Msaada: Hii vita mimi na Wife

Msaada: Hii vita mimi na Wife

Kwa chemistry ya kifamilia, hili halitakiwi.

Ni sheria tu inapita, taarifa ya habari haina discussion, nikiwa home ni lazima tuangalie.
Elimu hii nimeshafika lakini imeshindikana...yaani,kutumia nguvu sio poa.
 
mwache wife aangalie tamthilia zake

kama tibici wakati mwingine wanakinaishaga kwa akina mama
 
Ndio shida ya mwanaume kuwahi kurudi nyumbani hiyo, leo mnagombania remote kesho mtaanza kugombana wenyewe.

Karibu counter mkuu.






Let's meet at the top, cheers 🥂
 
Elimu hii nimeshafika lakini imeshindikana...yaani,kutumia nguvu sio poa.

Ulichelewa mkuu, huwezi kuibadilisha kwa sasa.

Unachotakiwa kufanya tafuta kijiwe cha kuangalizia taarifa.

That is very simple, tena unaaga au unatoa taarifa kwamba naangalia taarifa ya habari. Akikuhitaji mwambie kama taarifa iko nakuja home.
 
Kwa kweli Sijui niwalaumu hawa wamiliki wa Tv stations au sijui nifanyeje! Ninapokuwa home vita ni kali sana mpaka tunanuniana...Kwa Akili ya remote. Wife yeye hachoki kuangalia Tamthilia mimi nataka Taarifa ya Habari,mbaya zaidi muda wa kipindi ni mmoja! Halafu nimegundua wanaongalia Tamthilia nao Akili zao km sisi washabiki wa mpira hawataki kuhadithiwa yaani ni Hatari.
Shida hapo mmeoana badala ya wewe kuoa! Wanaume siku hizi mbona tumepungua hivi!?
 
Taarifa ya habari ni undisputed, hata kama siangalii, muda ukifika weka taarifa waliopo waangalie.

Hilo unatakiwa uliweke toka siku ya kwanza mnaanza kukaa pamoja au siku ya kwanza mnanunua TV.

Halina ubishi hili.

Mleta mada kaongelea yeye na mke,suala la muda wa habari kufika iwekwe channel yenye habari hata kama waliopo hawataki kuangalia hilo halipo....sio lazima
 
Sio kutofautiana mkuu bali tumebaki wachache kama sio kuisha
Kwani humu kunatakiwa thread za aina gani,za wanaume? Lakini mbona watu wananipa ushauri tuu fresh...Nyie wengine mngekuwa mods. Humu mngebaki wenyewe tu kwa uchaguzi wenu!
 
Baada ya mama mtoto kusafiri hii inaenda wiki ya pili tv haijawashwa.

Kutokana na namna yangu ya kuhustle ni kuzurura na kurudi nyumbani usiku saa tano au sita mimi siyo rafiki wa tv.

So ninapoona hapa kuna mtu anagombea tv na mkewe hebu otea namchukuliaje...
 
Mleta mada kaongelea yeye na mke,suala la muda wa habari kufika iwekwe channel yenye habari hata kama waliopo hawataki kuangalia hilo halipo....sio lazima

Unless nimehamia kwa mke wangu, au mimi ni baba wa nyumbani.

Otherwise hilo halina discussion na halitakiwi kuwa na discussion.
 
Mmoja wenu ajitolee kuangalia kipindi kwenye simu ..huo mgogoro utaisha.
 
Kwani humu kunatakiwa thread za aina gani,za wanaume? Lakini mbona watu wananipa ushauri tuu fresh...Nyie wengine mngekuwa mods. Humu mngebaki wenyewe tu kwa uchaguzi wenu!
Hamna brooo usimind. Lakini hili ni jambo dogo sana kama mwana mume kuli solve. Kakini pia unategemea na mtu na mtu
 
Back
Top Bottom