Msaada: Familia imedhulumiwa mafao ya marehemu baba yetu.

Msaada: Familia imedhulumiwa mafao ya marehemu baba yetu.

Sela Son

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,992
Reaction score
8,910
Wasalam wanaJF

Bila shaka mu wazima wa afya kama mimi hapa. Leo bwana nimekuja na jambo linalotesa moyo wangu kwa muda mrefu sana.

Familia yetu imedhulumiwa mafao ya marehemu baba yetu. Mzee wangu alifariki mwaka wa 2015 akiwa amebakiza miaka takribani miwili kustaafu. Mimi enzi hizo nilikuwa mdogo but ndugu zangu wawili wa kiume walikuwa tayari na 18 years+ .

Baada ya baba kufariki kuna bwana mmoja alijitolea kama msimamizi wa mirathi ambae alikuwa ni mtoto wa shangazi yetu mdogo. Yule bwana alishiriki kuhakikisha anaipata hadhi hiyo kwa kutumia nyaraka mbalimbali alizoacha baba, ikiwemo pia kututembeza mimi, mama na ndugu mahakamani ili kupata ridhaa hiyo.

Kwa kweli enzi hizo nilikuwa sielewi chochote nikiwa darasa la Saba. Kumbe alifanikiwa bwana kutimiza vigezo hivyo, hivyo basi pengine bila shaka alichukua mgao wetu na kuanza kutumia kwa maslahi yake. Kwani baada ya hapo akatoka kuwa maskini na kuwa mtu anayejiweza kwelikweli kiuchumi.

Sasa nimekuwa mtu mzima nimeshagundua kumbe kuna uwezekano kwamba alichukua fedha hizo na hakutukumbuka tena. Mama na ndugu zangu nikiwauliza hili wananikaripia kwa kuniambia niachane na jambo hilo tulishadhilumiwa na tukubali.

Kwa sasa Sina A wala Be hata chuo sikwenda sikuwa ada njaa kali. WanaJF naombeni mnisaidie kujua kwamba angalau nitembelee ofisi gani ambayo itanipa taarifa hizo kwamba je mtoto wa shangazi alifanikiwa kuchukua mgao huo?

Kama hakufanikiwa nianze kufuatilia. Na je taarifa za kufuatilia nianze na zipi . Mama alisharudi kijijini kwao hali mbaya familia yetu kwa ujumla hali mbaya. Anyway mama angekwa na elimu asingekubali kusainishwa nyaraka bila kujua lengo na athari za kufanya hivyo.
 
Una uhakika na hao ndugu zako lakini maana msimamizi wa morathi anakuja vp wakati mama enu mzazi alikuepo na tayari kaka zako wana miaka 18+
Ndio mkuu nipo nao bahati mbaya hawana elimu yoyote tumebaki kulalamika tu hasa tunapokumbwa na hali mbaya ya uchumi.
 
Kama imeshachukuliwa na saini zilipigwa unafikiri hata ukianzisha kesi itakuwaje..? Au mtaanzisha kesi ya madai dhidi yake..?
 
Kama imeshachukuliwa na saini zilipigwa unafikiri hata ukianzisha kesi itakuwaje..? Au mtaanzisha kesi ya madai dhidi yake..?
Mkuu nataka namna ya kuthibitisha tu je mtu yule alifanikiwa? Kama hakufanikiwa tuanze sasa
 
Ndio mkuu nipo nao bahati mbaya hawana elimu yoyote tumebaki kulalamika tu hasa tunapokumbwa na hali mbaya ya uchumi.
Huyo mtu bado ni msimamizi wa marathi mpaka sasa
 
Je siwezi kufika pale NSSF Dodoma wakanipa mawili matatu?
 
As long as mama Yako, yupo na alikuepo, basi qnajua kila kitu tena na kaka zako walikua na 18 kuendelea, waulize vizuri
Nisikudanganye mkuu kungekuwa na chochote ningejua tu. Hali yetu hakuwahi kubadilika toka baba alipoondoka. Hakuna msaada wowote uliotoka kwa ndugu baada ya kipindi hicho. Licha ya kuwa nilikuwa dogo lakini miaka 14 nisingeacha kukumbuka chochote kilichotokea. Nakumbuka kila kitu baba aneondoka ndugu wakatudhulumu ng'ombe wetu, nyumba yetu, na baadae tukashangaa huyo ndugu anatusogelea. Kumbe lengo ilikuwa kutumaliza zaidi
 
hatua unayoweza kuanza nayo.

Nikwenda mahakani ambako shauri la mirathi lilifunguliwa. Kwakua umesema aliwazungusha naamini unakumbuka baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na mahaka ambapo mirathi ilifunguliwa.

mahakama itakupatia taarifa juu ya mwenendo mzima kuanzia uteuzi ulivyofanyika, mali zilivyogawanywa kama kulikuwa na kufoji wanufaika utajua na jinsi mirathi ilivyofungwa.

Baada ya hapo utapata mwanga wanini kilijili. Then kama msimamizi alijinufaisha mwenyewe unaweza kumfungulia kesi ya madai yeye mwenye binafsi ikiwa mirathi ilishafungwa. Ili kudai vitu vyote alivyochukua.

NB: KUWA MSIMAMIZI WA MIRATHI SIO TIKETI YA KUJIMILIKISHA MALI ZA MAREHEMU NA KUMINYA HAKI ZA WARITHI HALALI.

KESI ZA MIRATHI ZINACHANGAMOTO NYINGI HAKIKISHA UNAJIDHATITI KWELI KWELI
 
Back
Top Bottom