Uchaguzi 2020 Mrisho Gambo: Kwa gharama yoyote lazima Jimbo la Arusha lirudi CCM

Uchaguzi 2020 Mrisho Gambo: Kwa gharama yoyote lazima Jimbo la Arusha lirudi CCM

Hivi kauli kama hiyo ya Gambo ingetolewa na Kiongozi wa upinzani, si angefungiliwa mashitaka na kuozea ya uchochezi na uhaini na kuozea jela??

Hivi hii nchi kwa ubaguzi unaoendelea Magufuli anaipeleka wapi, kwa mpinzani kuswekwa ndani kwa uchochezi na akiongea mwanaccm anahimizwa "dogo" wewe chapa kazi!
 
Sijui ni kwa nn hii nchi inaonekana inaendeshwa na maRC wa dar na arusha? Yaani kiongozi wa serikali anatoa kauli hiyo na hadi sasa Rais hajatengua uteuzi.

Mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa anatoa kauli hiyo lakini si m/kiti wa chama taifa wala katibu wake aliyejitokeza na kulaani au hata kufuta nafasi yake kama mjumbe wa kamati ya siasa.

Si vyombo vya dola wala waziri anayekemea, wote wanapima upepo maana unaweza kujifanya kimbele mbele kukemea na matokeo yake ww ndo ukafukuzwa kazi.

Kama TRA, waziri wa fedha vs RC wa dar. Kila mtu kichwa chini. Angalau zamani walikuwa wanawafukuza waandishi wa hbr kwenye vikao vyao ili wapange mikakati yao, siku hizi hakuna ni kupasua tu ili anaejiona hana damu ayakaribie mauti.
Nadhani ndo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya mkoa..!!!! Anahamasisha vurugu ifanyike..!!??
 
Imbombo ngaafu! Tunachotaka ni maendeleo na amani! Neno vurugu ndio nini sasa!?
 
Kuna muda / wakati huwa mnamuonea na kumsingizia sana Rais Dr. Magufuli kwa ' Upuuzi ' tu wa ' makusudi ' wa Watendaji wake wachache. Hebu mwacheni Dr. Magufuli aongoze nchi jamani! Mmezidi sasa kumtupia kila aina ya lawama. Tubadilike!
Hivi lakini jamani, lazima tufike mahali tupige mstari. Kauli kama hii imejaa uchochezi wa hali ya juu, Mkuu wa Mkoa anatangaza watu wafanye fujo? hivi angekuwa ni Mbowe au hata huyo Lema awaambie wafuasi wake wafanye hivyo kwa matawi ya CCM, mbona Polisi wangeshamshughulikia mapema sana? katika utawala wa sheria kweli, Bosi wa Gambo asingekubali "kula" matapishi kama haya. angemtumbua mara moja. lakini anapeta kwa sababu most likely, hayo ndiyo maneno JPM anasuburi yaongelewe. maana JPM mwenyewe aliwauliza majaji, hivi mumemtuma huyu Fatma Karume awasemee matatizo yenu? maana sijasikia kukanusha wala kutoa kauli. sasa sisi tunamuuliza JPM, je, ulimtuma Gambo aseme hayo maneno? maana hatuoni kuchukua hatua yoyote. Nakushangaa sasa wewe ambaye unajaribu kutetea huu mfumo wa kibaguzi na ukandamizaji wa hali ya juu kiasi hiki?
 
Ohoooo Gambo Anasema CCM wafanye vurugu ili Jimbo tu la Arusha lirudi CCM! Msisitizo, Wafanye hata Vurugu..... Hii kauli ingetolewa na Upinzani mmmmghh..

Leo May 27, 2018 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amefungua semina ya umoja wa wanawake wa wilaya ya Arusha mjini ( UWT) yenye lengo la kuwajengea uwezo ikiwa ni pamoja na kuelekezana namna ya kutimiza majukumu yao pamoja na mada za kuwajengea uwezo.

Gambo amesema jimbo la Arusha mjini haliwezi kugawanywa kama inavyozungumzwa na katika uchaguzi ujao kwa gharama yoyote jimbo hilo litakuwa la CCM

Huyu ni mchochezi aliyebobea na alitakiwa kwa sasa awe mahabusu kwa Uchochezi...!!
Kauli kama hii ni ya kihuni, kichochezi na ya kishenx. Watu kama Gambo hawatakiwa katika jamii ya Kitanzania.Ingawa kwa Utawala huu wa A5 viongozi wajingawajinga kama hawa ndo wanapendwa na Mkulu na kupandishwa vyeo kila kukicha...!!!
 
