Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika, Julitha Kabete ameondoka leo kuelekea nchini Nigeria katika fainali ya michuano hiyo inayofanyika Novemba 26 mwaka huu huku akiwaahidi watanzania kwua ataipeperusha vyema bendera ya Tanzania .
Akizungumza kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Kabete amesema kuwa lengo lake ni kuwa mmoja wa wawakilishi bora katika shindano hilo na kuitangaza vyema nchini pamoja na kurudi taji hilo na kwa kupitia kampuni ya Millen Magese Group chini ya Mkurugenzi wake ,Happiness 'Millen' Magese ameshukuru kwa kuingia nae mkataba ili aweze kushiriki michuano hiyo na kufanya Kazi nyingine za urembo.
"Mimi kama mwakilishi wa Tanzania nitahalikisha anafanya vizuri katika shindano hilo, ambalo nimepata nafasi ya kuwa mpeperusha bendera wa nchini yangu Tanzania " amesema. Kabete alikabidhiwa bendera ya taifa na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye.