Mc cane
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 5,570
- 10,517
Mafisi wapo kila kona![]()
Jacqueline Obeid ‘Posh Queen’
SITAKI!
Mlimbwende matata mitandaoni (socialite) wa Bongo, Jacqueline Obeid ‘Posh Queen’ ambaye hivi karibuni alitengeneza vichwa vya habari mitandaoni baada ya kuwa ni msichana mwenye umbo kali aliyemaliza Stashahada ya Insurance and Risk Management katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha jijini Dar, amesema hataki kuajiriwa kwani anajua atakavyosumbuliwa.
Posh aliiambia Over Ze Weekend kuwa, anamshukuru Mungu kwani hata alipokuwa chuoni alikuwa ameshaanza kufanya biashara hivyo baada ya kumaliza chuo atajiari mwenyewe. “Sitaki kuajiriwa maana najua nitakayokutana nayo. Ni bora kujiajiri mwenyewe nitakuwa huru na umbo langu,” alisema Posh mwenye mzigo wa maana nyuma.
Akiwakimbia kibaruani atawapata kwenye biashara na shughuli nyingine
Kuna mafisi ma supplier wa malighafi (raw materials)
Kuna mafisi Wanunuzi wa bidhaa (soko)
Kuna mafisi Wakusanya kodi
Kuna mafisi wakagua na wadhibiti ubora wa bidhaa
Hivyo popote atakapokuwa ajipange
Lakini kubwa ninaloliona yeye mwenyewe anajiweka katika mazingira ya kukaribisha mafisi