Hivi lakini jamani, lazima tufike mahali tupige mstari. Kauli kama hii imejaa uchochezi wa hali ya juu, Mkuu wa Mkoa anatangaza watu wafanye fujo? hivi angekuwa ni Mbowe au hata huyo Lema awaambie wafuasi wake wafanye hivyo kwa matawi ya CCM, mbona Polisi wangeshamshughulikia mapema sana? katika utawala wa sheria kweli, Bosi wa Gambo asingekubali "kula" matapishi kama haya. angemtumbua mara moja. lakini anapeta kwa sababu most likely, hayo ndiyo maneno JPM anasuburi yaongelewe. maana JPM mwenyewe aliwauliza majaji, hivi mumemtuma huyu Fatma Karume awasemee matatizo yenu? maana sijasikia kukanusha wala kutoa kauli. sasa sisi tunamuuliza JPM, je, ulimtuma Gambo aseme hayo maneno? maana hatuoni kuchukua hatua yoyote. Nakushangaa sasa wewe ambaye unajaribu kutetea huu mfumo wa kibaguzi na ukandamizaji wa hali ya juu kiasi hiki?

Tafadhali heshimu mawazo yangu kama ambavyo nami nayaheshimu yako. Ahsante.
 
Tafadhali heshimu mawazo yangu kama ambavyo nami nayaheshimu yako. Ahsante.
Nadhani hujanielewa. Nimeyaheshimu mawazo yako ndio maana nimechangia. katikati ya huo uchungu kuna hoja za msingi ambazo unahitaji kuzijibu. kimsingi ulichosema ni kwamba JPM asihusishwe na kauli za watendaji wake. Yaani unamtenga JPM na uwajibikaji wake kwa wateule wake. Hoja yangu ni kwamba hiyo haiwezi kumwepusha JPM na responsibility yake. Lazima awajibike na hao aliowateua.

Hoja ya pili ni kwamba kawatuma. Na ushahidi ni kwamba wateule wake wengi sana amewatumbua kwa sababu moja ama nyingine. Yuko makini sana na suala la amani. hataki hata kusikia upinzani wana kikao cha ndani, maana watafanya uchochezi na kuvuruga amani. Lakini hii kauli ya Gambo ni uvunjaji wa amani, siyo tena by implication, lakini moja kw amoja.

Sasa hizo hoja mbili badala ya kuzijibu, wewe unasema mimi sijakuheshimu. ila kama unataka kusema umeshindwa kujibu hoja, basi nimekuelewa
 
Hiyo kauli isipuuzwe na Chadema. Waifanyie kazi wakati wote katika maisha yao. Inawezekana kajiandaa kuua watu na pengine kuwafunga.
 
Hata ikibidi kuua watu haina shida gambo damu itamwagika maana ndio mnachokitaka.
 
Ohoooo Gambo Anasema CCM wafanye vurugu ili Jimbo tu la Arusha lirudi CCM! Msisitizo, Wafanye hata Vurugu..... Hii kauli ingetolewa na Upinzani mmmmghh..

Leo May 27, 2018 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amefungua semina ya umoja wa wanawake wa wilaya ya Arusha mjini ( UWT) yenye lengo la kuwajengea uwezo ikiwa ni pamoja na kuelekezana namna ya kutimiza majukumu yao pamoja na mada za kuwajengea uwezo.

Gambo amesema jimbo la Arusha mjini haliwezi kugawanywa kama inavyozungumzwa na katika uchaguzi ujao kwa gharama yoyote jimbo hilo litakuwa la CCM

Watu wakati mwingine ni lazima wawe makini na lugha wanazotumia,hasa unapokuwa kiongozi kwa kuwa wewe ni mfano wa kuigwa na wengine.Gambo anaposema kwa gharama yeyote,ana maana gani?Hata kwa damu?Lugha hizi zinaleta ukakasi sana.It seems most people do not know the story behind politics, wangejua wasingefikia hatua hizi na wakati mwingine hata kuuana.It's very inappropriate, laughable,ludicrous and absurd.
 
Back
Top Bottom