Poker
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 5,445
- 14,828
Habari za wanga! Muda ni 1:00 usiku wa manane, mbalamwezi na nyota zinaonekana vizuri kabisa. Nimeamua kuzima kabisa main switch, ili kuwe na giza totoro.
Nimechukua mahitaji yangu ambayo niliambiwa lazima uwe nayo, yaani kichana, tufani na kioo. Mimi nikaongeza mishumaa, uwaridi nyekundu na kaniki nyekundu.
Hivyo niliwasha mishumaa kuzunguka kioo nikapanga uwaridi na kujifunga kaniki nyekundu. Kisha nikachukua tufani jekundu na kuanza kula huku nikitizama kioo na kuchana nywele zangu, ilinichukua kama dakika 2 hivi nikaona mwanamke amesimama mbele yangu, yaani tunatizamana nilipo jaribu kuhamaki na kupepesa macho sikumuona tena.
Nikarudia mara pili, sa hii nikaamua kuongeza na uturi na habbat soda ili nione tamati yake. Lakini cha miujiza nilipoanza kutizama tena kioo kilitingishika na kupasuka na ile mishumaa ikazima ghafla. Imenibidi nikimbilie main switch tena niwashe maana naona mauza uza tu.
NB: Niliingia saiti ili nijionee kama tomaso na nimeleta feedback, feel free na wewe kujaribu it's fun 😊 though!
MY TAKE: Mi binafsi nahisi ni hallucinations na wala hamna ukweli wowote ila kioo kupasuka na mishumaa kuzima nimehisi labda ni upepo ambao ulipiga ghafla.
Ila ni hallucinations, kwasababu baada ya kuwasha taa nimejaribu tena hilo zoezi kwenye kioo cha bafuni nikajiangalia bila kupepesa kope, kiufupi sura iliotokea siitambui ila sio mimi! Kwahyo ni hallucinations zinazobadili imaginations kwenye kichwa.
UZI WA Rakims huu hapa chini.
Thread 'Jinsi ya kumuona utakayemuoa au utakayeolewa naye' Jinsi ya kumuona utakayemuoa au utakayeolewa naye