Mimi nilikosa uaridi nikaamua nitumie maua ya alizeti na tufani pia kwakua sijui ni tunda gani nikaamua nitumie mapera, ghetto huwa sina kioo natumiaga kioo cha dirisha ila hadi nitoke kwa nje ndo najiona kwa ndani huwa sijioni usiku nikaamua kwenda kufanya hilo zoezi kwa nje alafu ni nyumba ya wapangaji, baada ya kuwasha mishumaa na kuvaa kaniki huku natafuna pera ilikua ni kwenye dirisha la jirani nilichoona ni dirisha linafunguliwa na kuskia sauti ya mwanamke anapiga kelele
Ghafla watu wakanizunguka walikua ni watu kama watano wawili wameshika rungu mmoja kashika tochi alafu wanaulizana kwa kusema huyu si ni lucha? Kabla sijajibu nilihisi Kuna kitu kizito kimetua kichwani nikaona giza sikuskia sauti ya watu tena nikaja kushtuka ndugu zangu wamenizunguka nipo hospital na kwenye ile nyumba walihamisha vyombo vyangu vyote kabla sijashtuka wakavirudisha nyumbani.
Sasa sijui nilipigana na mashemeji kabla sijamuona mchumba au kilitokea nini