Msaada anataka kunyang'anywa nyumba yake na kuuzwa kutokana na deni la sh 96,000

Msaada anataka kunyang'anywa nyumba yake na kuuzwa kutokana na deni la sh 96,000

Mkuu, nimemkuta huyo dada katika hali ya huzuni na akiwaza kujiua kutokana na hayo yote kama nilivyoyaeleza hapo juu, sijajua alivyokopa alipewa masharti gani wala dhamana, mimi nilileta kwenu ili kutafuta namna ya kumsaidia kisheria ili apate haki yake
wajibu kwanza haki baadaye...
wajibu kulipa deni
 
Deni la 96 iwe dhamana nyumba. Mkuu hivi huyo mwanamke yupo TIMAMU KWELI au unataka kutuseti?? Ila ninamkumbuka sana yule dogo wa kuomba elfu 30 sijui alipata kibarua pale kwa bakhresa buguruni🙏
Mkuu ukihitaji namba yake naweza kukudm akueleze yote
 
Inabidi tujue mkataba wao ulisemaje.

Kiasi ni shilingi ngapi kwa riba ya asilimia ngapi.

Kama mkopeshaji ana leseni ya BOT.

Inabidi tujue mkataba wao ulisemaje.

Kiasi ni shilingi ngapi kwa riba ya asilimia ngapi.

Kama mkopeshaji ana leseni ya BOT.
Nilitaka kukudm namba zake ili uwasiliane naye umuulize yote hayo nikakuta umefunga dm
 
Nilitaka kukudm namba zake ili uwasiliane naye umuulize yote hayo nikakuta umefunga dm
Weka tu hapa. Mbona siyo siri hayo mambo.

Ila naona ogically haiwezekani mkopo wa 96,000 dhamana ikawa nyumba.

Tufanye kweli dhamana ni nyumba. Je hii nyumba itachukuliwa kama vitisho vyao vinavyodai?

Itachukuliwa ila kwa utaratibu, ambapo inabidi kesi ifike mahakamani na mdaiwa kuonekana hawezi lipa hicho kiasi na hana mali nyingine ya kuweza kulipa 96,000 basi nyumba itauzwa kwa amri ya mahakama.

Hata hivyo kama nyumba ni ya wanandoa na mwanandoa mmoja hajui kuhusu mkopo au hakuridhia mwanandoa anaweza weka pingamizi na nyumba haitauzwa.
 
Back
Top Bottom