MREJESHO: Uzoefu wangu wa kutapeliwa na member, jihadhari!

Attachments

  • C7475524-8D86-4429-B591-A63A981568FB.png
    C7475524-8D86-4429-B591-A63A981568FB.png
    357 KB · Views: 20
Natumai wote mko salama.

Napenda kushiriki kwa uchungu na tahadhari kuhusu tukio lililonikumba hivi karibuni kupitia jukwaa hili. Niliingia mawasiliano na mmoja wa wanachama humu ambaye aliniahidi kutuma game pamoja na simu Tulizungumza kwa muda, akanivuta kwa uaminifu na hatimaye nikatuma kiasi cha pesa shilingi laki tatu sitini.

Baada ya hapo – mawasiliano yakakatika. Hajawahi kujibu tena, na kila dalili zinaonesha kuwa ilikuwa ni njama ya kitapeli.

Ninachotaka kufikisha hapa ni tahadhari kwa wanajamii wengine:
  • Jihadharini kabla ya kutuma fedha kwa mtu yeyote mtandaoni.
  • Hakikisheni mna uthibitisho wa kutosha kuhusu mtu, huduma, au bidhaa kabla ya kufanya miamala.
  • Kama kuna wasiwasi wowote – ni bora kuuliza kwanza hapa JF au kufanya utafiti wa kina.
Nimesikitishwa sana kwa kuwa nilikuwa na imani kuwa JamiiForums ni jukwaa salama kwa mijadala na hata biashara, lakini tukio hili limenifungua macho. Natarajia uongozi wa JF wataendelea kuweka mazingira salama kwa wote.

Nawashukuru kwa kunisoma – na naomba ujumbe huu uwafikie wengi ili wengine wasije wakakumbwa na hali kama yangu.

View attachment 3357376View attachment 3357377
Sa mwamala mbona unasoma 160,000/= badala ya laki tatu na sitini!!?
 
Umetapeliwa kishamba sana !

Ulitakiwa mkubaliane bei, then umuambie aende offc ya kampuni utakayochagua wewe tena uwe na mawasiliano na mtu huyo umtoe hela nzuri, alafu jamaa aende hapo offcn akupigie video call yupo na mtu wa kampuni husika ya mabasi/cargo, alafu mtu wa cargo akishapokea ndo utume hela,,,,, ! Mind you call zote ziwe recorded, pamoja na sms zote tunza na sms za miamala utunze,,,, !!!

Incase lilitokea lotote sasa utadili na kampuni husika !!!!

Pole ngosha, karibu mjini !
 
Natumai wote mko salama.

Napenda kushiriki kwa uchungu na tahadhari kuhusu tukio lililonikumba hivi karibuni kupitia jukwaa hili. Niliingia mawasiliano na mmoja wa wanachama humu ambaye aliniahidi kutuma game pamoja na simu Tulizungumza kwa muda, akanivuta kwa uaminifu na hatimaye nikatuma kiasi cha pesa shilingi laki tatu sitini.

Baada ya hapo – mawasiliano yakakatika. Hajawahi kujibu tena, na kila dalili zinaonesha kuwa ilikuwa ni njama ya kitapeli.

Ninachotaka kufikisha hapa ni tahadhari kwa wanajamii wengine:
  • Jihadharini kabla ya kutuma fedha kwa mtu yeyote mtandaoni.
  • Hakikisheni mna uthibitisho wa kutosha kuhusu mtu, huduma, au bidhaa kabla ya kufanya miamala.
  • Kama kuna wasiwasi wowote – ni bora kuuliza kwanza hapa JF au kufanya utafiti wa kina.
Nimesikitishwa sana kwa kuwa nilikuwa na imani kuwa JamiiForums ni jukwaa salama kwa mijadala na hata biashara, lakini tukio hili limenifungua macho. Natarajia uongozi wa JF wataendelea kuweka mazingira salama kwa wote.

Nawashukuru kwa kunisoma – na naomba ujumbe huu uwafikie wengi ili wengine wasije wakakumbwa na hali kama yangu.

View attachment 3357376View attachment 3357377
Sa mwamala mbona unasoma 160,000/= badala ya laki tatu na sitini!!?
 
😹😹😹😹😹😹
Yani kitendo cha mtu kuingia humu tayari inatakiwa uwe makini…!!
Sehemu ambayo watu wanatumia fake Id wewe unataka kujifanya kumjua zaidi…!! 🤣

Weka id yake hapa tumsute, ila maboya hamji kuisha…!! 😹
 
Ila watu mnajiweza aisee unatuma kabisa pesa kwa mtu humjui, mimi hata buku situmiiii yaani kweli kila mtu yupo tofauti
Sasa utakuaje mfanya biashara bila kutuma pesa kwa watu, biashara ina mambo.
 
Back
Top Bottom