britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 16,295
- 33,994
Ameyasema Bungeni kwamba Serikali ilikurupuka kuwafuta Kazi
========
MRISHO GAMBO: Wafanyakazi 14,409 ambao ni sawa na asilimia 2.82 walibainika kuwa na vyeti feki. Mheshimiwa naibu spika hoja yangu ambayo nataka niijenge hapa, pamoja na kuunga mkono zoezi la serikali kuwatambua watumishi wenye vyeti feki na kuchukua hatua stahiki lakini lazma hawa watumishi walifanya kazi ya kuitumikia nchi hii.
Hata masuala tunayojivunia leo wao pia ni sehemu ya kazi ambayo tumeifanya. Ni vizuri sasa wafanyakazi hawa tukaangalia utaratibu wa kuwapatia haki zao kwasababu wakati wanafanya kazi waliweza kukatwa fedha ambazo zikaenda NSSF, leo zile fedha zimekwenda kule, zinamnufaisha nani?
Wengine walipitisha muda kisheria, miaka 15, 20.. walistahili pia kulipwa kiinua mgongo, pamoja na serikali kuwaondoa kazini, nilikuwa naomba serikali hii ya awamu ya sita ikaangalie jambo hili kwa jicho la huruma, ikawaangalie wananchi hawa 14,409 ambao wana familia zinawategemea wakaweze kupata kiinua chao mgongo, wakapate na mafao yao na baada ya hapo tuendelee kuchukua watumishi wenye sifa maana sisi kama serikali tulichangia kuingia kwa watumishi hao maana waliingia kwa utaratibu"