Msaada - Gharama ya Kujenga Nyumba Hii..!!

OGOPASANA

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2009
Posts
262
Reaction score
144
Habari wakuu, naomba wenye ujuzi na uelewa katika maswala ya ujenzi na gharama za ujenzi wa nyumba mnisaidie makadilio ya gharama ya kujenga nyumba hii. Thank you in Advance.

NY001.jpgNY002.gifNY004.gifNY003.jpg
 
Inaweza kufika kama milioni 250
inategemea pia na aina na finishing materials!
 
Kama unaijenga kwenye kiwanja ambacho ni flat na barabara inafika mpaka kiwanjani, unahitaji mil 12 mpaka linta. Kislab kitakucost mil. 5. Kuezeka inategema na aina ya roofing materials utakazotumia. Kama utatumia bati za kawaida utahitaji mil. 3.5 kuezeka.
Kama utaweka grill na madirisha ya aluminium jumla itakucost 2.5 mil. Umeme iwapo hutahitaji kununua nguzo, kufanya wiring na kuvuta ni 2mil. Jumla mil. 25.
Hapo tayari unaweza kuhamia.

makorombwezo mengine ya tiles, ceiling, plastering and painting, plumbing, pavements, fencing, landscaping and gardening bei zake zina tofautiana mno kiasi kwamba haina maana kutoa kamadirio, unless uwe specif aina ya finishing unayotaka.
 
Gharama ya kujenga nyumba na finishing kabisa kwa kutumia wataalamu ni tzs 500,000 kwa kila square meter. Kwa hiyo jua ni square meter ngapi za sakafu unazo mara hicho kiwango. Usiogope, zinaonekana nyingi lakini ukiweka kiduchu kiduchu wala hautajua umemalizaje.
 
Habari wakuu, naomba wenye ujuzi na uelewa katika maswala ya ujenzi na gharama za ujenzi wa nyumba mnisaidie makadilio ya gharama ya kujenga nyumba hii. Thank you in Advance.
Unataka kuijenga wapi? Bei zinatofautiana sana kulingana na maeneo na kiwango cha ubora unachokihitaji (ikijumuisha utaalamu/wataalamu utakawatumia). Unataka kuijenga itokee kama inavyoonekana kwenye hiyo picha (materials, finishing etc)? Kwa kutizama hivyo vipimo kwa haraka, nyumba hiyo ina kama square metre 120. Kama unaweza kupata viwango vya bei (kwa sq m) kwa eneo unapotaka kujenga nyumba hiyo, unaweza kuzidisha kiwango hicho kwa eneo hilo la 120 sq m.

Kuna mchangiaji hapo juu ametoa kiwango cha TZS 500,000 per sq m (kwa Dar mimi naamini ipo juu zaidi hasa kama ni kwa kiwango kinachoonekana katika hiyo picha).

=> 120x500,000=60,000,000
 
Kama unaijenga kwenye kiwanja ambacho ni flat na barabara inafika mpaka kiwanjani, unahitaji mil 12 mpaka linta. Kislab kitakucost mil. 5. Kuezeka inategema na aina ya roofing materials utakazotumia. Kama utatumia bati za kawaida utahitaji mil. 3.5 kuezeka.
Kama utaweka grill na madirisha ya aluminium jumla itakucost 2.5 mil. Umeme iwapo hutahitaji kununua nguzo, kufanya wiring na kuvuta ni 2mil. Jumla mil. 25.
Hapo tayari unaweza kuhamia.

makorombwezo mengine ya tiles, ceiling, plastering and painting, plumbing, pavements, fencing, landscaping and gardening bei zake zina tofautiana mno kiasi kwamba haina maana kutoa kamadirio, unless uwe specif aina ya finishing unayotaka.

Ze marcopolo embu elezea kidogo unaezeka na nini majani au alafu magril plus alluminium for that price embu funguka kidogo how about electricity maelezo please
 
Kwa ramani hiyo itakuwa ina basement so kibongobongo bado
 
Ze marcopolo embu elezea kidogo unaezeka na nini majani au alafu magril plus alluminium for that price embu funguka kidogo how about electricity maelezo please

Mkuu, mbona kila kitu nimefafanua. Kuhusu kuezeka nisome vizuri. Kuhusu gril na aluminium inategemea design na atakayekutengenezea lakini 2,5 inaosha.
Kama kuna kitu hakiko clear sema tu mkuu tutajitahidi kufafanua zaidi...
 
Ukijinyima kula mihogo na tembele unajenga mbona
 
Mkuu, mbona kila kitu nimefafanua. Kuhusu kuezeka nisome vizuri. Kuhusu gril na aluminium inategemea design na atakayekutengenezea lakini 2,5 inaosha.
Kama kuna kitu hakiko clear sema tu mkuu tutajitahidi kufafanua zaidi...

