Mrisho Mpoto alaumiwa kwa kumkejeli Padri Kitima Ikulu


Yupi mpumbavu? Je, aliyetoa hotuba kwamba maoni ya wananchi (wakiwemo akina Fr. Kitima) yamezingatiwa kufikia hayo makubaliano yaliyotiwa sahihi siku hiyo au yeye aliyeenda na mipasho ya kula pilau?

Wakati mwingine huyu mwezetu ni mtu wa kusamehe maana elimu aliyonayo na ukubwa wa jina lake ni vitu viwili tofauti, na kitokacho mdomoni ni reflection ya uwezo wa ubongo wa mtu kuchakata mambo.
 
Wewe ni mvaa kobazi na chuki zako tu
 
Hujui kitu.
Bora ufiche ujinga wako. Ili ujue wale ni wabaguzi na kujiona ni daraja la kwanza,subiri itokee atawale raisi mkiristo lakini awe mlutheri(ngumu kutokea) utajiunga na sisi tunaowekwa daraja la pili.
Acha Udini kwenye mambo ya kitaifa
Mwisho wa uislamu wako ni msikitini mnapokuwa waislamu kwa pamoja.

Nje na msikitini unakutana na jamii zenye imani tofauti.
Jifunze kuishi nazo!
Akiongea muislamu usijadili kwa kuwa muislam kaongea.
Pia akiongea mpagani au mkristo usijadili kwa kuwa mpagani au mkristo kaongea.
Jifunze kujadili hoja.
 
Anaadika Malisa GJ

Nimesikitika kuona Mrisho Mpoto akimdhihaki Dr.Kitima, kwenye hafla ya utiaji saini mikataba midogo ya uendeshaji wa bandari (HGAs) kati ya serikali na DP World.

Mpoto akimlenga Dr.Kitima alikejeli kwa kusema "mama wengine walipinga lakini leo tutakula nao pilau. Wengine wameacha kuchunga kondoo wamegeukia siasa, lakini kwa kuwa wewe ni mama wa upendo umewaita wote"

1. Kwanza Kitima hakujua kama anaalikwa kwenye hafla ya serikali na DP World. Kadi ya mwaliko aliyopewa inasema ni hafla maalum. Sasa angepiga ramli kujua inahusu DP World?

2. Kitima ana mchango mkubwa kwa taifa hili. Ni Mbobezi wa Constitutional Law na ameshiriki kuandika miswada mingi ya Katiba nje na ndani ya nchi.

Ni mwanazuoni mahiri, mwenye Bachelor degree mbili, Masters mbili na PhD moja. Ni Vice Chancelor mstaafu wa chuo kikuu binafsi kikubwa zaidi nchini (SAUT), na Katibu Mkuu wa TEC. Sasa mtu kama huyu Uzalendo wake utapimwa na Mrisho Mpoto kweli?

Kitima form six alipata div.1 ya point 3 yani A zote. Mpoto alipata ngapi? Ooh sorry sidhani kama for six amefika. Form four ana D ngapi? [emoji1787]

3. Mwambieni Mpoto waliopinga mkataba wa bandari ni wazalendo kuliko waliounga mkono. Ndio maana serikali imefanya marekebisho kwenye HGAs. Kama vile;

- Ukomo wa mkataba umekua miaka 30 tofauti na IGA ambayo haikua na ukomo.

-DPW imepewa magati manne tu (no.4 hadi no.7) tofauti na awali ambapo ilipewa magati yote.

- Gati no.0 hadi no.3 yataendeshwa na TPA kwa kushirikiana na DPW. Na gati no.8 hadi no.11 yatatafutiwa mwekezaji mwingine.

- DPW itaendesha bandari ya Dar tu na sio bandari zote kama IGA ilivyoeleza.

- TRA itakusanya mapato tofauti na hapo awali ambapo mapato yangekusanywa na Dubai.

- CAG atakagua hesabu tofauti na awali ambapo alikua haruhusiwi.

- Serikali itachukua 60% ya mapato ghafi na DPW 40% tofauti na awali ambapo ilikua siri.

- DPW itawekeza $250M kama amana ya kwanza kwa miaka mitano, tofauti na awali ambapo ilikua siri.

Marekebisho haya yasingefanyika kama wote tungekua makasuku wa kukubali kila kitu. Waraka wa TEC na sauti za wote waliopinga ndio zimefanya serikali ifyate mkia na kufanya marekebisho haya. Makasuku kindly be informed.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitima alikwama wapi??? Kadi ya mwaliko isoelezea Tukio gan linaenda fanyika??.

Kumbe ndo maana walimuingiza Cha kike.

Anyway, Bado hakijaribika kitu
Hivi wananchi walitangaziwa kuwa kutakuwepo na tukio (hafla) fulani?
Kama HAPANA... na kwa uthibitisho wa uandishi wa kadi ya mwaliko NASEMA DPW ni mchongo haramu!
Muda utasema!!
 
Lile li-mpoto lina akili za kuelewa kilichoandikwa humu??
 
Huyo Dr. Kitima ni mmoja... Je, wananchi walijua kuwa kuna moja na mbili Ikulu??
Je, baada ya zile kelele za Bandari/DPW wananchi walipewa mrejesho??
 
Njaa ni mbaya sana unatumika na wenye hela kuwasemea yamoyoni halafu wewe uliyesema ndio unaonekana kituko cha haja! Na bado pumba zitajitenga na Mchele!.
Watu wanaota vipara unaweza kusema wanahekima kumbe bado ni wapuuzi wanaotakiwa kukanywa na mama zao!.
Mpoto kaidharirisha nchi,ikulu na yeye mwenyewe ifike hatua ikulu ihalike watu wenye Hali ya utafakari na sio uchawa wakutoa Kila neno!
 
Hamjui ya kwamba wasanii wa bongo ni waganga njaa...
 
Hujui kitu.
Bora ufiche ujinga wako. Ili ujue wale ni wabaguzi na kujiona ni daraja la kwanza,subiri itokee atawale raisi mkiristo lakini awe mlutheri(ngumu kutokea) utajiunga na sisi tunaowekwa daraja la pili.
wakatoliki nawajua vizuri in and out katika siasa za kwetu na siasa za dunia hii najua nguvu zao kiroho na kisiasa. Ni kweli hata kwa rais mlutheri au dhehebu lolote lisilo la kikatoliki watamsigina tu kwa nyaraka zao wakiamua usidhani ni kwa rais muislam tu. Ni hulka yao na wakabiliwe kwa hoja hizo hizo wanazozijenga kuliko kusema eti kwa kuwa rais ni muislam wakati mnajua ni kila rais asiyekuwa mkatoliki watamlima waraka tu.
 
Sehemu ukivunjiwa heshima unatakiwa kusimama na kuondoka muda huohuo haijalishi alie mbele yako ni nani
Angefanya hvyo ningemuona wa maaana Sana bal alibaki na zito kumsikiliza huyu ndumilakuwili
 
Kitima alikwama wapi??? Kadi ya mwaliko isoelezea Tukio gan linaenda fanyika??.

Kumbe ndo maana walimuingiza Cha kike.

Anyway, Bado hakijaribika kitu
Alfu ajabu ni Kwamba taarifa za kutiliana saini imefanyika kwa Siri sna nilishanga kuona leo ndio tukio lenyewe Tena asbh saa nne nne hv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…