Mrisho Gambo ataka Bunge liahirishwe, kujadili mfumuko wa bei

Mrisho Gambo ataka Bunge liahirishwe, kujadili mfumuko wa bei

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo leo Ijumaa Aprili 8, 2022 ametoa hoja akitaka bunge liahirishe shughuli zake ili wabunge wajadili kwa kina kuhusu upandaji wa bei za bidhaa nchini ikiwemo vyakula na vifaa vya ujenzi.
 
Wazo zuri, tatizo hao wanaopaswa kujadili suluhisho ndio walioanzisha hayo matatizo. Sasa tusitarajie wamiliki wa vituo vya mafuta, hardware stores na mashamba waliojaa humo bungeni kuja na suluhisho lolote litakalofanya wapate hasara.

Kupanda huku kwa bei wanufaika wakubwa ni wao na washirika wao.
 
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo leo Ijumaa Aprili 8, 2022 ametoa hoja akitaka bunge liahirishe shughuli zake ili wabunge wajadili kwa kina kuhusu upandaji wa bei za bidhaa nchini ikiwemo vyakula na vifaa vya ujenzi.
Wakijadili ndio bei zitashuka? Unless wao wakubali kufyekwa mapato yao kufidia mapato ambayo serikali itapoteza in case wanaondoa au kupunguza Kodi kadhaa..
 
Wenzake wako busy wana taka plate namba za magari yao ili wasisumbuliwe na polisi.. Ccm bwana!!!
 
Huu ni ujanja wa kutaka kuongeza siku za kukaa Bungeni kwenye mkutano huu wa Bajeti
Kweli mkuu maana hakuna asiyejua kwamba kuna mfumuko wa Bei sio tuu Tanzania bali Dunia yote na sababu zinafahamika..

Pili mfumuko wa bei kwa Tzn imeshuka kidogo kutoka 4.2 mwezi Desemba hadi 3.7 mwezi machi..

Mfano bando ya Bati za rangi imepungua kutoka 459,000 mwezi tajwa hadi wastani wa 432,000 kwa sasa..

Kwenye vyakula bei zitazidi kupungua kwa sababu tunaelekea msimu wa mavuno,walo mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ni mashahidi kwamba Bei za vyakula zimeanza kupungua.
 
Wakijadili ndio bei zitashuka? Unless wao wakubali kufyekwa mapato yao kufidia mapato ambayo serikali itapoteza in case wanaondoa au kupunguza Kodi kadhaa..
CHAWA huyu anaupiga mwingi sana kwakweli, kwa niaba ya wa-TZ wezangu wote mliopo ndani na nnje ya JF, napendekeza awe anapewa kipato kikubwa sana kuliko CHAWA wengine wote [emoji87]
 
Back
Top Bottom