PreGE2025 Mrema: Kauli za Lissu na Lema zinaleta hofu ya kujieleza CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Unayo katiba ya chama inayosema, mwanachama au kiongozi akitaka kuongea na wanachama wengine ni lazima aombe ruhusa ya mweyekiti?
Ndiyo: Kutoka katiba ya Chadema Sura ya Saba (7), Ibara 7.6( Majukumu ya Viongozi wakuu wa Chama), kipengele cha 7.6.1 (Wenyeviti), sehemu iii. Kuwa msemaji Mkuu wa masuala ya Chama kwangazi yake baada ya kushauriana na Katibu Mkuu/ Katibu, kamati ya utendaji/kamati kuu ama secretariati ya ngazi husika.
===
Leta swali lingine.
 
“Pamoja na kupokea wito wa kushiriki mkutano huo maalum, sisi -wagombea ubunge wa 2020 na watiania wa ubunge wa 2025 – tumeona kuna viashiria vya kutopewa au kutopata nafasi ya kutosha kusikilizwa katika mkutano huo maalum, na kwa hiyo, tumeamua kukuandikia Waraka huu, kwasababu zifuatazo: Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe Tundu Lissu, akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Iringa ametamka wazi kuwa, “wote wanaoona, “No Reforms, No Elections” haiwezekani ni wana-CCM pamoja na vibaraka wao”. Kauli hii ya Mwenyekiti tayari imezuia uhuru wetu wa kutoa maoni au ushauri mbadala dhidi ya “No Reforms, No Elections”, kwani, kwa mujibu wa Mwenyekiti wetu, watu wa namna hiyo ni wana-CCM au vibaraka wao. Aidha Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Chama ya kuchangisha fedha kwaajili ya “No Reforms, No Elections”, Mhe Godbless Lema, akihutubia mkutano jijini Arusha, amenukuliwa akisema kwamba “wote wanaotaka ubunge au udiwani bila reforms waondoke CHADEMA”. Kauli hii ya Mhe. Lema ya kufukuza watu wenye maoni mbadala ndani ya Chama, haijakanushwa na Chama, na inazidi kuondoa mantiki ya mkutano huo maalum wa kujadili mwenendo wa “No Reforms, No Elections”, kwani tayari washiriki tumewekewa mipaka na vitisho katika kujadili suala hilo”, - Mrema.

John Mrema, mmoja wa wanaounda kundi la G-55 ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akisoma waraka wao kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA wakati akizungumza na wanahabari kwa niaba ya wenzake ambao baadhi walikuwapo eneo hilo mkoani Dar es Salaam siku ya Jumapili Aprili 6, 2025

View attachment 3294789
Mrema: Ni no reforms No Erection na siyo No reforms No Election.
 
Ndiyo: Kutoka katiba ya Chadema Sura ya Saba (7), Ibara 7.6( Majukumu ya Viongozi wakuu wa Chama), kipengele cha 7.6.1 (Wenyeviti), sehemu iii. Kuwa msemaji Mkuu wa masuala ya Chama kwangazi yake baada ya kushauriana na Katibu Mkuu/ Katibu, kamati ya utendaji/kamati kuu ama secretariati ya ngazi husika.
===
Leta swali lingine.
Je alikwambia alikuwa anakisemea chama????
Angalia contents, kusemea chama kwa ngazi husika(waliitwa wanachama wa Chadema ili kuelezwa maswala ya chama kwa ngazi hiyo.??) vs individual kuongea mambo yake na misimamo yake bila kutumia chama.

2: Kilikuwa kikao cha ngazi gani cha chama?? Au mkutano upi kwa jina la chama?
 
“Pamoja na kupokea wito wa kushiriki mkutano huo maalum, sisi -wagombea ubunge wa 2020 na watiania wa ubunge wa 2025 – tumeona kuna viashiria vya kutopewa au kutopata nafasi ya kutosha kusikilizwa katika mkutano huo maalum, na kwa hiyo, tumeamua kukuandikia Waraka huu, kwasababu zifuatazo: Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe Tundu Lissu, akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Iringa ametamka wazi kuwa, “wote wanaoona, “No Reforms, No Elections” haiwezekani ni wana-CCM pamoja na vibaraka wao”. Kauli hii ya Mwenyekiti tayari imezuia uhuru wetu wa kutoa maoni au ushauri mbadala dhidi ya “No Reforms, No Elections”, kwani, kwa mujibu wa Mwenyekiti wetu, watu wa namna hiyo ni wana-CCM au vibaraka wao. Aidha Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Chama ya kuchangisha fedha kwaajili ya “No Reforms, No Elections”, Mhe Godbless Lema, akihutubia mkutano jijini Arusha, amenukuliwa akisema kwamba “wote wanaotaka ubunge au udiwani bila reforms waondoke CHADEMA”. Kauli hii ya Mhe. Lema ya kufukuza watu wenye maoni mbadala ndani ya Chama, haijakanushwa na Chama, na inazidi kuondoa mantiki ya mkutano huo maalum wa kujadili mwenendo wa “No Reforms, No Elections”, kwani tayari washiriki tumewekewa mipaka na vitisho katika kujadili suala hilo”, - Mrema.

John Mrema, mmoja wa wanaounda kundi la G-55 ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akisoma waraka wao kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA wakati akizungumza na wanahabari kwa niaba ya wenzake ambao baadhi walikuwapo eneo hilo mkoani Dar es Salaam siku ya Jumapili Aprili 6, 2025

View attachment 3294789
Kwa Chadema hii, hizi zote ni kelele tu hazina mashiko. Chadema inashikiliwa na wanachama na Lissu, Heche na Lema... Waliobaki ni wafuata upepo tu hawana madhara wala dalili za madhara. Angalia tu turn out ya watu kwenye mikutano.

Hebu leo Mrema huyo aitishe mkutano wa hadhara, matokeo atakayoyapata ndio nguvu yake kwenye chama
 
Watu walioweza kumchagua Lissu kuwa kiongozi wao mkuu ni wehu tu, mtu mwenye akili hawezi kufanya hivyo. Lisuu hafai kuwa kiongozi, mtaelewa siku akikizika Chadema

Lissu ni kiboko. Kamstaafisha Mbowe siasa kwa lazima.
 
Back
Top Bottom