Kuna wakati atataka kuuza kununua nyingine kupata wateja ni shida ww huoni dualis zilikuja Kasi saizi nyingi zimepaki[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Nitakupa jibu refu kidogo:
Anayewaza kuuza gari wakati wa kununua ni mlengaji.
Gari ni jambo binafsi sana, ukinunua unatengeneza attachment nalo, mpaka uje kuliuza limeshakupa huduma uliyokuwa unahitaji na kulitoa unalitoa kwa uchungu.
Gari lihudumie vizuri kiasi kwamba wanaokuzunguka walitake bila promotion.
Usinunue gari bovu, nunua jipya au used abroad with low km kisha toa huduma takatifu kwa kipindi chote cha maisha yenu.
Kuna wakati wanaokuzunguka wataanza kukusihi uwauzie kabla hata hujatangaza kuuza. Na bado kwa attachment uliyo nayo na gari lako utakuwa mzito maana kama ulilitunza unajua thamani yake.
Nimeshawahi kukutana na Nissan namba A dashboard inasoma km 600000. Na unakuta mtu ana service book. Historia yote ya service na parts replacement ipo kwenye kitabu. Unasoma kama hadithi tangu imenunuliwa mpaka ilipofika hapo ilipo.
Kuna mzee huko Arusha anatoka Asia nadhani, ana Suzuki vitara ambayo alinunua kipindi zimeanza ingia nchini, miaka hiyo. Hiyo gari ukiiona na historia yake na km zake ukiambiwa toa m10 nikupe kama unajua gari unatoa hapo hapo.
Huko Moshi kuna mzee ana benz tangu tupo watoto wadogo leo yeye sidhani kama anaona hata kuona ila benz ni mpyaaaa.
Vijana wa leo unaenda kununua gari unajiuliza siku ya kuuza itakuaje? Kwani unaanzisha biashara ya kuuza gari? Ukinunua na kuuza mambo mengine ya kimaendeleo utafanya sa ngapi? Si utakuwa kazi ni kukimbizana na ununuzi wa gari tu?
Kwa mazingira yetu maamuzi ya kununua gari, ukae nalo miaka m3 sijui uuze, ununue tena ukae miaka m4 uuze ni maamuzi yenye usumbufu wa muda na uchumi wako. Nunua gari, jipe 10 years za kufanya maendeleo mengine unless unasafiri sana na gari linachoka mapema.
Wenzetu wanabanwa na sheria kuendesha gari za zamani au km nyingi, na hii ni kibiashara zaidi sababu usiponunua jipya nani ataendesha mapya? otherwise kuna watu nje wangetunza magari yao na kufanya maintainance kubwa ili yadumu yaendelee kuwahudumia mpaka pale litakapohitajika kuzikwa kwa kufanyiwa recycling, kuyeyushwa na kutengeneza gari jipya.