Mrisho Gambo: Sisi mpinzani wetu siyo vyama vya siasa ni changamoto za Watanzania

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,419
“Sisi Mpinzani wetu sio Vyama vya Siasa, Mpinzani wetu ni changamoto za Watanzania leo ukizungumza Watumiwhi wana manung’uniko kuhusu mishahara yao, wana manung’uniko kuhusu kupanda madaraja kwa miaka mitano hawajapanda madaraja, leo ukizungumza kuhusu bodi ya mikopo unaona sheria ilikuwa inasema asilimia 8 baadae imekwenda asilimia 15 lakini hayo mambo yamepitishwa ndani ya Bunge hili" Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini.

"Lakini ukiangalia tuna changamoto kwenye bima ya afya, tuna changamoto kwenye ajira, manung’uniko ni makubwa. Kazi ya Bunge hili ni kurekebisha sheria, kutoa mapendekezo na ushauri ambao Serikali ikifanyia kazi matumaini yataendelea kudumu kule kwa Watanzania" Mrisho Gambo.

Your browser is not able to display this video.
 
Kwa kweli hapo Mrisho Gambo umenena. Shughulikieni changamoto za wananchi. Hiyo Minyukano ya Kundi la Mwendazake na la Samia haitusaidii. CCM haina mwelekeo wa kuisaidia nchi. Angalia sasa hicho chama hakina mwenyekiti, katibu wala katibu mwenezi. Ni chama kinachoningínia mahali fulani hewani tu.
 
Naona ule mgando kichwani umeanza kuyeyuka wanaanza kupata akili sa hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…