Uchaguzi 2020 Mrisho Gambo: Kwa gharama yoyote lazima Jimbo la Arusha lirudi CCM

Uchaguzi 2020 Mrisho Gambo: Kwa gharama yoyote lazima Jimbo la Arusha lirudi CCM

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Ohoooo Gambo Anasema CCM wafanye vurugu ili Jimbo tu la Arusha lirudi CCM! Msisitizo, Wafanye hata Vurugu..... Hii kauli ingetolewa na Upinzani mmmmghh..

Leo May 27, 2018 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amefungua semina ya umoja wa wanawake wa wilaya ya Arusha mjini ( UWT) yenye lengo la kuwajengea uwezo ikiwa ni pamoja na kuelekezana namna ya kutimiza majukumu yao pamoja na mada za kuwajengea uwezo.

Gambo amesema jimbo la Arusha mjini haliwezi kugawanywa kama inavyozungumzwa na katika uchaguzi ujao kwa gharama yoyote jimbo hilo litakuwa la CCM
 
Hawa wapo tayari hata kuua ili mradi washinde uchaguzi, na wanajua kabisa kwamba hawapendwi ila wanalazimisha. Upinzani nao wapo kwa ajili ya kujipendendekeza kama alivyofanya Lema kwa huyo Gambo eti wamezika tofauti zao, ilitakiwa watu waambiwe kuwa hawa sio wenzetu.
 
Nimejiunga CCM Rasmi ili kukitafutia chama Kura mwaka 2020. Hakika nimeziunga Juhudi Za Rais Wangu Magufuli katika kuiletea Tanzania Maendeleo. Na Maendeleo hayana Vyama.
 
Kauli mbiu ya magufuli hiyo maendeleo mtayasikia huko kwa kenyatta huku tunawekeza kwenye kutawala tu.

Yakiambiwa yameiba kura,kukimbia na viapo kupiga wapinzani yanabisha yenyewe yanatoa siri.
 
Nimejiunga CCM Rasmi ili kukitafutia chama Kura mwaka 2020. Hakika nimeziunga Juhudi Za Rais Wangu Magufuli katika kuiletea Tanzania Maendeleo. Na Maendeleo hayana Vyama.
Mkawaamshe na wakina moses machali na kafulila sijui katambi anafanya nini huko? Muendelee kuongeza idadi ya kura
 
Sijui ni kwa nn hii nchi inaonekana inaendeshwa na maRC wa dar na arusha? Yaani kiongozi wa serikali anatoa kauli hiyo na hadi sasa Rais hajatengua uteuzi.

Mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa anatoa kauli hiyo lakini si m/kiti wa chama taifa wala katibu wake aliyejitokeza na kulaani au hata kufuta nafasi yake kama mjumbe wa kamati ya siasa.

Si vyombo vya dola wala waziri anayekemea, wote wanapima upepo maana unaweza kujifanya kimbele mbele kukemea na matokeo yake ww ndo ukafukuzwa kazi.

Kama TRA, waziri wa fedha vs RC wa dar. Kila mtu kichwa chini. Angalau zamani walikuwa wanawafukuza waandishi wa hbr kwenye vikao vyao ili wapange mikakati yao, siku hizi hakuna ni kupasua tu ili anaejiona hana damu ayakaribie mauti.
 
Maoni tu kila mtu yupo huru kusema haijalishi..........
wewe ni mpuuzi sana, hujui kwa kauli hizo ndo zimechangia Mbowe na wenzake kuwa na kesi hadi sasa. Hukumbuki siku ya kuhitimisha kampeni zao jimbo la Kinondoni? Wewe ni mpuuzi sana, ulitakiwa usime RC hapo ameteleza, siyo kauli ya kutolewa na kiongozi/mkiti wa kamati ya ulinzi ya mkoa mbele ya vyombo vya hbr.

Kwa kauli hizo, serikali inaepuka vipi lawama za uvunjifu wa amani? Kuna umri ukifika unalazimika kujifunza kuwa na busara.
 
Huu ndio upuuzi wa kiwango cha phd.kuna shda gani km ikiwa chadema au ccm?kwnn ubaguzi?je huu uccm unatofouti gani na ukaburu wa enzi zile za p botha?
Kwao ccm ni Bora kuliko Tanzania na watanzania
 
Back
Top Bottom