Mrejesho wa kutafuta kazi

Sawa. Kesho ni Jumapili, sidhani kama utaukuta utawala. Ila kazi huwa zinaendelea. Ni Kampuni, ila sijui taratibu za malipo. Kufika kwa miguu, yawezekana. Tatizo sina uwezo wa kukuelekeza kwa njia ili ufike. Pia Niko na namba za mmoja wa watumishi pale. Ila sina ridhaa ya kukupa mpaka nimjulishe mwenyewe. Ushauri wangu, fika kwenye hicho kituo, waulize haohao madereva bodaboda, wakuelekeze. Mimi si mwenyeji mzuri kule.
 
Hiyo ni kampuni kaka inaitwa Chanika Poultry farm ltd.
WaAlishaji wa kuku wa nyama na mayai. Ni kweli huwa wanatoa ajira Kwa vijana wengi tu na vigezo ni kwamba uwe na TIN number, kitambulisho Cha taifa au namba, cheti at least Cha form 4 au hata kama huna maana Kuna kazi za nguvu tu.
Changamoto itakayompata ndugu yetu ni kwamba pale wanalipa Kwa mwezi, Yani Kila tarehe 30 hata ukianza kazi Leo ikifika tarehe 30 mnalipwa wote.
 
Sawa Sawa mkuu. Asante kwa kuongeza nyama. Nadhani ni vyema akasogea pale na kupata taarifa zaidi, na akafanya maamuzi.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu. Uwezo wa kufanya hiyo kazi ninao ila changamoto ni hapo kwenye malipo kidogo itakuwa ngumu kwangu
 
All the best mwamba,binadamu tunapitia changamoto tofauti tofauti,muhimu kila hatua dua isikosekane! Mimi ni mdau wa ujenzi....naweza kuku accomodate kwa ujira wa 15000 kwa siku kwa msaidizi wa fundi tatizo ushasema una hitilafu ya kiafya!
 

Pole sana kwa Changamoto haya yote ni mapito yataka sawa.

Maisha bora yanapatikana vijijini, kama unaona mjini hakuna dalili yoyote ya kutoboa maisha rudi kijijini ukalime, saizi ni msimu wa kuandaa mashamba.

Una nusu heka hiyo inatosha kuanzia, kipindi cha masika vijijini kuna kazi nyingi tu za vibarua.

Asilimia kubwa watu wa DSM kazi za ovyo wanazidharau, usiogope kudharauliwa, uoga wako do umasikini wako, amuka ukapambane.


Hatima ya maisha yako bora iko mikononi mwako, na hatima ya maisha mambaya iko kichwani kwako (either kichwa cha Juu au Kichwa cha Chini).

Mwanaume usiogope kazi, pambana, hakuna mtu atakuja kukusaidia bila kujipambania, hapa utatiwa moyo tu ila hakuna atakayekusaidia.

Cha mwisho, umefanya kosa kubwa sana kumfanya mkeo awe kama baba wa Familia, yaani wewe unagubali Familia yako ilishwe na mkeo tena kazi ya mgahawani ????

Tunajua fika kazi ya mgahawani ni moja ya kazi ya kuzalilishwa sana, kila aina ya mwanaume atakuwa anamshika shika mke wako.

Umenishangaza sana yaani wewe unalea watoto nyumbani na mkeo anaenda mzigoni kusaka maisha.

Embu wanaume tupambaneni Jamani, hii ni aibu sana kwa upande wako, mkeo atafikia hatua akuchoke na atakudharau.

Mungu akusaidie na afungue riziki katika maisha yakoo, Jmosi njema.
 

Umekosa mtaji ?? Unasema huna mtaji wakati una smart phone ambayo inakupa access ya Kuingia JAMII FORUM.

uza hiyo smart phone upate mtaji wa kuanzia. Bora hapo akili ni dogo tu bwana boshe.
 
All the best mwamba,binadamu tunapitia changamoto tofauti tofauti,muhimu kila hatua dua isikosekane! Mimi ni mdau wa ujenzi....naweza kuku accomodate kwa ujira wa 15000 kwa siku kwa msaidizi wa fundi tatizo ushasema una hitilafu ya kiafya!
Ndugu kama kuna uwezekano naomba msaada wa saidia fundi mawasiliano yng ni 0766889930
 
Umekosa mtaji ?? Unasema huna mtaji wakati una smart phone ambayo inakupa access ya Kuingia JAMII FORUM.

uza hiyo smart phone uoate mtaji wa kuanzia. Bora hapo akili ni dogo tu bwana boshe.
Aisee!? Sio wazo baya lakini kumbuka hii ndio inanisaidia kupata connection mbali mbali mkuu, hata kazi ya mwanzo nisingepata bila hii maana ndio natumia kutafutia ajira mbali mbali zinazotangazwa sasa nikiuza mkuu itakuwaje? Je umejaribu kuwaza na hilo?
 

Nunua simu dogo ya 25,000
 
Nimepokea ushauri wako mkuu. Lakini eneo niliponunua ni barabarani kabisa (town) ni ngumu kusema utafanya kilimo, lakini pia hata lingekuwa kijijini nisingewaza kwasasa sababu kilimo kinataka ujipange uwe na nyenzo zote, hizo napata wapi kwa sasa sina?

Na kuhusu wife kupush mazingira hapa home jaribu kupitia tena post yangu then utaelewa vizuri kwanini nimerudi tena hapa jukwaani ni kwa sababu hiyo ya dharau anayoipata wife huko sipendi kuona ikiendelea ndo maana nataka abaki home nirudi mtaani mwenyewe. Naimani hapo utakuwa umenielewa mkuu
 
Una una uchungu na jamaa safi nimependa lakini ushauri wako umekaa kitapeli sana
 
Ila kuacha kazi kwa sababu wanalipa katikati na mwezi wa mwezi haijakaa poa. Labda ungesema mshahara ni mdogo au mazingira ya kazi ni magumu, tungeweza kuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…