mwaya mdogo wangu mzuri
Joanah,
Cooking is an art, ndiyo maana chakula hicho hicho kimoja watu wana mapishi mengi na tofauti balaa, hivyo lolote lile lisiku disappoint, hata kwa wanaojua kuna siku vyakula vinagoma kabisa..!!
Imagine, Jana kuna group moja wadada walikuwa wanasema huwa wanaanza kupika wali na maji baridi, yaani wanatia maji na mchele kwa pamoja na vinaiva vyema na kwa pamoja, tukabaki tunashangaa..!!
kupika ni baby steps, unajaribu -unakosea, kesho unatazama ni wapi ulikosea unarekebisha tena, ili usipate tabu, pika chakula kidogo ili pia isiwe hasara incase ukatoa muujiza..!!
Leo umekosea sababu umezidisha mafuta, jaribu kesho, punguza mafuta, punguza chumvi, na siku zote jitahidi pale mchele unapoishia kwenye sufuria maji yasipite sana, na wali wako ukichemka tu vizuri, punguza moto mpaka mwisho kabisa, yaani mpaka natamani nikupigie simu nikuelezee kwa sauti..!!
you're such a smart lady, kitu kama kupika hakiwezi kukushinda akili mdogo wangu, cha kuzingatia ni usichoke kujaribu wala usikate tamaa hata ukiharibu mara kadhaa..!!