Mrisho Gambo: Sisi mpinzani wetu siyo vyama vya siasa ni changamoto za Watanzania

Wasalaam,niende kwenye hoja,wakati mbunge wa Arusha mjini,Mrisho Gambo akichangia kuhusu bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu, jana bungeni.Kwa wenye clip wanisaidie kuiweka kuanzia dk ya 2:30 utagundua aliongea vitu vya msingi sana,hakukuwa na makofi zaidi ya mara moja moja makofi yaliyopigwana na jirani yake Mh. Kingu.Anasema wapinzani wao sio vyama vya siasa bali changamoto za wananchi(sijui legitimacy ya kauli hii),anabainisha kwa miaka mitano Watumishi wamekuwa na malalamiko ya kutoongezewa mishahara wala kupandishwa madaraja na malalamiko ya ajira.Ametaja pia mkanganyo mkubwa wa sheria nne kwenye Uhamiaji,kazi,Uwekezaji na Kodi,na jisnsi ilivyongumu kufanya biashara Tanzania.Anaenda mbali zaidi kwa kuongea Ongezeko la makato ya mkopo kutoka Asilimia 8 mpaka 15,Anabainisha Sheria hizi zote zimepitishwa na bunge hili.
"Wabunge wote kimyaaaa",lipi lengo la Mh.Gambo kwa hotuba hii?Kuna cha kujifunza na kuzingatia pia kwa alichokisema bila kuangalia uhalali wa aliyekisema.
 
Kaongea kama mtu aliyewahi kuwa kiongozi lakini alishindwa jinsi ya kuwatetea wananchi.
 
Huyu mpuuzi na mnafiki mkubwa. Yeye wakati wa Ukuu wake wa Mkoa ameshiriki kuwaangamiza Wawekezaji kwenye sekta ya Utalii A town. Leo eti nae anajidai kitoa ushauri! Asubiri 2025 apepete tena mchele.
 
Jamaa katema madini sana.

Hawa ndo aina ya watu tunaowahitaji, watu wa uobgea masuala ya wananchi kwa upeo mkubwa
 
Ni kujikweza kwa boss
Huyu mpuuzi na mnafiki mkubwa. Yeye wakati wa Ukuu wake wa Mkoa ameshiriki kuwaangamiza Wawekezaji kwenye sekta ya Utalii A town. Leo eti nae anajidai kitoa ushauri! Asubiri 2025 apepete tena mchele.
 
Wabunge wengi wanapenda vitu vya umbea na kuzodoana sana
 
Wapinzani hawakwepeki mkuu Ccm mna Changamoto mbili usijidanganye Wapinzani na Wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…