Mrisho Gambo: Vyeti Feki walipwe, Serikali ilikurupuka!

Ila Watanzania tumekuwa wanafiki hadi tunajidhalilisha mbele ya wengine, huyu Gambo si ndio alikuwa kwenye serikali hii anayoinange haya mbona hakuyasema? kwa mtu mkweli kama kuna kitu haafiki alitakiwa ajiondoe kwenye serikali na si kuja hapa kujilambalamba midomo, hawa vijana wanapima upepo na kumjaribu mama naona sasa kila mtu anatoka tunduni kisa mama katoa ruksa,hawajui wanaji kaanga wenyewe, waache kumjaribu mama, naamini angekuwa hai mwendazake hakuna ambaye angeleta ujinga wa kusema pumba bungeni. Mama kaa standby vijana wanakupima upepo.
 
Hii nchi ya ajabu sana vyeti feki wanaungwa mkono! Wanauhalali na wameonewa kutolewa na walipwe mimi naona tuulize hata sheria nchi majirani zetu wenyewe huwa wanafanyaje juu ya hili
Tena wangeshitakiwa kuhujumu uchumi.

Vijana wanakosa ajira ambao wana vigezo
 
Hapa mkuu

Forgery ya vyeti is a crime at least wangekua wawazi

Tunajua cost ya kuhudumiwa na fake certificate person?

Watanzania msikubali magumashi

Vyeti feki ni ufisadi pia

Mbona mlifumbia mamcho kwa Makonda,Kigwangala,Mwigulu,palamagamba na Jiwe? Hao wote ni mafisadi wa elimu kama Msemakweli kinerugaba alivyowaita....Zoezi zima lilikuwa biased lilipagua watu hivyo alikuwa zoezi la haki bali chuki za jiwe kupunguza wafanyakazi.
 
Meko alichofanya ni redundancy ya kihuni na kidhulumati ili apunguze wage bill apate pesa ya kutosha kutekeleza mamiradi yake ambayo yalikuwa yanampa ulaji binafsi na wapambe zake....There is no way out hawa watu lazima walipwe kwa sababu serikali ndo iliwaajiri na hadi wanathibitishwa kazini walikuwa wamejiridhisha na vigezo na uwezo wao wa kufanya kazi.....
 
Hilo zoezi alijaendeshwa kihaki ,kama Makonda,mwigulu,palamagamba,kigwangala na jiwe wangeondolewa hapo ningeona zoezi liliendeshwa kiha ila wamepunguza tu wafanyakazi kwa vigezo vya kubumba ,basi walipwe mafao yao.
 
HIvi awamu ya sita inayolazimishwa na wanasiasa akiwemo mheshimiwa Rais ni Mkakati wa CCM kuelekea uchaguzi wa 2025 kuwa wameisha pita bila kupingwa au ni kutokuwa na elimu ya uraia?.

Kikatiba awamu ya tano inaisha mwezi October 2025 na itafuatiwa na kampeni za urais na ubunge kwa awamu ya sita,.. kilichobadilika ni kufariki kwa Rais wa awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli akiwa madarakani na kurithiwa na Makamo wake katika kipindi cha pili cha awamu ya tano.

Inashangaza kusikia mwanasiasa kama Gambo aliyekuwa kiongozi kwenye kipindi cha kwanza cha awamu ya tano na wengine wa aina yake akikitambua kipindi cha pili cha awamu ya tano kama awamu ya sita.

Inawezekana ikawa ni ghiriba za wanasiasa tu, lakini inawezekana pia kwamba kuna wanasiasa wengi tu vilaza waliojazana kwenye uwanja wa siasa,na kwa bahati mbaya ndio hawa wanaofanya maamuzi wa mustakabali wa taifa hili....Aibu!.
 
Acha nae atoke vipi ....acha ajenge hoja ijadiliwe kwa mapana yake
 
Hatukufumbia macho

Tena wewe mkongwe humu, tulisema Sana chifu

Labda kama.umesahau
 
Hilo zoezi alijaendeshwa kihaki ,kama Makonda,mwigulu,palamagamba,kigwangala na jiwe wangeondolewa hapo ningeona zoezi liliendeshwa kiha ila wamepunguza tu wafanyakazi kwa vigezo vya kubumba ,basi walipwe mafao yao.
Hivi ukibanwa ukaambiwa utoe ushahidi concrete kwamba hao unaowataja wamefoji vyeti unaweza kweli.Acheni kushabikia story za vijiweni ninyi.Kama umebambwa na cheti feki beba msalaba wako mkuu,tafuta ulaji mahali pengine,serikalini kume-chacha.
 
Tena wangeshitakiwa kuhujumu uchumi.

Vijana wanakosa ajira ambao wana vigezo
Halafu hawa watu hawana huruma aisee.Jambo la kushangaza ni kwamba wanamuona Magufuli aliyewaondoa kwamba ndiye mwenye roho mbaya!Na wao waliochukua ajira za watu wanaostahili huku wao wakiwa hawastahili tuwaiteje?I think they are super idiots.
 
Hatukufumbia macho

Tena wewe mkongwe humu, tulisema Sana chifu

Labda kama.umesahau

Chifu kama zoezi lingeanda haki bin haki wangebaki wachache sana serikalini,hauwezi kuondoa vyeti feki halafu kada nyingine ukaacha,zoezi lile lilikuwa na lengo la kupunguza wafanyakazi tu....Kama vyeti feki basi ingekula kuanzia police,jwtz,tiss,magereza,jkt lakini hao hawajaguswa ,kwanini hawakuwagusa? Hapo ndipo naposema lile zoezi halikuwa la haki.
 
Hivi ukibanwa ukaambiwa utoe ushahidi concrete kwamba hao unaowataja wamefoji vyeti unaweza kweli.Acheni kushabikia story za vijiweni ninyi.Kama umebambwa na cheti feki beba msalaba wako mkuu,tafuta ulaji mahali pengine,serikalini kume-chacha.

Yaani wewe kweli Empty Set ,yaani haujui kwamba Makonda ni Daudi Albert Bashite? Said Nassor Bagaile ni Hamis Kigwangala? Lameck Madelu ni Mwigulu Nchemba? Hao wote wamefoji elimu wanavyeti feki ,Palamaganda hadi kwenye list alikuwepo unataka ushahidi gani? Jiwe alikuwa na Phd Feki Ushahidi uliwekwa dhahiri na Ben Saanane ,baada ya kuweka unajua kilichompana Ben ClockEight.
 
Aiseeee ibilisi Jiwe kaumiza Sana familia za wahanga , walipwe aisee wanamchango mkubwa sana kwenye nchi hii kuliko hata Jiwe , Jiwe yeye mchango wake Ni kulitia hasara tu taifa Tena kwa matilioni .
 
Hatuhitaji empty words,kama una ushahidi concrete peleke sehemu husika.Maneno ya vijiweni hayatusaidii sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…