Ni Kauli ya Msanii lakini imebeba ujumbe mzito sana
Yawezekana hao 5% waliopelea kwa mujibu wa takwimu za Mpoto ni wale Chadema na akina Mwabukusi
Sijajua Dr Mrisho Mpoto alitaka kumaanisha nini hasa lakini Ujumbe wake kwa tafsiri yoyote ile ni mzito
Mungu wa Mbinguni awabariki 😀
MAONI YA WAKILI BONIFACE MWABUKUSI
Maoni na hoja zangu za Awali kuhusu kusainiwa kwa mikataba mitatu ya uwekezaji wa Bandari. Na Boniface Mwabukusi
1.Mikataba hiyo imefichwa na haijawekwa wazi kwa wananchi wala kuwasilishwa Bungeni kama sheria inavyotaka.kwa hiyo ni muendelezo wa vurugu na ukiukwaji wa sheria.
2.Mikataba hii(HGA) haina nguvu dhidi ya IGA mkataba mama ambapo licha ya mikataba hii (HGA) kusema kuwa itatumia sheria za Tanzania haielezi iwapo sasa zitatumika mahakama na mabaraza ya ndani ya Tanzania katika utatuzi wa migogoro.
3.Rais anasema mkataba huu ni matokeo ya IGA ,Mwingine anasema mikataba hii ni matokeo ya Public Private Partnership.Kama mikataba hii ni matokeo ya PPA kwanini mulipeleka Azimio na Mkataba wa IGA kuridhiwa na Bunge? Kama ni PPA kwanini muweke exclusive clause? Kwanini mgeni amiliki asilimia 40? Je sheria Na.5 na No 6 za mwaka 2017 zinasemaje kuhusu umiliki wa Raslimali za Asili ?
4.Wametuambia kwamba eti tutamiliki kwa ubia wa asilimia 60 kwa Serikali na Asilimia 40 kwa DPW...Hiyo Asilimia 60 ni yaserikali ipi ya Muungano au Tanganyika?
5. Je Zanzibar itapata mgawo kwenye mapato ya bandari ya Tanganyika? Je katika hiyo asilimia 60 kuna viongozi wa Zanzibar wataingizwa kwenye usimamizi wa Bandari za Tanganyika ambazo siyo za muungano?
6. Je hawa wenzetu wametuambia na kutufafanulia ili kupata hiyo asilimia 40 DPW kawekeza kiasi gani na katika maeneo yepi? Kwanini hamjaweka feasibility study wazi kwa Umma ili umma ujue badala yake mkafanya siri na kuitana kwa faragha kana kwamba nchi hii ni shamba lenu binafsi?
7.Je kama HGA ni ya miaka 30 Inter Governmental Agreement (IGA) ni ya miaka mingapi?
Muhimu kujua:
1 .Mbuzi hawezi kuzaa Tembo.IGA ni haramu inapoka Mali asili za watanganyika na kuziweka kwenye mikono ya watu wa chache kwa njia ya ujanja ujanja.
2.Hitaji letu ni IGA ifutwe na kama kuna uwekezaji unafanyika lazima uzingatie maslahi ya Umma na siyo ya viongozi wa ccm na familia zao kwa kuhakikisha
@ Bandari za Tanganyika zinamilikiwa na Umma kama sheria zinavyotaka
@. Kama ni uwekezaji lazima uwe wa mfumo unaotoa nafasi na fursa kwa watanganyika na kampuni za kitanzania kumiliki sehemu kupitia hisa badala ya Kampuni moja ya kigeni kupewa asilimia 40?
WEKENI HUO MKATABA WA HGA WAZI ILI TUUONE NI MATAKWA YA KISHERIA.
BAK MWABUKUSI
SHAMBANI BUSOKELO.