Mkuu 2.5 ni figure tu njoo na mabati mangapi mbao kiasi gani na price pia fundi utampa ngapi hivyo hivyo na kwenye magrill
 
Mkuu gharama za Ando TIles sasa hivi zikoje? nataka kufanya roofing kwa kutumia Ando Tiles
 
Mkuu 2.5 ni figure tu njoo na mabati mangapi mbao kiasi gani na price pia fundi utampa ngapi hivyo hivyo na kwenye magrill

Kaka, kuezeka nimekadiria 3.5 but ukweli ni kwamba mtu hata akitaka kuezeka kwa mil 20 anaweza lakini option ya kutumia 3,5 kwa nyumba kama hii ipo. Mara nyingi huwa najaribu kutoa mahesabu ya chini kwa sababu angalau yenyewe yana uhakika zaidi kuliko kadirio la juu kwa sababu halina ceiling. Nimeshawahi kuezeka nyuma sq.m 120 kwa 2.8 mil kwa bati za kawaida gage 28. Bei ya fundi hapo ni sh. laki nane na 2 mil materials of which bati zilikuwa laki 9.5 the rest ni mbao na usafiri. Kwa hiyo nimeongeza laki saba na kukadiria 3.5 kwa sababu siku zimepita. By the way, haya ni makadirio tu, siku zote gharama halisi hujulikana kazi ikianza. Cha msingi ni kwamba makidirio yasiwe mbali sana na uhalisia.
 
Kama unaijenga kwenye kiwanja ambacho ni flat na barabara inafika mpaka kiwanjani, unahitaji mil 12 mpaka linta. Kislab kitakucost mil. 5. Kuezeka inategema na aina ya roofing materials utakazotumia. Kama utatumia bati za kawaida utahitaji mil. 3.5 kuezeka.
Kama utaweka grill na madirisha ya aluminium jumla itakucost 2.5 mil. Umeme iwapo hutahitaji kununua nguzo, kufanya wiring na kuvuta ni 2mil. Jumla mil. 25.
Hapo tayari unaweza kuhamia.

.
mkuu hii si kweli unajidanganya na kutudanganya!
 
Watu wengi huwa wanaogopa kujenga kwa sababu wamezoea kuona figure za mamia ya mamilioni.
Ingekuwa hivyo, mafundi cherahani wasingekuwa wanamiliki nyumba Kinondoni, Tandika na kwingineko.
Ukisimamia kazi yako vizuri unaweza kujenga kwa gharama ya kawaida tu...

Hii nyumba wengi wenu inawachanganya kwa sababu ni storey house, lakini mnachotakiwa kujua ni kwamba ujengwaji wa storey house yenye upper level ndani ya paa ni tofauti na ujengaji wa ghorofa la kawaida. Katika ujenzi wa nyumba kama hii kwanza matofauti hauina ulazima wa kuyalaza, pili slab yake haina sababu ya kuwa strong sana kwa sababu inabeba watu tu, actually kuna nyumba nyingine kama hizo hawaweki slab ila wanaweka mbao tu. Yaani hiyo upper level ni kwamba vyumba vipi darini sio kwamba unajenga tena level nyingine.
 
Hello wana JF.. leo nimeona nitoe mchango kidogo juu ya hii mada ya Ogopasana kwani nina ufahamu kiasi na sekta ya ujenzi kwa kuwa mimi na msanifu majengo/architect in training...

kwanza, picha na ramani ulizotoa hazijitoshelezi kimaelezo kutoa gharama halisi ya ilo jengo.

pili: kuna vitu vingi vinavyoathiri gharama vya kuangalia unapopandikiza nyumba iliyokusudiwa kujenga sehemu 1 ya mazingira pekee na kuipeleka mahali pengine mf. msingi wa nyumba, upatikanaji wa vifaa, wajenzi na technologia.

Tatu: mazingira Vs comfortability ya site.. ujenzi na uchaguzi wa materials utategemea mazingira ya site vitu kama mvua, joto, baridi, unyevunyevu na hali ya udongo vitachangia comfortability ndani ya nyumba yako na kwa upande mwingine gharama.

maoni yangu: toa maelezo zaidi kuhusu eneo unalotaka kujenga na mazingira yake.
pia kwa haraka haraka nimeona kuna beams na columns zikiashiria kwamba kuna slab ya zege, kuta za nyumba nazo zimewekwa cladding materials, halafu ukiangalia ngazi za porche ni za mbao; kwa haraka naeza sema material zilizotumika kwa kiasi kikubwa ni mbao, tofali kiasi, zege, claddings na mouldings..

ps: milioni 250 ni exaggeration ya over estimation. lol
 
Kama unaijenga kwenye kiwanja ambacho ni flat na barabara inafika mpaka kiwanjani, unahitaji mil 12 mpaka linta. Kislab kitakucost mil. 5. Kuezeka inategema na aina ya roofing materials utakazotumia. Kama utatumia bati za kawaida utahitaji mil. 3.5 kuezeka.
Kama utaweka grill na madirisha ya aluminium jumla itakucost 2.5 mil. Umeme iwapo hutahitaji kununua nguzo, kufanya wiring na kuvuta ni 2mil. Jumla mil. 25.
Hapo tayari unaweza kuhamia.

makorombwezo mengine ya tiles, ceiling, plastering and painting, plumbing, pavements, fencing, landscaping and gardening bei zake zina tofautiana mno kiasi kwamba haina maana kutoa kamadirio, unless uwe specif aina ya finishing unayotaka.
Safi sana
 
Back
Top Bottom