Mrisho Gambo acha Unafiki

Mrisho Gambo acha Unafiki

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Kama kuna mambo yanachukiza basi ni huu unafiki wa kiwango cha SGR. Moderator naomba msifute.

Hivi karibuni huyu kijana ameonekana "akijaribu" kwa kiwango kikubwa sana kujitenganisha na Utawala katili na dhalimu wa Magufuli, kitu ambacho hakijui ni kwamba hawezi kukwepa sehemu udhalimu huo.

Jana alisikika "akikandia" uporwaji wa Bureaus uliofanywa na serikali ya Magufuli huku yeye akiwa Mkuu wa Mkoa husika na akakaa kimya kwa wakati huo! Jana anadai kuwa kitendo hicho hakikua cha kibidamu.

Leo ameibuka tena baada ya watu wenye akili kuhoji kauli zake hizo, Leo anadai kuwa UTAWALA ule haukumpa nafasi yeye kama RC kutenda haki na majukumu yake yalitekelezwa na "Junior" wake kwa kisingizio cha "maelekezo kutoka juu".

Namkumbusha Gambo kuwa, hata huo Ubunge alionao Leo hapo anajua fika kuwa hakustahili kuwepo hapo, hivyo namshauri AJENGE HOJA aache kutukumbusha machungu ya ndugu zetu waliofilisiwa na Utawala dhalimu wa mwendazake

2809233_Don_Mbowe_on_Instagram_15_February_2019..0A.0AVitu_vya_kuogopa_Sana_Hapa_Duniani_ni_Mu...jpg
 
Yupo sahihi kwa upande wake, Magu na yeye alikuwa sahihi kwa hiyo style yake ya utendaji, mkuu wa mkoa sio raisi wa mkoa, anaweza kuendeshwa na Raisi vile impendezavyo raisi.
Hapana, yeye anadai aliendeshwa na junior, rais sio junior kwa RC
 
Kama kuna mambo yanachukiza basi ni huu unafiki wa kiwango cha SGR. Moderator naomba msifute.

Hivi karibuni huyu kijana ameonekana "akijaribu" kwa kiwango kikubwa sana kujitenganisha na Utawala katili na dhalimu wa Magufuli, kitu ambacho hakijui ni kwamba hawezi kukwepa sehemu udhalimu huo.

Jana alisikika "akikandia" uporwaji wa Bureaus uliofanywa na serikali ya Magufuli huku yeye akiwa Mkuu wa Mkoa husika na akakaa kimya kwa wakati huo! Jana anadai kuwa kitendo hicho hakikua cha kibidamu.

Leo ameibuka tena baada ya watu wenye akili kuhoji kauli zake hizo, Leo anadai kuwa UTAWALA ule haukumpa nafasi yeye kama RC kutenda haki na majukumu yake yalitekelezwa na "Junior" wake kwa kisingizio cha "maelekezo kutoka juu".

Namkumbusha Gambo kuwa, hata huo Ubunge alionao Leo hapo anajua fika kuwa hakustahili kuwepo hapo, hivyo namshauri AJENGE HOJA aache kutukumbusha machungu ya ndugu zetu waliofilisiwa na Utawala dhalimu wa mwendazake

DAH BEST UKO SAHIHI SANA, DHULUMA ALIYOFANYIWA LEMA NA KUKAA KISONGO KWA MDA MREFU UKU DHAMANA ZAKE ZIKIFANYIWA UHUNI ILIKUWA IKIRATIBIWA NA GAMBO.

ZAIDI NIMESHANGAA UNAFIKI WA WABUNGE WA CCM KUIKOSOA TFF KTK UCHAGUZI WAO UNAOTARAJIWA ATI WANADAI HAKI ITENDEKE WAKATI WOTE WABUNGE WALIOKO KTK BUNGE HILI NI ZAO LA HARAMU NA HARAMU ILIYO RATIBIWA NA DIKTETA MAGUFULI.

MWISHO TUMSHUKURU SANA MUNGU KWA KULIONDOA LILE LIDIKTETA JPM, MUNGU WETU ANA HURUMA SANA NA SISI, ALITUONEA HURUMA WATANZANIA KWANI ALIJUA KAMA DIKTETA MAGUFULI ANGEENDELEA KUWEPO SINCERELY ANGEANZA KUTULA NYAMA ZETU KWANI ALIFURAIA MATENDO YA HAWA AKINA SABAYA, UYU GAMBO, IGP, HAWA WASIOJULIKANA N.K KUTUDHURU NA KUWA POTEZA WATU NA NDIO HATA HAKUWA AKIWAKEMEA
 
Kuna siku jiwe alisema

"Na wengine hamkuchaguliwa na wananchi"

Kweli ushirika wa wachawi haudumu! Je Mrisho na wengine wengi walikubali kunajisi masanduku ya kura kwa maslahi yao kwa miaka 5??

Watanzania kwa miaka hii mitano watayajua mengi yaliyopandikizwa October 2020..
 
Back
Top Bottom