha hapa ni tahadhari kwa wanajamii wengine:
Nawashukuru kwa kunisoma – na naomba ujumbe huu uwafikie wengi ili wengine wasije wakakumbwa na hali kama yangu.

- Jihadharini kabla ya kutuma fedha kwa mtu yeyote mtandaoni.
- Hakikisheni mna uthibitisho wa kutosha kuhusu mtu, huduma, au bidhaa kabla ya kufanya miamala.
- Kama kuna wasiwasi wowote – ni bora kuuliza kwanza hapa JF au kufanya utafiti wa kina.