Mrisho Gambo acha Unafiki

Mrisho Gambo acha Unafiki

Sijakataa ila kwanini aseme Leo? Tutaaminije maneno yake? Je, kama aliweza kugeuka na kuyasema haya, tunajua kesho atasema nini? Kelele zake hazisaidii tena
Una hoja nzuri sana. Unafiki unaitafuna Tanzania. Hawa wote walitakiwa wasiwepo tena kwenye uongozi wa aina yoyote. Sikumpenda Magufuli kwa sababu ya uongozi wake ila nimebaki kumuonea huruma sana kwani alidhani kina Lema ndiyo maadui zake akafanya kila hila ili wasipate tena ubunge na kuwapa sampuli ya kina Gambo, kumbe ndiyo walikuwa wabaya wake. Ila huyu jamaa kwa wale wanaojua kusoma haiba za watu kila nikimwangalia naona kabisa ni mpigaji fulani aliyejiingiza kwenye siasa tu. Hana sifa za kuwa kiongozi kabisa.
 
Ivi mnadhani kwenye utawala wa yule dhalimu Kuna mtu ambae angethubutu kwenda kinyume chake?? Au mmesahau yaliyomkuta Nape Nnauye na wengineo wengi
Kwanini hakujiuzulu kwa sababu zozote zisizohusiana na kukataa kutii maagizo yenye nia OVU?

Mbona kuna mkuu wa wilaya alishawahi kukataa uteuzi na hakuchukuliwa hatua zozote za kisasi?

Kama kulikuwa hakuna mtu aliyekuwa na uthubutu wa kupinga utekelezaji wa jambo fulani ambalo lingeleta athari kwa jamii au taswira ya serikali kwanini aanze kutapika nyongo mbele za watu wengine wasiohusika wakati aliyetakiwa asemwe hivyo hayupo tena kujitetea?

Baadhi ya wabunge ni wanafiki na hawako kwa ajili ya kutumikia wananchi ila matumbo yao tu.

Ni bora Godbless Lema arudishwe jimbo la Arusha ama kwa uchaguzi mdogo au uchaguzi mkuu maana huyu hana anachokisimamia.

Kama aliweza kukaa kimya kisha kushurutishwa kufanya vitendo wakati akijua ni kinyume na sheria anatakiwa awajibishwe kama alivyofanyiwa Lengai Ole Sabaya maana alimtesa sana Lema huyu. Hafai hapo arudi akagombee Kibaha vijijini kwao
 
Lakini ameongea ukweli mtupu

Ni kweli, ila yeye ni mfaidika wa moja kwa moja wa huyo dhalimu aliyepora hela za watu wa Bureau de change. Aliyepora fedha za Bureau de change, ndio aliyeagiza pia Gambo atangazwe mbunge wa huko Arusha mjini. Kama kweli hakuwa sehemu ya uporaji ule wa Bureau de change, aachie ubunge kwani pia hakuupata kihalali.
 
Kama aliweza kukaa kimya kisha kushurutishwa kufanya vitendo wakati akijua ni kinyume na sheria anatakiwa awajibishwe kama alivyofanyiwa Lengai Ole Sabaya maana alimtesa sana Lema huyu. Hafai hapo arudi akagombee Kibaha vijijini kwao
Yes, ina maana kama ananunulika kirahisi hivyo au kama hana nguvu ya kusimamia anachokiamini basi hata ubunge haumfai maana anaweza kuwa manipulated kama alipokua RC!
 
