Msaada/confession: Sijui kupika wakuu

Msaada/confession: Sijui kupika wakuu

Unahitaji upwige bolo la mikono 🤔umri huo hujui kupika
 
Mkuu chakula sio wali Pelee


Kuna


Maboga
Viazi
Mihogo ya kuchemsha
Mayai

N.k

Bila kusahau kukata kata matunda..mume hawez kukuachia kisa wali

Napenda wali 😁
 
mwaya mdogo wangu mzuri Joanah,
Cooking is an art, ndiyo maana chakula hicho hicho kimoja watu wana mapishi mengi na tofauti balaa, hivyo lolote lile lisiku disappoint, hata kwa wanaojua kuna siku vyakula vinagoma kabisa..!!

Imagine, Jana kuna group moja wadada walikuwa wanasema huwa wanaanza kupika wali na maji baridi, yaani wanatia maji na mchele kwa pamoja na vinaiva vyema na kwa pamoja, tukabaki tunashangaa..!!

kupika ni baby steps, unajaribu -unakosea, kesho unatazama ni wapi ulikosea unarekebisha tena, ili usipate tabu, pika chakula kidogo ili pia isiwe hasara incase ukatoa muujiza..!!

Leo umekosea sababu umezidisha mafuta, jaribu kesho, punguza mafuta, punguza chumvi, na siku zote jitahidi pale mchele unapoishia kwenye sufuria maji yasipite sana, na wali wako ukichemka tu vizuri, punguza moto mpaka mwisho kabisa, yaani mpaka natamani nikupigie simu nikuelezee kwa sauti..!!

you're such a smart lady, kitu kama kupika hakiwezi kukushinda akili mdogo wangu, cha kuzingatia ni usichoke kujaribu wala usikate tamaa hata ukiharibu mara kadhaa..!!

Mbona mie wali naupika kwa mfumo huo uliowashangaza wa maji ya baridi 😀

Nitajitahidi kupika mara nyingi nikiweza, asante sis 🙏
 
Sema inawezekana ulijifunzia youtube. Kuna kipindi nilikuwa refa mzuri tu (mechi za mtaani) nilijifunzia youtube, tangu nimeacha sikumbuki hata katika zile sheria kumi na saba za soka sheria ya kwanza ni ipi.

😂😂😂 mmmh
 
Pole sana, unaweza usijue kupika vizuri ila ukawa mzuri kwenye kutwanga na kupepeta...


Cc: Mahondaw
 
I wish T.I.D apitie hii thread!! Kwani una undugu na Abigail chams??
 
Nimekuja mwaya International Chef wangu, naomba umshushie yale madini yako tafadhali sana..!!

Na umeanza lini uchoyo wa kutonialika iftari..??
Yaani stay tune madikodiko yanaanza soon hapa nishashop Nazi zangu za buku buku🤣🤣🤣
 
Wakuu,

Nilishawahi kuleta uzi wa kutojua kupika way back Mwanamke kutojua kupika inaweza kuwa sababu ya kupewa talaka?
Jioni hii nimepika wali...nauangalia hapa naona aibu mimi...wali una mafuta huoo

Nilianza kujua kupika lakini sjui nimesahau ama ni vipi lakini kila nikipika naharibu 🙌

Nisaidieni tips za kujua kupika vizuri...

Aaliyyah
Mwachiluwi
Sis Carleen

Bro Evelyn Salt nisaidie braza
Joanah mbona kupika sio kitu chenye ugumu hivyo!
Labda mtindo wa makuzi yako ulikuweka mbali na mapishi lakini ni kitu rahisi sana .
Kama umepika wali umeona kuna makosa fulani kesho pika tena ukirekebisha pale ulipo kosea leo na kurudia hivyo hivyo jadi ujenge mazoea.
Hamia chakula kingine , mwisho wa siku utajikuta mpishi mzuri kuliko wengi walio na taaluma hio.
 
Nilikuwa kama ww nikatafuta mwanaume ambae hajui mapishi aise nasifiwa najua lakini mama akila anasema unajitahidi ila bado mwanaume kama mwachiluwi hapana aisee ataniumbua
Aisee kumbe kutafuta Mwenza kuna Mambo/vigezo vingi namna hii....
 
Wakuu,

Nilishawahi kuleta uzi wa kutojua kupika way back Mwanamke kutojua kupika inaweza kuwa sababu ya kupewa talaka?
Jioni hii nimepika wali...nauangalia hapa naona aibu mimi...wali una mafuta huoo

Nilianza kujua kupika lakini sjui nimesahau ama ni vipi lakini kila nikipika naharibu 🙌

Nisaidieni tips za kujua kupika vizuri...

Aaliyyah
Mwachiluwi
Sis Carleen

Bro Evelyn Salt nisaidie braza
Ohoo.pole sana.hilo ni tatizo la kuto lichukulia mzaha.nenda veta jifanye unataka kujifunza mapishi contemporary kumbe unataka basics
 
Back
Top Bottom