Uchaguzi 2020 Mrisho Gambo: Kwa gharama yoyote lazima Jimbo la Arusha lirudi CCM

Uchaguzi 2020 Mrisho Gambo: Kwa gharama yoyote lazima Jimbo la Arusha lirudi CCM

CHADEMA weka mwanasheria aimbe naye mahakamani. Mnatuaibisha kutochukulia hatua watu wote wanao lipuka hovyo kuwadhalilisha CHADEMA. Sweka mahakamani, kitendo cha kumfungulia mashitaka mtu (siyo cheo) itakuwa funzo kwa walopokaji wengine wakiwemo wanao lazimisha au kutoa vitisho kwa watendaji wengine kuchukua hatua za kisheria kwa wapinzani. Fungua mashitaka, wanasheria wa chama vipi???!! Ukimya wenu utawagharimu wananchi na wanachama wenu. Kukaa kimya maana yake mnakubaliana na maelekezo juu yenu wapinzani. Hivi mnajua hassle ya ruti za kesi mahakamani? Shitaki nao wapate mikiki ya kuhudhuria na kuhukumiwa. Huwezi kuwa kiongozi unaye hamasisha kutenda maovu wakati unatakiwa kusimamia sheria. Angekuwa kajamba nani au hata Lema mwenyewe katamka hivyo, angekuwa bado mtaani?????
 
Hivi neno uchochezi lipo tu kwa kauli za wapinzani?
Hili Taifa kweli linaongozwa na washamba
 
Sawa mwache afanye juu chini alikomboe jimbo kwenye media na majukwaani ila sisi tutalibakisha kwenye sanduku la kura.
 
JF kweli imevamiwa, watu wameshindwa kuelewa maana ya kufanya fujo kutoka kwa RC.. RC amewataka Wana CCM wanaotaka kugombea Ndiyo wafanye fujo (kuanza harakati za kugombea katika jimbo la Arusha)
 
Kama Wamerogwa"" ....Sasa Hizo si Kauli Za Uchochezi Hizo " Maana Hapo Itabidi Wananchi Ambao Wapo Vyama Pinzani Nao Waanze Kujiandaa" Kupambana na Hao walioagizwa Kufanya Fujo...
.
na chuga walivyo walipopewa bodaboda bado walionesha alama za v hihihi
 
Ohoooo Gambo Anasema CCM wafanye vurugu ili Jimbo tu la Arusha lirudi CCM! Msisitizo, Wafanye hata Vurugu..... Hii kauli ingetolewa na Upinzani mmmmghh..

Leo May 27, 2018 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amefungua semina ya umoja wa wanawake wa wilaya ya Arusha mjini ( UWT) yenye lengo la kuwajengea uwezo ikiwa ni pamoja na kuelekezana namna ya kutimiza majukumu yao pamoja na mada za kuwajengea uwezo.

Gambo amesema jimbo la Arusha mjini haliwezi kugawanywa kama inavyozungumzwa na katika uchaguzi ujao kwa gharama yoyote jimbo hilo litakuwa la CCM



Aseme "kwa goli la mkono" asubirie matokeo yake
 
hawa watu wanao onekana vijana wa sisiemu ni watu wa aina gani??????? tukianza na katibu mwenezi alithibitisha lema hawezi rudi bungeni 2020..leo hii huyu anatuambia mambo ya fujo..ipo siku hili wanalo lipanda watalijutia..tulizoea kuhubiriwa amani ila leo mkuu wa mkoa anatuhubiria vita..sijui atawaficha wapi wajukuu zake za vilembwe siku bomu hili wanalo litega litakapo lipuka..

bado kitambo kidogo


Tarehe kama ya Leo mwezi uliopita
 
Hivi machalii wa Arusha walikufa wote nini alifu?!
 
Kuna muda / wakati huwa mnamuonea na kumsingizia sana Rais Dr. Magufuli kwa ' Upuuzi ' tu wa ' makusudi ' wa Watendaji wake wachache. Hebu mwacheni Dr. Magufuli aongoze nchi jamani! Mmezidi sasa kumtupia kila aina ya lawama. Tubadilike!
Tatizo lake hao watendaji wake wakiongea kauli kama hizo hawakemei wala kuwaonya sasa kwann tusimlaumu!
 
Kuna muda / wakati huwa mnamuonea na kumsingizia sana Rais Dr. Magufuli kwa ' Upuuzi ' tu wa ' makusudi ' wa Watendaji wake wachache. Hebu mwacheni Dr. Magufuli aongoze nchi jamani! Mmezidi sasa kumtupia kila aina ya lawama. Tubadilike!
Analaumiwa kwa kuwa yeye ndiye anayeteua na kutengua

Kwa matamshi ya hatari kama hayo aliyotamka Gambo, Magufuli alipaswa amtumbue mara moja

Kwa kukaa kwake kimya maana yake amebariki upuuzi huo na anauunga mkono!
 
Hakika nimeziunga Juhudi Za Rais Wangu Magufuli katika kuiletea Tanzania Maendeleo
hivi Wabunge na Madiwani wa Vyama vilivyo tafauti na cha Raisi bado WANAJIUZULU Nyadhifa zao "kuunga nkono" juhudi za Raisi kuwaletea maendeleo?
 
Kwahiyo Nikikutukania Mama Yako Hapa "" Nitakuwa " Sijafanya Kosa " Maana Nitakuwa Nimetimiza Uhuru Wangu Wakutoa Maoni ""
Una mapya umeyafungua kwenye nailoni au ni hayo ya kawaida we tukana!
 
Back
Top Bottom