Ni kweli, ila yeye ni mfaidika wa moja kwa moja wa huyo dhalimu aliyepora hela za watu wa Bureau de change. Aliyepora fedha za Bureau de change, ndio aliyeagiza pia Gambo atangazwe mbunge wa huko Arusha mjini. Kama kweli hakuwa sehemu ya uporaji ule wa Bureau de change, aachie ubunge kwani pia hakuupata kihalali.
Yes! Hapa ndio patamu
 
Anachofanya Gambo ni kujaribu kubadili sura na mtazamo walio nao watu juu yake
Mapema kabla miaka haijasogea songea

Ili miaka ikisogea awe kwenye uhusika mwingine kabisa na watu wamuone anafaa kuendelea na awamu nyingine

kwa kuwa mtetezi wake amesharudisha namba lazima apambane na hali yake mbeleko hakuna tena na huwenda akafanikiwa sana raia wanasahau haraka sana

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini hakujiuzulu kwa sababu zozote zisizohusiana na kukataa kutii maagizo yenye nia OVU?

Mbona kuna mkuu wa wilaya alishawahi kukataa uteuzi na hakuchukuliwa hatua zozote za kisasi?

Kama kulikuwa hakuna mtu aliyekuwa na uthubutu wa kupinga utekelezaji wa jambo fulani ambalo lingeleta athari kwa jamii au taswira ya serikali kwanini aanze kutapika nyongo mbele za watu wengine wasiohusika wakati aliyetakiwa asemwe hivyo hayupo tena kujitetea?

Baadhi ya wabunge ni wanafiki na hawako kwa ajili ya kutumikia wananchi ila matumbo yao tu.

Ni bora Godbless Lema arudishwe jimbo la Arusha ama kwa uchaguzi mdogo au uchaguzi mkuu maana huyu hana anachokisimamia.

Kama aliweza kukaa kimya kisha kushurutishwa kufanya vitendo wakati akijua ni kinyume na sheria anatakiwa awajibishwe kama alivyofanyiwa Lengai Ole Sabaya maana alimtesa sana Lema huyu. Hafai hapo arudi akagombee Kibaha vijijini kwao
angejiuzulu watoto zake ungewalisha wewe mkuu??au kuongea Ni Rahisi sana!,
Yaan we imekuuma sana Gambo kusema uovu ambao walitendewa watanzania wenzenu kwa kuporwa fedha zao kwenye berue de change??? Ivi nyie mandondocha ya mwendazake mna tatizo gani??!
 
Kama kuna mambo yanachukiza basi ni huu unafiki wa kiwango cha SGR. Moderator naomba msifute.

Hivi karibuni huyu kijana ameonekana "akijaribu" kwa kiwango kikubwa sana kujitenganisha na Utawala katili na dhalimu wa Magufuli, kitu ambacho hakijui ni kwamba hawezi kukwepa sehemu udhalimu huo.

Jana alisikika "akikandia" uporwaji wa Bureaus uliofanywa na serikali ya Magufuli huku yeye akiwa Mkuu wa Mkoa husika na akakaa kimya kwa wakati huo! Jana anadai kuwa kitendo hicho hakikua cha kibidamu.

Leo ameibuka tena baada ya watu wenye akili kuhoji kauli zake hizo, Leo anadai kuwa UTAWALA ule haukumpa nafasi yeye kama RC kutenda haki na majukumu yake yalitekelezwa na "Junior" wake kwa kisingizio cha "maelekezo kutoka juu".

Namkumbusha Gambo kuwa, hata huo Ubunge alionao Leo hapo anajua fika kuwa hakustahili kuwepo hapo, hivyo namshauri AJENGE HOJA aache kutukumbusha machungu ya ndugu zetu waliofilisiwa na Utawala dhalimu wa mwendazake

Acha ujinga.Kwa hiyo unataka akumbate upompompo?Jirekebishe kenge weye!🤣🤣🤣
 
Mwanaharakati huru alisema "ili kuwa ccm lazima uwe na PhD ya unafiki, ukiwa na PhD ya unafiki utakuwa mwanaccm mzuri sana"....tuvumiliane tukiwa tunahamisha akili kutoka filosofia za mwendazake na kuhamia kwa "mama"🤸🤣🐒
 
