Pre GE2025 Mrisho Gambo: Barabara ya Esso - Long'Dong Arusha mjini kujengwa kwa kiwango cha lami

Pre GE2025 Mrisho Gambo: Barabara ya Esso - Long'Dong Arusha mjini kujengwa kwa kiwango cha lami

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Serikali kupitia uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imechukua hatua za kuboresha miundombinu ya barabara kwa kuhakikisha ujenzi wa barabara ya Esso - Long’dong mkoani Arusha, yenye urefu wa kilomita 1.8 unaanza hivi karibuni. Barabara hii inayounganisha Kata ya Unga Limited na Kata ya Sokon 1, itajengwa kwa kiwango cha lami ili kuondoa changamoto ya muda mrefu kwa wakazi wa maeneo hayo.

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo, akizungumza katika hafla ya uhamasishaji wa elimu ya nishati safi kwa viongozi wa Baraza la Wazee wa Jiji la Arusha, amesema kuwa Rais Samia alimtuma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais– TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, kufuatilia utekelezaji wa mradi huo.

Amesema kwa sasa, mkandarasi ameshapatikana na yupo tayari kuanza kazi na kwamba gharama za ujenzi wa barabara hiyo ni Shilingi bilioni 3.135, na kwa mujibu wa taratibu za manunuzi, mkandarasi anatarajiwa kuingia kazini ndani ya mwezi huu, au ifikapo tarehe 15 Machi 2025.

Gambo ameeleza kuwa wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakihitaji barabara hiyo kwa muda mrefu, na baadhi yao wamejitolea hadi kuvunja nyumba zao kwa gharama zao wenyewe ili kuruhusu upanuzi wake. Amemshukuru Rais Samia kwa juhudi zake za kuboresha miundombinu na kusisitiza kuwa kazi yake inapaswa kuendelea kwa kipindi kingine cha miaka mitano ili miradi inayotekelezwa iwe ya kudumu.

"Kama kuna mtu anadhani hii ni kazi nyepesi, anapoteza muda, kwa sababu matendo ya Rais Samia yanaishi, yanaonekana. Hatuhitaji mtu wa kuja kujifunza au kupiga porojo, tunamhitaji mtu anayejua anachokifanya, ambaye ni Rais Samia," amesema Gambo.

 
Back
Top Bottom