Msaada gari yangu aina ya Toyota Passo inakula sana mafuta

grizzman

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2015
Posts
225
Reaction score
407
habari zenu wana ndugu,

nimejichanga changa nimenunua ka passo kwa mtu lkn cha kushangaza kinakula mafuta vibaya nikiweka mafuta lita 5 natoka kimara to tegeta nakurudi inakua imeisha mafuta tatizo nn wadau.
nakaribisha maoni yunu nashukrani
 
Maelezo yako hayajitoshelezi mkuu,hiyo gari umenunua Kwa mtu au yard? Pia ni namba A,B,C au D.
Ushauri wangu peleka Kwa fundi acheki:-
1) silence
2)badilisha air cleaner
3)rekebisha muffler/mafundi wanajua jinsi ya kurekebisha muffler utulie
4) weka plugs mpya
 
namba cys
 
mkuu tafuta boda au bajaj ndo itakufaa, wew gari huiwezi.
 
Sawa mkuu. Mara nyingi gari hula mafuta sana kama yakiwa mjini na hii ni kutokana na foleni za hapa mjini na kusimama simama mara kwa mara. Kwa hiyo ni kawaida kwa gari hilo kula mafuta.

Ukiwauliza watu wanaotumia magari kama brevis au mark x na crown watakuambia ulaji wake wa mafuta uko vipi
 
Kwa uzoefu tu engine ndogo kama hiyo 990cc sio suluhisho la gari kula vizuri mafuta, Pili Kimara to Tegeta kupitia mwenge ni 25 km x 2 ni 50 km /5ltrs =10 km per litre hayo ni matumizi kawaida na sio high way tena mazuri sana kwa gari ndogo za toyota, nyingi zipo hadi 7 to 9 km per litre?

Wakati mwingine huwa siwaelewi kabisa watanzania, au shule huwa tunaenda kufanya nini tena elimu ya darasa la nne tu, hapo usoni dash board inakuhesabia km kama ulitaka kuipima ilikujua ulaji ungeleta angalau viwango viwili kwamba toka kimara na kurudi nimetembea km 52 na nimetumia lita 5 maanake gari langu linatembea km 10.4 kwakila lita moja JE ULAJI HUU WADAU MNAUONAJE ? ? Usishangae ana diploma au hata degree.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…