Uchaguzi 2020 Mrema (TLP), Mbatia (NCCR), Kimei (CCM) na Kiwelu (CHADEMA) wafanya kampeni za ubunge Vunjo (K'Njaro) kuwa zenye ushindani mkali kuwahi kutokea

Kimei atapewa kura na watu wa Marangu mtoni, Mrema atapewa na watu wa Kilema na Mbatia Kirua, kura za nyongeza zitatoka Kahe, Mwika n.k
 
ilipofikia sasa ni vyema kumpa mtu za uso tu[emoji28][emoji28],namkubali magu kwa hili.

maana hatuwezi lea ugonjwa kisa dawa chungu.
Mkichagua wapinzani sileti maji,stupid
 
Wanaume ndo wana nafasi kubwa hapo hasa Mbatia na Mrema.
 
ilipofikia sasa ni vyema kumpa mtu za uso tu[emoji28][emoji28],namkubali magu kwa hili.

maana hatuwezi lea ugonjwa kisa dawa chungu.
Nitawashangaa sana wapinzani watakao jinadi kwa wananchi kwamba serikali haijafanya kazi ilihali wamekua wabunge kwa miaka na hakuwahijua hizo kero
 
Nimeshangaa ktk kampeni mbatia anaahidi tena alivyoahidi 2015...
Unamshangaa Mbatia, umeshindwa kumshangaa Meko na CCM wanao rudia ahadi tangu uhuru.

Tangu Nyerere maadui ni ujinga, umasikini na maradhi. Ndio maana kampeni za CCM miaka yote ni maji, miundombinu, umeme, elimu nk, yale yale.

Hivi kwa akili ya kawaida ukae na adui yako miaka 60 huja muangamiza, huyo si amekuwa rafiki yako sasa!!
 
Hivi lile fungu na mbeleko CCM B , enisisira wiki chache kabla kuvunjwa Bunge ule upepo wa dharula uliishia wapi?
 
Ahadi nyingine bhana...sasa utatenbea uchi wapi, au humu jf?[emoji28]
[emoji23][emoji23][emoji23] kwani inashindikana mkuu?! Si anapost picha akiwa anatembea uchi... [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Muwe mnatafakari hata kidogo kabla ya kuchangia. Hivi kuna mbunge wa CCM (yoyote yule) anayewakilisha kero/changamoto/mahitaji ya wapiga kura kama wa upinzani?

Sababu kubwa ya kutoa bunge live ilikuwa kuzuia wananchi wasione jinsi wapinzani wanavyo wasemea ili kuwanyima political mileage.

Pia serikali ina organs nyingi sana za kuwakilisha hizo kero mbali na mbunge.

Hivi idara ya elimu haiwasilishi reports za upungufu wa madarasa/walimu/vifaa vya kufundishia?

Idara ya afya haiainishi changamoto zake? TANROADS na TARURA hawapeleki changamoto za miundombinu? nk nk.

Sasa ni vipi jitu moja lije liseme eti huyu mpinzani hajawasilisha kero zenu nanyi mnaliamini? Na vipi majimbo ambayo yanayokaliwa na CCM tangu uhuru, yote yana maendeleo? Hapo shida sio wabunge wa CCM?[emoji116][emoji116]

Hayo maendeleo ni wajibu wa serikali kupeleka kwa kuwa wanakusanya kodi za hao wananchi. Angesema pia basi kuwa hatakusanya kodi majimbo ya upinzani, kodi unakusanya bila kuuliza kadi za chama then maendeleo ndio unajua kuwa kuna upinzani? Roho za kishetani kabisa.[emoji116][emoji116]
Ndio maana wanaambiwa wakirudia kuwachagua maendeleo hakuna
 

Muwe mnatafakari hata kidogo kabla ya kuchangia. Hivi kuna mbunge wa ccm (yoyote yule) anayewakilisha kero/changamoto/mahitaji ya wapiga kura kama wa upinzani?

Sababu kubwa ya kutoa bunge live ilikuwa kuzuia wananchi wasione jinsi wapinzani wanavyo wasemea ili kuwanyima political mileage.

Pia serikali ina organs nyingi sana za kuwakilisha hizo kero mbali na mbunge.

Hivi idara ya elimu haiwasilishi reports za upungufu wa madarasa/walimu/vifaa vya kufundishia?

Idara ya afya haiainishi changamoto zake? TANROADS na TARURA hawapeleki changamoto za miundombinu? nk nk.

Sasa ni vipi jitu moja lije liseme eti huyu mpinzani hajawasilisha kero zenu nanyi mnaliamini? Na vipi majimbo ambayo yanayokaliwa na ccm tangu uhuru, yote yana maendeleo? Hapo shida sio wabunge wa ccm?

Hayo maendeleo ni wajibu wa serikali kupeleka kwa kuwa wanakusanya kodi za hao wananchi. Angesema pia basi kuwa hatakusanya kodi majimbo ya upinzani, kodi unakusanya bila kuuliza kadi za chama then maendeleo ndio unajua kuwa kuna upinzani? Roho za kishetani kabisa.
 
Jitu baya kuliko wote ni lile linaloongea bila kujua kazi ya madiwani na wabunge katika kuwasilisha mahitaji ya wananchi, kama wewe.

Halafu hapa tunamuengelea John Pombe Magufuli na utendaji wa serikali yake, hatuongelei CCM tangu uhuru wala CHADEMA tangu 1992
Cc mkorinto
 
kazi ya mbunge ni ipi?
Kazi ya mbunge ni kuwakilisha kero, changamoto, matatizo ama mahitaji ya jimbo husika.

Hapo nimeongea kwa muktadha wa jimbo tu achana na zile za kitaifa za kuisimamia, kuikosoa na kuishauri serikali, kutunga sheria nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…