Ni kweli, ila yeye ni mfaidika wa moja kwa moja wa huyo dhalimu aliyepora hela za watu wa Bureau de change. Aliyepora fedha za Bureau de change, ndio aliyeagiza pia Gambo atangazwe mbunge wa huko Arusha mjini. Kama kweli hakuwa sehemu ya uporaji ule wa Bureau de change, aachie ubunge kwani pia hakuupata kihalali.
Ila Magufuli mimi huwa naamini kabisa alikuwa na ugonjwa fulani wa akili. Hivi watu kama kina Gambo, Kigwangala, Makonda, Sabaya, Muro etc mbona ukiwatazama na kufuatilia aina ya uongozi wao unajua kabisa hapa hamna kitu, ni watu wanafiki wanaoishi kijanja janja? Si walisema alikuwa ameweka wana usalama kila mahali? Yule baba aliharibu sana hii nchi. Naona na mamayetu naye kuna majaribio ya kuwekwa ''mtu kati'' na wapambe hivyo asipoangalia atapotea vibaya sana. Ogopa sana watu wanaokusifu kupitiliza.
 
huyu anafikiri anaweza kupendwa na watu wa Arusha kiasi cha kumpa msimu mwingine? jamaa hmna kitu na humu ndani kunna watu wake wanampigia chepuo hapo hakuna kitu anaonekana kama MSALITI hata afanye nini? hana jipya!
 
Ila Magufuli mimi huwa naamini kabisa alikuwa na ugonjwa fulani wa akili. Hivi watu kama kina Gambo, Kigwangala, Makonda, Sabaya, Muro etc mbona ukiwatazama na kufuatilia aina ya uongozi wao unajua kabisa hapa hamna kitu, ni watu wanafiki wanaoishi kijanja janja? Si walisema alikuwa ameweka wana usalama kila mahali? Yule baba aliharibu sana hii nchi. Naona na mamayetu naye kuna majaribio ya kuwekwa ''mtu kati'' na wapambe hivyo asipoangalia atapotea vibaya sana. Ogopa sana watu wanaokusifu kupitiliza.
Hahahaha
 
Hakuna cha unafiki, Gambo kaongea ukweli
Wafanyabiashara wa Maduka ya fedha Arusha ni wapiga kura wake lazima awatetee
Nani asiyejua kuwa Magufuli alikuwa mtawala katili, nani angefurukuta enzi zake?
Huu ni muda wa kurekebisha makosa
 
Kama kuna mambo yanachukiza basi ni huu unafiki wa kiwango cha SGR. Moderator naomba msifute.

Hivi karibuni huyu kijana ameonekana "akijaribu" kwa kiwango kikubwa sana kujitenganisha na Utawala katili na dhalimu wa Magufuli, kitu ambacho hakijui ni kwamba hawezi kukwepa sehemu udhalimu huo.

Jana alisikika "akikandia" uporwaji wa Bureaus uliofanywa na serikali ya Magufuli huku yeye akiwa Mkuu wa Mkoa husika na akakaa kimya kwa wakati huo! Jana anadai kuwa kitendo hicho hakikua cha kibidamu.

Leo ameibuka tena baada ya watu wenye akili kuhoji kauli zake hizo, Leo anadai kuwa UTAWALA ule haukumpa nafasi yeye kama RC kutenda haki na majukumu yake yalitekelezwa na "Junior" wake kwa kisingizio cha "maelekezo kutoka juu".

Namkumbusha Gambo kuwa, hata huo Ubunge alionao Leo hapo anajua fika kuwa hakustahili kuwepo hapo, hivyo namshauri AJENGE HOJA aache kutukumbusha machungu ya ndugu zetu waliofilisiwa na Utawala dhalimu wa mwendazake

Gambo yuko sahihi... RC mstaafu wa Kilimanjaro, Mama Anna analijua hili vizuri sana toka kwa askari mgambo wa mwendazake, baradhuli Sabaya
 
Back
Top Bottom