Habari za siku kadhaa ndugu zangu.
Narudi tena kwenu wakuu. Week kadhaa zilizopita nilileta bandiko la kutafuta kazi hapa, sipendi nieleze tena mapito yangu ila nataka kusema tu bado kwa upande wangu giza ni kubwa sioni mwangaza
Nimejaribu haya kwa upande wangu
1. Nimejaribu viwandani, nilienda kiwanda cha rasta pale mbagala lakini nilishindwa sababu ya kwamba hawalipi kwa siku wao wanalipa katikati ya mwezi na mwisho wa mwezi, ambapo kwa upande wangu ni vigumu sababu mimi nahitaji hela ya mlo wa siku na familia. Sikuweza kwenda viwanda vya kubeba vitu vizito sababu nina shida ya mbavu
2. Nimejaribu kusema na ndugu zangu wa karibu japo wanikopeshe mtaji nifanye business, niliwaza kufanya biashara ya kuku wa kuchoma, phone accessories, vile visendo vya kina dada au nyingine yoyote mradi kipatikane kipato kwa siku lakini bahati mbaya ndugu nao wanasema hawana kitu
3. Nimejaribu kutafuta mteja ili niuze eneo langu lipo huko mkoa wa kusini nusu eka, nililinunua nilipokuwa huko maana nilipata kazi ya kusimamia mradi wa mtu kwa muda. Lengo ilikuwa niuze nipate mtaji maana sina jinsi, lakini nalo kwa bahati mbaya sijapata mteja mpaka sasa
4. Nimejaribu kadili ya uwezo wangu kutafuta channels sehemu tofauti tofauti lakini wapi! Bado naona giza
Naishi vipi sasahivi?
Kiukweli kwasasa wife ndio anapush jahazi hivyo hivyo mdogo mdogo. Ipo hivi, baada ya upande wangu kuona mambo magumu ikabidi nimwambie yeye ajaribu kutafuta hata hizi za mama lishe za 3000 kwa siku, Mungu ni mwema kweli kuna sehemu amepata ndio hapo anajishikiza, akipata hiyo 3k akitoa nauli 1000 inabaki 2000 ndo anarudi na chochote cha kula siku hiyo.
Kwanini nimerudi tena? Nataka nini?
Kiukweli ndugu zangu hii ishu anayofanya wife mpaka mwenyewe namuonea huruma, huwa ananieleza changamoto anazokutana nazo nadhani wenyewe mnajua wanayopitia mama lishe, mbali ya hizo changamoto ni kwamba ikitokea siku biashara imeenda vibaya basi ndo harudi na chochote. Kwa upande wangu nashindwa tena kutoka kuangaika sababu yeye akitoka asubuhi mimi nabaki na watoto kuwazingatia mpaka usiku anaporudi kwahiyo siku inaisha hivyo.
Sasa nimerudi tena kuwaomba ndugu zangu, sihitaji msaada wa pesa hapana ila nipe tu kazi kama unayo ambayo naweza kupata kuanzia 5000 kwa siku utakuwa umenisaidia sana ili tu huyu mama nimpumzishe nyumbani awalee watoto wake vizuri. Hiko ndicho ninachohitaji ndugu zangu hata kama kazi yako inatoa ujira kwa mwezi, me nilipe tu kwa siku ili family ipate kula basi! Vinginevyo naona kabisa mzigo unanielemea halafu wa kunitetea sina
Kuna muda napata mawazo mabaya ya kumkosea Mungu lakini kila nikifikiria naona hata! Huu mzigo ni wangu sina wa kumuachia! Labda ningekuwa mwenyewe pengine ningesema nikajaribu maisha nchi za watu hapa bongo pamenikataa.
Naomba mnishike mkono ndugu zangu. Asanteni, usiku mwema
Pole sana kwa Changamoto haya yote ni mapito yataka sawa.
Maisha bora yanapatikana vijijini, kama unaona mjini hakuna dalili yoyote ya kutoboa maisha rudi kijijini ukalime, saizi ni msimu wa kuandaa mashamba.
Una nusu heka hiyo inatosha kuanzia, kipindi cha masika vijijini kuna kazi nyingi tu za vibarua.
Asilimia kubwa watu wa DSM kazi za ovyo wanazidharau, usiogope kudharauliwa, uoga wako do umasikini wako, amuka ukapambane.
Hatima ya maisha yako bora iko mikononi mwako, na hatima ya maisha mambaya iko kichwani kwako (either kichwa cha Juu au Kichwa cha Chini).
Mwanaume usiogope kazi, pambana, hakuna mtu atakuja kukusaidia bila kujipambania, hapa utatiwa moyo tu ila hakuna atakayekusaidia.
Cha mwisho, umefanya kosa kubwa sana kumfanya mkeo awe kama baba wa Familia, yaani wewe unagubali Familia yako ilishwe na mkeo tena kazi ya mgahawani ????
Tunajua fika kazi ya mgahawani ni moja ya kazi ya kuzalilishwa sana, kila aina ya mwanaume atakuwa anamshika shika mke wako.
Umenishangaza sana yaani wewe unalea watoto nyumbani na mkeo anaenda mzigoni kusaka maisha.
Embu wanaume tupambaneni Jamani, hii ni aibu sana kwa upande wako, mkeo atafikia hatua akuchoke na atakudharau.
Mungu akusaidie na afungue riziki katika maisha yakoo, Jmosi njema.