Mrejesho: Yeyote anayemjua mtaalam anayeweza kumrejesha ndugu yetu aliyefariki kifo cha kutatanisha

Nachojua mzazi ni Mungu wa 2 duniani mzazi akisikitika tu mambo yako hayataenda muombeni msamaha aise kabla hajaondoka duniani huyo mzee..anywys poleni...lakini kwanini msiache lipite mmkabidhi Mungu jambo hili?

Koo zinazoamini haya mambo mie naogopa hata ujirani nao aise🙌
 
Ndugu, hao Wataalam watawaletea Mtafaruku mkubwa zaidi kwa ninyi mliobaki. Ndugu yenu ameshafariki, jengeni amani baina yenu ninyi mliobaki.

Ukweli ni kuwa kamwe hatorudi. Ameshalala. Na nadhani, mwenye maumivu zaidi ni baba mzazi kuliko ninyi ndugu. Msiendelee kumuumiza.

Kama kakataa achaneni naye. Badala yake ninyi mkae kwa tahadhari.

Mengine yote hayana msingi kwa sasa.
 
Hapo mmekwama kwani hitajilenu Ni lipi?
1. Kumrejesha mpendwa wenu au
2. Kumtafuta aliye muua

Kama hitajilenu ni kumrejesha mpendwa wenu mbona mnatakakumhukumu mpendwa wenu mwingine (baba)

Kama ni kumtafuta aliye muua uzi usomeke hivi "tunataka kuua alie muua mpendwa wetu"

Nb: hata aliye muua mpendwa wenu hawezi kumrejesha.
 

Ufu 14:13 SUV​

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
 
Wewe unasema wataalamu wamemtaja Baba Mzazi. Halafu tena unakuja kwetu kukusaidie kupata wataalamu wengine!Mkuu unazingua. Na mimi nikisem ni mtaalamu na nimegundua muuaji ni wewe ntakuwa nasema urongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…