Mrejesho: Yeyote anayemjua mtaalam anayeweza kumrejesha ndugu yetu aliyefariki kifo cha kutatanisha

Mrejesho: Yeyote anayemjua mtaalam anayeweza kumrejesha ndugu yetu aliyefariki kifo cha kutatanisha

Nachojua mzazi ni Mungu wa 2 duniani mzazi akisikitika tu mambo yako hayataenda muombeni msamaha aise kabla hajaondoka duniani huyo mzee..anywys poleni...lakini kwanini msiache lipite mmkabidhi Mungu jambo hili?

Koo zinazoamini haya mambo mie naogopa hata ujirani nao aise🙌
 
Ndugu, hao Wataalam watawaletea Mtafaruku mkubwa zaidi kwa ninyi mliobaki. Ndugu yenu ameshafariki, jengeni amani baina yenu ninyi mliobaki.

Ukweli ni kuwa kamwe hatorudi. Ameshalala. Na nadhani, mwenye maumivu zaidi ni baba mzazi kuliko ninyi ndugu. Msiendelee kumuumiza.

Kama kakataa achaneni naye. Badala yake ninyi mkae kwa tahadhari.

Mengine yote hayana msingi kwa sasa.
 
Hapo mmekwama kwani hitajilenu Ni lipi?
1. Kumrejesha mpendwa wenu au
2. Kumtafuta aliye muua

Kama hitajilenu ni kumrejesha mpendwa wenu mbona mnatakakumhukumu mpendwa wenu mwingine (baba)

Kama ni kumtafuta aliye muua uzi usomeke hivi "tunataka kuua alie muua mpendwa wetu"

Nb: hata aliye muua mpendwa wenu hawezi kumrejesha.
 
Habari wakuu!

Heshima kwenu wana jukwaa mliojaa maarifa na utambuzi wa mambo.

Naomba niende moja kwa moja kwenye maada;

Nilileta maada tajwa hapo juu....kiufupi sisi ni watu tunaotokea mkoa wa morogoro lakini nadhani background yetu haiwezi kuwa na umuhimu katika hili.

Nimekuja tena ndugu yenu kuwapa mrejesho wa hili jambo na baada ya kumaliza nitaomba ushauri kutoka kwenu wakuu.

Kiukweli tunasikitika kwamba baada ya kutafuta suluhisho la tatizo kwa wataalamu mbali mbali tumekuja kujua ya kwamba baba mzazi wa marehem ndiyo muhusika mkuu wa kifo cha mtoto japo yeye amekana kabisa lakini wataalamu wote ambao tumeenda ndiyo wamesema kwa baba ni muhusika mkuu, najua hii kauli italeta mjadala lakini naomba nisinukuliwe vibaya...kuna watu hawaaamini katika ushirikina lakini naomba muwe wavumilivu katika hili.

Nisiandike sana wakuu maana nina mengi ya kusema lakini cha muhimu naomba kupata ushauri kutoka kwenu, ni hatua gani tunapaswa kufanya ili kulitatua hili tatizo kwa namna yoyote ile.

Pia Kama kuna mtaalam anayeweza kutusaidia kushughulikia hili jambo atusaidie

Angalizo: Mnaotukana na kujibu vibaya mbarikiwe sana kwasababu hakuna aliyeomba kuzaliwa katika familia yenye matatizo.

Karibuni.

Ufu 14:13 SUV​

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
 
Wewe unasema wataalamu wamemtaja Baba Mzazi. Halafu tena unakuja kwetu kukusaidie kupata wataalamu wengine!Mkuu unazingua. Na mimi nikisem ni mtaalamu na nimegundua muuaji ni wewe ntakuwa nasema urongo?
 
Back
Top Bottom